settings icon
share icon
Swali

Je, mapepo ni malaika walio anguka?

Jibu


Wakati hasa Mungu aliumba malaika ni wazi kwa mjadala, lakini chenye kinajulikana hasa ni kwamba Mungu aliumba kila kitu kikiwa kizuri kwa sababu Mungu, katika utakatifu wake, hawezi kuumba kitu kilicho na dhambi. Hivyo wakati Shetani, ambaye mara nyingine alikuwa Ibilisi, aliasi dhidi ya Mungu na akaanguka kutoka mbinguni (Isaya 14; Ezekiel 28), thuluthi moja ya jeshi la malaika walijiunga na uasi wake (Ufunuo 12:3-4, 9). Hakuna shaka malaika hawo walio anguka ndio sasa wanajulikana kama mapepo.

Tunajua kwamba kuzimu iliandaliwa shetani na malaika zake, kwa mujibu wa Mathayo 25:41: " Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa kushoto, 'Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na maliak zake." Yesu, kwa kutumia neno la umilikaji "wake" anaweka wazi kwamba malaika hao ni mali ya Shetani. Ufunuo 12:7-9 inaeleza nyakati za mwisho vita vya kimalaika kati ya Mikaeli na "malaika zake" na shetani na "malaika zake." Kutokana na hayo na mistari sawa nah ii ni wazi kwamba mapepo na malaika walioanguka ni sawa.

Baadhi hukataa wazo kwamba mapepo ni malaika walioanguka kutokana na ukweli kwamba Yuda mstari wa 6 inasema malaika waliokosa "atafungwa minyororo ya milele." Hata hivyo, ni wazi kwamba si wote wa malaika waliokosa "wamefungwa," jinsi Shetani bado ako huru (1 Petro 5:8). Kwa nini Mungu kuwafunga malaika wengine walioanguka, lakini kuruhusu kiongozi wa uasi kubaki huru? Inaonekana kwamba Yuda mstari wa 6 inamrejelea Mungu kuwalazimu malaika walio anguka, walioasi katika njia ya ziada, kuna uwezekano "wana wa Mungu" tukio katika Mwanzo sura ya 6.

Mbadala wa kawaida maelezo kwa asili ya mapepo ni kwamba wakati Wanefili wa Mwanzo 6 waliharibiwa katika mafuriko, nafsi yao iliyoharibiwa ikawa mapepo. Wakati Biblia haisemi hasa ni nini kilichotokea kwa nafsi za Nefili wakati wao waliuawa, kuna uwezekano kwamba Mungu bila kuharibu Nefilimu katika mafuriko na kuruhusu roho zao kusababisha mabaya hata zaidi kama mapepo. Maelezo thabiti ya kibiblia kwa ajili ya asili ya mapepo ni kwamba wao ni malaika walioanguka, na malaika waliomwasi Mungu na Shetani.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, mapepo ni malaika walio anguka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries