settings icon
share icon
Swali

Malaika wakuu in akina nani?

Jibu


Neno "malaika mkuu" hutokea katika mistari miwili ya Biblia. Wathesalonike wa kwanza 4:16 inashangaa, "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza." Yuda mstari wa 9 inasema, " Lakini Mikaeli malaika mkuu aliposhindana na Ibilisi, na kuhojian naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu, bali alisema, Bwana na akukemee." Neno "malaika mkuu" linatokana na neno la Kigiriki lenye maana ya "malaika mkuu." Linahusu malaika ambao anayeonekana kuwa kiongozi wa malaika wengine.

Yuda mstari wa 9 inatumia kihuzishi dhahiri "malaika mkuu Mikaeli," ambayo inaweza kuonyesha kwamba Mikaeli ni malaika mkuu tu. Hata hivyo, Danieli 10:13 inaeleza Mikaeli kama "mmoja wa hao wakuu." Hii huenda inaonyesha kwamba kuna malaika mkuu zaidi ya moja, kwa sababu inamweka Mikaeli kuwa juu ya kiwango sawa kama wengine "wakuu." Hiku kuwa na uwezekano kwamba kuna Malaika wengi, ni bora tusipuuze neno la la Mungu kwa kutangaza malaika wengine kama Malaika. Danieli 10:21 inamweleza Mikaeli malaika kama "mkuu," na Danieli 12:1 inabainisha Mikaeli kama "mkuu ambaye analinda." Hata kama kuna Malaika wengi, inaonekana kwamba Mikaeli ni mkuu kati yao.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Malaika wakuu in akina nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries