settings icon
share icon
Swali

Majira ya Kanisa ni nini? Je, majira ya kanisa yanafaa wapi katika historia ya Biblia?

Jibu


“Enzi” ni kipindi cha kihistoria cha wakati fulani au enzi. Baadhi ya wanahistoria hugawa historia ya mwanadamu katika enzi nyingi na kuzipa majina kulingana na sifa zao zinazozitambua: Enzi ya Kati, Enzi ya sasa, Enzi ya Baadaye, nk. Historia ya Kibiblia inaweza kugawanya katika enzi tofauti. Wakati sehemu hizo husisitiza jinsi Mungu uhusiana na uumbaji Wake, tunauita vipindi. Kwa upana zaidi, historia ya Biblia inaweza kugawanywa katika vipindi viwili, takribani kufuatia mgawanyiko wa Agano la Kale na Agano Jipya: Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema.

Enzi ya Kanisa ni kipindi cha muda kutoka siku ya Pentekote (Matendo 2) hadi unyakuzi (1 Wathesaloniki 4:13-18). Inaitwa Enzi ya Kanisa kwa sababu inashika kipindi ambacho kanisa litakua duniani. Hii inalingana na kipindi cha Neema. Katika historia ya kinabii, itakuwa kati ya majuma 69 na 70 ya Danieli (Danieli 9:24-27; Warumi 11). Yesu alitabiri Enzi ya kanisa katika Mathayo 16:18 wakati alisema, ”nitalijenga kanisa langu.” Yesu ametimiza ahadi yake, na Kanisa Lake sasa limekuwa likikua kwa takribani miaka 2000 sasa.

Kanisa linaundwa na watu ambao kwa imani wamemkubali Kristo Yesu kama Bwana na Mwokozi wao (Yohana 1:12; Matendo 9:31). Kwa hivyo, kanisa ni watu na siyo madhehebu au majengo. Ni Mwili wa Kristo ambao Yeye ndiye kichwa chake (Waefeso 1:22-23). Neno la Kigiriki eklesia, ambalo limetafsiriwa “kanisa” linamaanisha “kusanyinko lililoitwa.” Kiupeo kanisa ni la kilimwengu lakini hukutuna katika makundi madogo madogo.

Enzi ya Kanisa inajumuisha kipindi kizima cha Neema. “Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Mose, lakini neema na kweli imekuja kupitia Yesu Kristo” (Yohana 1:17). Kwa mara ya kwanza katika historia, Mungu kwa hakika anadumu ndani ya viumbe vyake, milele na milele. Katika nyakati zingine Roho Mtakatifu kila mara alikuwepo, na kuwa kazini kila mara, lakini Angewashukia watu kwa muda (k.m. 1 Samueli 16:14). Enzi ya Kanisa inatabulishwa na Roho Mtakatifu kudumu kwa watu siku zote (Yohana 14:16).

Maandiko yanatofutisha kati ya taifa la Israeli na Kanisa (1 Wakorintho 10:32). Kunao mwingiliano fulani kwa sababu, kibinafsi Wayahudi wengi wanamwamini Yesu kama Masihi wao na kwa hiyo wao ni sehemu ya Kanisa. Lakini ahadi ya Mungu na taifa la Israeli bado hazijatimizwa. Ahadi hizo zinangoja kutimizwa katika wakati wa Ufalme wa Milenia, baada ya Enzi ya Kanisa kukamilika (Ezekieli 34:37; 45; Yeremia 30; 33; Mathayo 19:29; Ufunuo 19).

Enzi ya Kanisa itatamatika wakati watu wa Mungu wamenyakuliwa kutoka ulimwengu na kuchukuliwa kuwa na Bwana (1 Wakorintho 15:51-57). Unyakuzi utafuatwa na chakula cha harusi ya mwana kondoo huko mbinguni (Ufunuo 19:6-9) kama kanisa, Bibi-arusi wa Kristo, atakapopokea taji yao ya mbinguni. Hadi wakati huo, Kanisa linaendelea kuwepo kwa tumaini, likihimizwa “simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure” (1 Wakorintho 15:58).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Majira ya Kanisa ni nini? Je, majira ya kanisa yanafaa wapi katika historia ya Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries