settings icon
share icon
Swali

Maadili ya ngono ni gani?

Jibu


Maadili ya kujamiiana ni mchanganyiko wa mambo ya kimaadili na wema na mabaya yanayohusiana na kujamiiana kwa binadamu. Maadili ya ngono ni pamoja na mitazamo na maadili yanayohusiana na utambuzi wa kijinsia, mwelekeo wa ngono, uzazi na ridhaa. Maadili ya kijinsia ya tamaduni kwa kawaida huhusishwa kwa karibu na dini ya utamaduni huo, ambayo hutoa thamani ya maadili kwa vipengele fulani vya kujieleza kingono. Kwa mfano, uamuzi wa ikiwa ubakaji, unyanyasaji, au uzinzi ni mbaya kimaadili hutofautiana kutoka kwa utamaduni hadi utamaduni na mra nyingi huhusishwa na kiwango cha ushawishi ambao Ukristo umekuwa nao katika eneo hilo. Katika mtazamo wa ulimwengu wa Kiyahudi-Kikristo, Biblia ina usemi wa mwisho juu ya maadili ya ngono na imekuwa kipimo kwa mataifa mengi huru kwa milenia mbili zilizopita.

Kabla ya Mwanzo sura ya sita, mwanadamu tayari alikuwa amekiuka kila kiwango cha maadili ambacho Muumba alikuwa amekiweka ndani ya moyo wao (Mwanzo 6:1, 5-6). Andiko la Mwanzo 6:5 linasema kwamba “kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya.” Tunaweza kufasiri hilo sahihi tukijumuisha mazoea ya ngono pia. Mitazamo ya kibinadamu kuelekea ngono imechafuliwa na dhambi, ubinafsi, na upotovu tangu mwanzo wa historia ya mwanadamu.

Tangu mwanzo, Mungu amekuwa na haki ya kufafanua maadili ya ngono kwa ajili yetu kwa sababu Aliumba kujamiiana. Alipomuumba Hawa kwa ajili ya Adamu na kumleta kwake (Mwanzo 2:21-25), alifafanua ndoa na kuibariki. Katika Maandiko yote kuna amri zinazoimarisha ufafanuzi huo (Kumbukumbu 5:18; Walawi 20:10; Marko 10:6-8; Waefeso 5:31). Ngono iliundwa kwa mume na mke ndani ya agano la ndoa. Waebrania 13:4 inasema, “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, nayo malazi yawe safi, kwa kuwa Mungu atawahukumu wazinzi na waasherati wote.” Kwa hiyo, usemi wowote wa ngono nje ya agano la ndoa ni dhambi, iwe ni uzinzi, ngono ya kabla au nje ya ndoa, ulawiti, ukahaba, au hata tamaa (Mathayo 5:28).

Maadili ya Mungu ya ngono ni kwa manufaa yetu, na sio madhara. Yeye hatupi sheria zake ili kuzuia furaha yetu au kupunguza uhusiano wetu. Mungu aliyetuumba anajua jinsi tunavyofanya kazi vizuri zaidi. Kama vile mvumbuzi wa teknolojia mpya anavyotoa maagizo ili kifaa kiweze kufanya kazi kwa viwango bora, ndivyo Mungu anavyotoa maagizo kwa uumbaji Wake, binadamu katika Neno Lake, Biblia (Zaburi 119:105). Anajua matokeo ya kutunza vibaya zawadi yake ya kujamiiana. Dunia yetu inayumba kutokana na uzito wa matokeo hayo. Mamilioni ya uavyaji mimba, magonjwa ya sinaa, talaka, kulawiti watoto, ubakaji, na visa vya ulanguzi wa binadau vingekomeshwa ikiwa tu tungeshililia maadili ya Mungu ya kingono.

Haijalilishi maamuzi yetu ya awali ya kimaadili, kila mmoja wetu ana chaguo mpya kila siku. Tunaweza kuendelea kugaagaa katika upotovu wa ulimwengu ambapo maadili ya ngono hubadilika kila saa kulingana na hisia za mtu kwa sasa. Au tunaweza kujitolea kupatanisha maoni yetu na ya Mungu na kuchukulia ngono kuwa zawadi takatifu kama ilivyo. Kama vile hatuwezi kutumia chombo kuukuu kuwekelea mafuta machafu kutoka kwa gari letu, vivyo hivyo hatupaswi kamwe kutumia miili yetu kwa njia zinazoidhalilisha na kuivunjia heshima kingono. Tuliumbwa kuwa hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 6:19-20). Hekalu la Mungu ni takatifu, na ni wajibu wetu kulitunza, kuliheshimu, na kulifanya patakatifu pake (Warumi 12:1). Tunapofanya hivyo, tunaweza kuepuka matokeo mabaya ambayo wengi wanapotea kwa sababu wanapuuza maadili ya Mungu ya ngono.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Maadili ya ngono ni gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries