Swali
Maombi ni nini?
Jibu
Fasili ya msingi zaidi ya maombi ni “kuzungumza na Mungu.” Maombi sio kutafakari au kuwaza tu; ni mazungumzo ya moja kwa moja na Mungu. Ni mawasiliano ya nafsi ya mwanadamu na Mungu aliyeiumba nafsi hiyo. Maombi ndiyo njia kuu ya muumini katika Yesu Kristo anawasilisha hisia zake na matamanio yake kwa Mungu na kuwa na ushirika na Mungu.
Maombi yanaweza kuwa ya sauti au ya kimya, ya kibinafsi au ya faragha, ya rasmi au yasiyo ya rasmi. Maombi yote lazima yatolewe kwa imani (Yakobo 1:6), katika jina la Bwana Yesu (Yohana 16:23), na katika uwezo wa Roho Mtakatifu (Warumi 8:26). Maombi ya Kikristo yanaelekezwa kwa Mungu wa Utatu wa Biblia. Tunaomba kwa Baba kupitia Mungu Mwana, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Waovu hawana hamu ya kuomba (Zaburi 10:4), lakini watoto wa Mungu wana hamu ya asili ya kuomba (Luka 11:1).
Sala inayofafanuliwa katika Biblia kuwa kutafuta kibali cha Mungu (Kutoka 32:11), kummiminia Bwana nafsi yako (1 Samweli 1:15), kuelekeza kilio chako mbinguni (2 Mambo ya Nyakati 32:20), kumkaribia Mungu (Zaburi 73:28), na kupiga magoti mbele ya Baba (Waefeso 3:14).
Paulo aliandika hivi: “Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu” (Wafilipi 4:6-7). Usijisumbue kwa jambo lolote; omba kwa ajili ya kila jambo.
Kila kitu? Naam, Mungu anatutaka tuzungumze Naye kuhusu kila jambo. Tunapaswa kuomba mara ngapi? Jibu la kibliblia ni ”ombeni bila kukoma” (1 Wathesalonike 5:17). Tunapaswa kuendeleza mazungumzo na Mungu siku nzima. Tunaweza kuomba chini ya hali yoyote. Maombi yanakuza uhusiano wetu an Mungu na yanadhihirisha imani yetu na kumtegemea Mungu kabisa.
Maombi ni njia ya Mkristo ya kuwasiliana na Mungu. Tunaomba ili kumsifu Mungu na kumshukuru na kumwambia jinsi tunavyompenda. Tunaomba kufurahia uwepo wake na kumwambia kile kinachoendelea katika maisha yetu. Tunaomba ili kufanya mahitaji yajulikane na kutafuta mwokozo na hekima ya Mungu. Mungu anapenda mawasiliano haya na watoto wake, kama vile tunavyopenda mawasiliano na watoto wake, kama vile tunavyopenda mawasiliano tuliyo nayo na watoto wetu. Ushirika na Mungu ndio kiini cha maombi. Mara nyingi tunapoteza ufahamu wa jinsi maombi yanavyostahili kuwa.
Wakati tunamjulisha Mungu haja zetu, tunamruhusu Mungu kujua mahali tunasimama na kile ambacho tungependa kitendeke. Katika maombi yetu, ni lazima tukubali kwamba Mungu ni mkuu kutuliko na hatimaye anajua kilicho bora katika hali yoyote ile (Warumi 11:33-36). Mungu ni mwema na anatuomba tumwamini. Katika sala, tunasema, kimsingi, “Si mpenzi yangu, bali mapenziyako yatimizwe.” ufunguo wa maombi yaliyojibiwa ni kuomba kulingana na mapenzi ya Mungu na kulingana na Neno lake. Maombi si kutafuta mapenzi yetu wenyewe bali ni kutafuta kujipatanisha na mapenzi ya Mungu kikamilifu zaidi (1 Yohana 5:14-15; Yakobo 4:3).
Biblia ina mifano mingi ya maombi na wingi wa himizo kuomba (ona Luka 18:1; Warumi 12:12; na Waefeso 6:18). Nyumba ya Mungu inafaa kuwa nyumba ya maombi (Marko 11:17), na watu wa Mungu wanapaswa kuwa watu wa kuomba: “Lakini ninyi wapendwa, jijengeni katika imani yenu iliyo takatifu sana tena ombeni katika Roho Mtakatifu. Jilindeni katika upendo wa Mungu” (Yuda 1:20-21).
English
Maombi ni nini?