settings icon
share icon
Swali

Je! Majina ya Shetani ni yapi?

Jibu


Shetani ni kiumbe wa kiroho ambaye aliongoza uasi mbinguni dhidi ya Mungu na hatimaye kutupwa duniani (Luka 10:18). Jina lake la kibinafsi, “Shetani,” linamaanisha “adui.” Jina hili linaonyesha asili ya msingi ya Shetani: yeye ni adui wa Mungu, kwa yale yote Mungu anafanya and yale yote Mungu anapenda.

Pia anaitwa “shetani” katika Agano Jipya. Neno “Ibilisi” linamaanisha “mshtaki wa uwongo” au “mkashifu.” Shetani anatekeleza jukumu hili katika Ayubu 1-2 anapoishambulia tabia ya Ayubu.

Katika Mathayo 12:24, Wayahudi wanamrejelea Shetani kuwa “Beelzebuli,” neno lilitokana na “Baal-zebu” (“bwana wa inzi”), mungu wa uwongo wa Wafilisti huko Ekroni (2 Wafalme 1:2-3,6)

Majina mengine vyeo ya Shetani ni pamoja na mjaribu (1 Wathesalonike 3:5), yule mwovu (Mathayo 13:19, 38), mkashifu wa waumini (Ufunuo 12:10), mungu wa dunia hii (2 Wakorintho 4:4), na mkuu wa uwezo wa anga (Waefeso 2:2). Wakorintho wa pili 11:14 inasema kwamba Shetani hujigeuza na kuwa “malaika wa nuru,” maelezo amabayo yanaonesha uwezo na madhumuni yake ya kudanganya.

Kuna vifungu kadhaa vinavyorejelea hukumu ya wafalme wa dunia hii lakini pia vinaweza rejelea Shetani. Cha kwanza ni Isaya 14:12-15. Hii inamzungumzia mfalme wa Babeli (aya ya 4), lakini maelezo pia yanaonekana kufaa sana yale ya kiumbe mwenye nguvu zaidi. Jina “Ibilizi,” ambalo linamaanisha “nyota ya asubuhi,” limetumika hapa ili kuelezea mtu ambaye alitafuta kupindua kiti cha enzi cha Mungu.

Kifungu cha pili ni Ezekieli 28:1-19, ambacho kinamzungumzia mfalme wa Tiro. Kama vile ilivyo katika kifungu cha “Ibilisi” unabii huu una maneno ambayo yanaonekana kuzidi maelezo ya mwanadamu wa kawaida. Mfalme wa Tiro anasemekana “kutiwa wakifu kama mlinzi wa kerubi,” lakini alishushwa chini kwa kiburi yake na “kufukuzwa” na Mungu Mwenyewe.

Fauka ya kutoa majina na vyeo ya Shetani, Biblia inatumia mafumbo mbalimbali kuonyesha tabia ya adui. Yesu katika mfano wa dongo nne, anamfananisha Shetani na ndege wanaonyakua mbegu iliyoanguka katika ardhi ngumu (Mathayo 13:4, 19). Katika mfano mwingine, Shetani anaonekana akiwa mpanzi wa magugu kati ya ngano (Mathayo 13:25,28). Shetani anafananishwa na mbwa mwitu katika Yohana 10:12 na simba anayenguruma katika 1Petro 5:8. Katika Ufunuo 12:9, Shetani “yule nyoka wa zamani aitwaye ibilisi … Shetani”-kwa wazi inamrejelea yule joka ambaye alimdanganya Hawa (Mwanzo 3:1).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Majina ya Shetani ni yapi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries