settings icon
share icon
Swali

Je! Kuna malaika wangapi?

Jibu


Ni malaika watatu pekee wametambuliwa katika Biblia. Gabrieli (Danieli 8:16), Mikaeli mlaika mkuu (Danieli 10:13), Ibilisi malaika aliyeanguka (Isaya 14:12). Hata hivyo malaika viumbe wametajwa mara 273 katika vitabu 34 vya Biblia. Ingawa hatujui hasa ni malaika wangapi waliopo, tunajua kutoka kwa Maandiko kwamba kuna idadi kubwa ya malaika.

Kitabu cha Waebrania kinaelezea umati wa malaika mbinguni ambao ni wengi sana kuhesabika: “Lakini ninyi mmekuja Mlima Sayuni, Yerusalemu ya mbinguni, mji wa Mungu aliye hai. Mmekuja penye kusanyiko kubwa la malaika maelfu kwa maelfu wasiohesabika wanaoshangilia” (Waebrania 12:22). Hii taswira inapanuliwa katika kitabu cha Ufunuo: “Kisha nikatazama, nikasikia sauti za malaika wengi wakiwa wamekizunguka kile kiti cha enzi, pamoja na wale viumbe wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne. Idadi yao ilikuwa kumi elfu mara kumi elfu na maelfu ya maelfu” (Ufunuo 5:11).

Ingawa Biblia haijataja hususani idadi ya malaika, wengine wanaamini kwamba kunaweza kuwa na malaika wengi zaidi ya idadi kamili ya wanadamu katika historia yote. Nadharia hii msingi wake uko katika Mathayo 18:10: “Angalia ili usimdharau mmojawapo wa hawa wadogo, kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba yangu aliye mbinguni” Kifungu hiki kinaonekana kupendekeza kwamba watu binafsi, au angalau watoto, wako na malaika walinzi wa kuwalinda. Kuna uwezekano kwamba Yesu alikuwa anazungumza hapa kwa njia ya jumla kuhusu jukumu la malaika kuwa walinzi kwa watoto. Kwa njia yoyote ile, Maandiko yako wazi kwamba malaika huwa wanawalinda na kuwakinga wanadamu (Zaburi 34:7;91:11-12; Mathayo 18:10; Matendo 12:9-15).

Biblia inaelezea aina mbalimbali za malaika. Malaika wengine-makerubi na maserafi-wameelezewa kuwa viumbe walio na mabawa. Makerubi hasa wanahudumu katika kiti cha enzi cha Mungu kama walinzi, huku ikionekana kuwa maserafi wanatumika katika kuabudu mbele za kiti cha enzi (Ezekieli 1:4-28; 10:1-22; Isaya 6:2-6). Biblia inazungumzia malaika wa nuru (2 Wakorintho 11:14) na malaika walioanguka (2 Petro 2:4; Yuda 1:6).

Katika Biblia malaika hutekeleza majukumu mbalimbali. Malaika wengine na wajumbe wa Mungu (Danieli 4:13). Malaika wengine ni wahudumu wa Mungu (Zaburi 103:20; Waebrania 1:7; Zaburi 104:4). “Malaika walinzi” wametajwa katika kitabu cha Danieli (Danieli 4:13,17,23). Mara nyingi malaika wameelezewa kuwa “kundi” la majeshi wa mbinguni (Yeremia 5:14; 38:17; 44:7; Hosea 12:5). Nyakati zingine malaika huitwa “wana wa mwenye nguvu” (Zaburi 89:6) au “wana wa Mungu” (Ayubu 2:1).

Vifungu vichache vya Maandiko vinaelezea malaika kama nyota (Ufunuo 9:1; 12:4; Ayubu 38:7-8; Danieli 8:10; Waamuzi 5:20). Wazo la nyota linaweza kutupa kidokezo bora zaidi cha ni idadi gani ya malaiko waliopo. Ikiwa malaika ni wengi mno kama nyota wa angani, basi wao ni wengi kuhesabika. Musa anasema katika Kumbukumbu 33:2 kwamba Bwana alikuja kuzungumza naye katika mlima Sinai pamoja na malaika “watakatifu makumi elfu.” Idadi kubwa mno inaeza kuwa ngapi? Ufafanusi wa kimsingi wa neno “isiyohesabika” kama kivumishi ni “idadi kubwa,” au “kubwa mno.” Zaburi 68:17 inasema kuwa malaika wa Mungu wemehesabika kuwa “ni makumi ya maelfu, na maelfu ya maelfu.” Kwa wazi mwandishi ana ugumu katika kukadiria idadi kamili ya malaika walioko.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kuna malaika wangapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries