settings icon
share icon
Swali

Maarifa yasiyohitaji ushahidi (ya kweli yasiyotegemea uzoefu au uchunguzi wa awali)(priori), kutoka kwa kile kilicho cha baadaye(posteriori), hoja yenye nguvu(fortiori)

Jibu


Katika falsafa, maarifa yanaainishwa kulingana na iwapo yanatoka katika kanuni za kimantiki za kilimwengu au inategemea uzoefu maalum na ushahidi. Tofauti kati ya hizi ni pana mno na huweka kikomo kati ya maarifa yasiyohitaji ushahidi na maarifa yatokanayo na kile kitakachotokea baadaye. Wakati kauli inaweza kutathminiwa kwa kina kupitia mantiki au ukweli wa watu wote ni dhana inayotokana na kile kilicho cha baadaye. Wakati tamko linahitaji uchunguzi maalum au maarifa ili litathminiwe, hii ni dhana ya maarifa yasiyohitaji ushahidi. Vile vile hii inatumika katika “mabishano” ya kifalsafa ambayo pengine yanaungwa na akili au yanahitaji data/habari ya majaribio.

Priori inamaanisha “kutoka mbeleni.” Maarifa yanafafanuliwa kuwa kuwapo tangu hapo nyuma huku yakiweza kuthibitishwa bila majaribio ya ushahidi, uzoefu, au uchunguzi. Kwa maneno rahisi, maarifa ya priori ni yale ambayo yanaweza kupatikana tu kupitia kwa mantiki. Kwa mfano, “miduara sio miraba” na “kapera ni mtu hajaoa” ni mirudiorudio ambayo hujulikana kuwa ya kweli kwa sababu hii kweli kulingana na ufafanuzi wao. Inachukuliwa kuwa kauli za mbeleni. Hilo hilo pia hutumika katika kauli za hisebati kama vile 2+2=4.

Neno posteriori linamaanisha “kutoka kwa kile cha baadaye/mwisho.” Maarifa yanaelezewa kuwa ya posteriori wakati tu pekee yanaweza patikana kupitia uzoefu au majaribio mengine. Kwa ufupi, maarifa ya posteriori na yale ambayo yanaweza kuwa ya kweli au ya uwongo tukizungumza kimantiki, na kwa hivyo lazima yatathminiwe kwa kutumia uchunguzi halisi. Kauli “Yohana ni kapera” haiwezi kuthibitishwa kwa kutumia mantiki; tunahitaji kuchunguza ukweli dhabiti kumhusu Yohana ili kujua ikiwa kauli hii ni kweli au la. Vile vile, “Niko na dola tano kwa mfuko” ni tamko ambalo linaweza kuwa kweli au la uwongo; linaweza thibitishwa au kukanushwa kupitia njia za kitaalamu.

Ni muhimu kutambua kwamba maarifa ya priori sio lazima itolewe kiukamilifu kupitia mantiki, angalau kwa suala la mjadala fulani. Hoja inayohusika inahitaji kuthibitishwa au kutupiliwa mbali kupitia mantiki pekee. Pindi ukweli fulani au wazo linasingatiwa kuwa la “kweli” kwa makusudi ya bishano, basi hoja ya baadaye inaweza tathminiwa kwa ukamilifu kulingana matokeo ya kimantiki ya wazo hilo. Kwa mfano, ikiwa pande zote za mabishano zinakubali kwamba “Yohana alikuwa Kansas mnamo tarehe mosi mwezi wa tatu” kuwa tamko la kweli, basi tamko “Yohana hakuwa katika mwezi mnamo tarehe 2” pia itachukuliwa kuwa kweli, kwa ajili ya mjadala huo.

Tambua kuwa kauli ya pili inaelezeka vizuri sana kana kwamba ni hitaji kimantiki likipewa nafasi ya kwanza. Hii ndio sababu inaweza kuitwa “priori ya kweli.” Ikiwa kauli ya kwanza ni kweli, ya pili inaweza kuthibitishwa yote zima kwa misingi ya mantiki, na sio kwa ukweli wowote ulioongezwa. Hii ndio maana halisi ya priori: “kutokana na lile la kwanza.” Kwa sababu tumekubali kauli ya kwanza kuwa ya kweli, kimantiki, basi kimantiki ni lazima tukubali ile ya pili.

Tofauti kati ya priori na posteriori huwa muhimu wakati unajaribu kuthibitisha au kukanusha dhana fulani. Hatua ya kwanza, kwa jumla ni kuchunguza dai la uthibitisho wa priori kuwa ni kweli- kwa ufupi je, inajirejelea au ni ya manufaa kimantiki? Ikiwa ni hivyo, basi “imethibitishwa” kuwa priori ya kweli. Hii haifanyi maarifa kama hiyo kuwa ya manufaa, bali inamaanisha kwamba dhamani ya ukweli ya tamko kama hili haiwezi kujadiliwa. Ikiwa sio ukweli wa priori, hatua inayofuata ni kuuliza ikiwa taarifa hiyo inajipinga yenyewe au haiwezekani kimantiki. Ikiwa ndivyo, basi inaweza kutupiliwa mbali kama priori ya uwongo.

Ikiwa kauli haiwezi kutathminiwa kwa misingi ya priori, lazima itathminiwe kwa kutumia ushahidi zaidi au uchunguzi: ni maarifa ya posteriori. Madai mengi katika hali nyingi huitaji kiwango fulani cha maelezo ya majaribio ili iweze kuchunguzwa. Ikiwa kauli haijakubaliwa kikamilifu kama priori, basi kauli hiyo ni ya posteriori, na watu wengi hukubali kuwa ni ya posteriori.

Neno priori ndilo neno hutumika mara nyingi sana. Katika mantiki na mijadala, uwezo wa kuweka kitu alama kama maarifa priori ni ubainifu wa maana. Kwa wakati huo huo, sio kawaida kuona wazo kutambuliwa kuwa posteriori. Wakati hili linafanyika, mara nyingi hukusudiwa kukanusha dai kwamba kauli hiyo inaweza kujulikana kama priori.

Neno lisilotumiwa sana, fortiori, linaelezea kitu kinachohusiana na maarifa ya awali lakini sio vile kilivyo kamili. Neno fortiori linamaanisha “kutoka yenye nguvu ziadi,” na linarejelea bishano ambalo linatafuta kuthibitisha jambo “dogo” kwa kusihi uhakika wa hoja “kubwa”. Kwa mfano, ikiwa mtu atasema anaweza kumudu kutumia $100, tunadhani kwamba anaweza kumudu $10. Kama kunywa kiwango kidogo cha kitu kioevu ni hatari, tunachukulia kuwa kukunywa kikombe kizima pia ni hatari. Ikiwa mtu anawezakushikilia pumzi yake kwa dakika tatu, basi tunadhania kuwa anaweza kushikilia pumzi yake kwa dakika moja. Ikiwa inachukuliwa kuwa ni dhambi kumpiga mtu ngumi, pia tunachukulia kuwa kumdunga mtu kisu itakuwa dhambi pia.

Wakati tunahoji hoja fulani kwa msingi wa dhana moja kubwa au pana, tunatumia bishano la fortiori. Katika mazungumzo ya kawaida, mara nyingi tunatumia kifungu kama “hata zaidi hivyo” au “zaidi ya yote.” Hii ni kwa maneno ya jumla yanoyosihi utumiaji wa mantiki, na mifano iliyotolewa yote inaweza kutajwa kwa kutumia aina ya lugha hiyo.

Kuzungumza kimakini, mabishano ya fortiori haijalindwa kiwango sawia na kauli ya kweli ya priori. Katika mfano wa hapo juu, ikiwa mtu anayeangaziwa angepewa hundi la $100 na rafiki, kiasi cha pesa anaweza kutumia ni $100. Kwa maneno mengine, kimantiki kuna uwezekano kwamba ataweza “kukidhi” kutumia $100 bali sio $10, kwa kuwa hana hela zingine. Kwa hivyo mabishano ya priori ni ya busara, kimantiki ya kweli kabisa, kwa hivyo sio priori halisi.

Kama ilivyo kwa mawazo yote ya kifalsafa, Maandiko na uzoefu wa Kikristo huakisi ufahamu wa dhana ya priori, posteriori na fortiori. Kitabu cha Waebrania kinauliza, kama dhabihu ya wanyama ina athari fulani ya kiroho, “sembuse ile ya Kristo” ambayo ina athari kubwa (Waebrania 9:13-14)? Hili ni bishano la kifortiori. Yesu alitumia bishano la kifortiori wakati alisema, “Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?” (Mathayo 7:11)- hoja ya Yesu inategemea kifungu ni jinsi gani zaidi. Paulo anaonyesha kwamba Ukristo umefungamanishwa bila kubatilishwa na wazo la ufufuo-ikiwa hakuna ufufuo, basi imani yetu ni ya uongo (1 Wakorintho 15:12-19). Hii ni kauli priori. Kinyume chake, papo hapo maneno ya Pualo yaliyofuata ni kwamba Kristo kwa kweli alifufuliwa kutoka kwa wafu (1 Wakorintho 15:20), ambayo ni dhana ya kiposteriori. Maandiko yanaweka umuhimu mkubwa katika ushahidi na kuchunguza ukweli (Luka 1:1-4; 2 Petro 1:16; Matendo 17:11).

Uinjilisti wa Kikristo na watetezi pia ulijumuisha mambo haya matatu. Baadhi ya hoja za kuwepo kwa kwa Mungu ni dhana ya kipriori, ambayo inategemea mantiki, kama vile hoja ya ontolojia (inayojishughulisha na asili ya uhai). Tuchukulie kwamba ulimwengu una mwanzo, hoja ya sayansi kuhusu ulimwengu (kosmolojia) inakuwa madai ya kipriori. Mazungumzo mengi yanayohusisha watetezi na uinjilisti kimsingi hutegemea ufahamu wa kiposteriori, haswa wale wanaojadili ni jinsi gani maandiko ni ya kutegemewa au wakiakikisha kutumia hoja inayoelezea kuwepo kwa Mungu. Majadiliano kuhusu jinsi gani haki za kibinadamu na hitaji la maadili ni sambamba na sifa za Mungu za upendo na utakatifu ni aina ya mabishano ya kifortiori. Hivyo ndivyo ilivyo kuhusu ulinganisho unaoonyesha kuwa Biblia ni ya kweli, ya kihistoria, na yenye kutegemeka kisayansi: kutokana na uthibitisho huo “inahoji mabishano” ambayo siyo ya kweli na yanahitilafiana na Biblia kwa kuegemea msingi wa fortiori.

Kujua tofauti kati ya dhana hizi ni muhimu sana kwa mambo ya kifalsafa na katika kutafsiri kwetu Maandiko.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maarifa yasiyohitaji ushahidi (ya kweli yasiyotegemea uzoefu au uchunguzi wa awali)(priori), kutoka kwa kile kilicho cha baadaye(posteriori), hoja yenye nguvu(fortiori)
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries