settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu anayaruhusu maovu kuwapata watu wazuri?

Jibu


Hili ni mojawapo la maswali magumu katika uchanganusi wa bibilia. Mungu ni wa milele, hana mwisho, anajua kila kitu, ako kila mahali na ako na nguvu kuliko mtu yeyote au kitu chochote. Ni kwa nini wanadamu (hawaishi milele, hawajui mambo yote, hawako kila mahali, hawana nguvu zote) wanatarajia kuelewa njia za Mungu? Kitabu cha Ayubu kinashugulikia hali hii. Mungu alimuruhusu shetani kufanya chochote alichokitaka kwa Ayubu lakini si kumuua. Je Ayubu alifanya nini? “Tazama, ataniua; sina tumaini; Ila hata hivyo nitaithibitisha njia yangu mbele yake” (Ayubu 13:15). “Akasema, Mimi nilitoka tumboni mwa mama yangu nili uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe.” (Ayubu 1:21). Ayubu hakuelewa ni kwa nini Mungu alimuruhusu shetani afanye aliyoyafanya, lakini alijua Mungu ni mwema na kwa hivyo aliendelea kumtumainia. Hatimaye hiyo yatupasa tuwe na msimamo kama huo.

Ni kwa nini maovu yanawapata watu wema? Jibu la kibibilia ni, hakuna watu “wema”. Bibilia inaifanya kuwa wasi kabisa kwamba, wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu (Mhubiri 7:20; Warumi 6:23; 1Yohana 1:8). Warumi 3:8-18 haiweki vizuri kama hakutakuwa na watu wenye “haki” “kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Simu ya fira i chini ya midomo yao. Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawakuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.” Kila mwanadamu chini ya nyota hii anastahili kutubwa jehanamu kwa wakati huu. Kila nukta ya dakika tunapokuwa na uai ni kwa neema na rehema za Mungu. Hata tunapo pitia machungu katika nyota hii, Mungu ni wa huruma tukilinganisha na tunayostahili ambayo ni jehanamu ya milele, ziwa la moto.

Swali nzuri laweza kuwa “Ni kwa nini Mungu anayaruhusu mazuri kuwatokea waovu?” Warumi 5:8 yasema, “Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.” Mbali na uovu, unyonge, na hali ya dhambi ya watu wa ulimwengu huu, Mungu bado atupenda. Anatupenda ya kutosha hadi kufa ili achukue hukumu ya dhambi zetu (Warumi 6:23). Tukimpokea Yesu kama Mwokozi wa maisha yetu (Yohana 3:16; Warumi 10:9), tutasemehewa na tuaidiwe mji wa milele mbinguni (Warumi 8:1). Tunachostahili ni jehanamu. Na chenye tumepewa ni uzima wa milele kama tutakuja kwa Yesu kwa imani.

Naamu, wakati mwingine mambo maovu huwapata watu wanaoneka hawastahili kuyapata. Lakini Mungu huyaruhusu hayo kutokea kwa kusudio lake, haijalishi kama tunayaelewa. Fauka (zaidi) ya hayo, kwa hivyo lazima tukumbuke kuwa Mungu ni mwema, mwenye haki, na ni wa huruma. Kila mara mambo hutupata yenye hatuwezi kuelewa sababu. Ingawa badala ya kuushuku wema wa Mungu, jukumu letu liwe kumtumainia Mungu. “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako” (Mithali 3:5-6).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu anayaruhusu maovu kuwapata watu wazuri?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries