settings icon
share icon
Swali

Je, kuna maana katika mkasa?

Jibu


Wakati mkasa umetokea, ni kawaida watu kuuliza, “Je, hii inamaanisha nini?” Wakati tunashuhudia maafa au mauaji ya halaiki, kuna hisia ya kawaida kwamba ambacho kimetokea hakikupaswa kutokea. Hii hisia ya asili ya “ukosaji” ni dokezo kwa maana katika matukio haya. Wakati tunatafuta kupata maana katika mkasa, lazima tuwe na mtazamo sahihi. Tunapaswa kutazama swali kwa njia ambayo inaruhusu jibu madhubuti, na hili linawezekana pekee kupitia mtazamo wa kiulimwengu wa kikristo. Kwa sababu Mungu anaweka maana katika kila kipindi na tukio katika historia, kupitia Yeye tunaweza anza kupata maana katika mateso. Asili ya dunia hii inajikopesha yenyewe kwa matukio ya mkasa. Kwa bahati, Mungu anatuzungumzia, ili tuweze kupata sio maana tu, lakini pia ukombozi na nafuu kutoka kwa mateso ya dunia.

Wakati tunasoma azimio ya fizikia, ni muhimu kufahamu mtazamo. Kasi na mchapuko ina maana tu katika mwunganisho kwa baadhi ya vitu; vitu hivi ni hoja ya kumbukumbu. Njia ambayo hoja ya kumbukumbu inasonga huathiri mtazamo wetu. Hiyo ni kweli katika maana yetu ya sahihi na uongo. Kwa dhana ya nzuri, mbaya, sahihi, uongo, au mkasa kuwa na maana, huzingatiwa na hoja ya kumbukumbu ambayo haibadiliki au kusonga. Hoja ya kumbukumbu ya pekee sahihi kwa swala hili ni Mungu. Ukweli kwamba tunazingatia mauaji ya halaiki kuwa mbaya, inaunga mkono kwa nguvu fikra ya Mungu kama pointi ya kumbukumbu kwa maana yetu ya mema na uovu. Bila Mungu, hata matukio ambayo tunazingatia kuwa mkasa mkubwa sana si ya maana kuliko kitu chochote kile. Lazima tufahamu asili ya dunia hii na uhusiano wetu na Mungu ili kupata maana kutoka vitu tunavyoona.

Mungu anapenyeza kila kipindi na kila tukio na maana na kutupa Imani kwamba anaelewa yale tunayopitia. Wakati Yesu alianzisha karamu takatifu, aliunganisha kale, sasa, na baadaye pamoja. 1 Wakorintho 11:26 inasema, “Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo.” Ufahamu wa Mungu wa matukio yote inamaanisha kuwa hakuna kitu kisicho cha maana Kwake. Kama Mungu anajua wakati shoromo inaanguka, hakika anajua wakati tunakumbwa na mkasa (Mathayo 10:29-31). Kwa kweli, Mungu alituhakikishia kwamba tutakumbana na matatizo dunini (Yohana 16:33) na kwamba kibinafsi amepitia magumu yetu (Waebrania 2:14-18; Waebrania 4:15).

Huku tukifahamu kwamba Mungu anatawala vitu vyote, ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu siye chanzo cha mkasa. Wingi wa mateso mengi ya binadamu yanasababishwa na dhambi, mara kwa mara dhambi ya watu wengine. Kwa mfano, mauaji ya halaiki ni makosa ya muuaji kutotii sheria ya maadili ya Mungu (Kutoka 20:13; Warumi 1:18-21). Wakati tunatafuta maana katika tukio kama hilo, lazima tufahamu ni kwa nini dunia hii iko jinsi ilivyo. Magumu ya ulimwengu huu kiasili yalisababishwa na dhambi ya mwanadamu (Warumi 5:12), ambayo kila wakati ni jambo la kuchagua (1 Wakorintho 10:13). Huku Mungu akiwa na uwezo kikamilifu wa kusimamisha mikasa kabla ianze, wakati mwingine anachagua kutofanya hivyo. Wakati labda hatuwezi jua ni kwa nini, tunajua kwamba Yeye ni mkamilifu, mwenye haki, na mtakatifu, na hivyo ndivyo mapenzi Yake yaliko. Pia, mateso tunayopitia katika dunia hii yanafanya mambo matatu. Yanatuongoza kumtafuta Mungu, kukuza uwezo wetu wa kiroho, na yanaongeza shauku yetu ya mbinguni (Warumi 8:18-25; Yakobo 1:2-3; Tito 2:13; 1Petro 1:7).

Katika bustani ya Edeni, Mungu alizungumza na Adamu na kuongea kwa njia ya wazi na ya moja kwa moja, sio katika wazo la dhahanio. Mungu anatuzungumzia kwa njia hiyo hivi leo. Kwa njia nyingine, hii ndiyo maana muhimu zaidi kupatikana katika mkasa wowote. Matukio ya mkasa yanaonyesha maana yao kwa namna tunavyoyaitikia. C.S. Leewis alisema, “Mungu anatunong’onezea katika furaha yetu, huzungumza katika dhamiri zetu, lakini anapiga kelele katika uchungu wetu. Ni kipaza sauti chake cha kuamsha ulimwengu hausikii.” Hii haimaanishi kwamba Mungu husababisha mkasa, lakini anatumia huitikiaji wetu kwa mkasa kuzungumza na sisi. Matukio ya mkasa hayatukumbushi pekee kwamba tunaishi katika dunia isiyokamilika na yenye imeanguka, lakini kwamba kuna Mungu ambaye anatupenda na anataka kitu bora kwetu zaidi ya kile dunia inatoa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kuna maana katika mkasa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries