settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Biblia inafaa kuwa chanzo chetu cha maadili?

Jibu


Ikiwa Biblia sio chanzo cha maadili kwa Mkristo, basi swali linafaa kuulizwa, “chanzo kinafaa kuwa kipi?” Mtazamo wa Mkristo unaegemea usemi wa misingi mbili: 1) Mungu yupo, na 2) Mungu amezungumza kwetu kupitia Biblia. Ikiwa dhamira hizi mbili sio mahali pa kuanzia kwa mtazamo wa Mkristo, basi hatuko tofauti na wengine wote ambao hujaribu kutafuta kutopendelea mahali ambapo sio halisi.

Kulingana na Biblia, mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Sehemu ya mfano huo humfanya mwanadamu kuwa kiumbe mwenye maadili. Sisi ni mawakala ambao hufanya uamuzi wa maadili na tuna uwezo wa kutofautisha kati ya mema na mabaya. Ufahamu wetu wa sheria ya Mungu ndio ndio msingi mkuu ambao tunatofuatisha wema na mabaya, na ufahamu huo unatoka katika vyanzo viwili-ufunuo na dhamiri. Ufunuo unajieleza. Mungu alitoa amri kwa Adamu na Hawa katika bustani. Aliwapa Waisraeli Amri Kumi, pamoja na sheria na taratibu nyingi kwa Waisraeli baada ya kutoka Sinai. Yesu alifupisha sheria za Agano la Kale kwa amri mbili muhimu-mpende Mungu na umpende jirani yako. Haya yote yanawakilisha ufunuo wa Mungu wa sheria yake ambayo ni akisi tu ya tabia yake ya kimaadili kwa watu wake.

Biblia pia inasema kwamba Mungu aliandika sheria Zake mioyoni mwetu (Warumi 2:15). Hii ni dhamira. Kwa meneno mengine, hata bila ufunuo wake Mungu katika amri, kihisia tunajua sheria ya Mungu kwa msingi kwamba tuliumbwa kwa mfano Wake. Ingawa kwa sababu ya anguko (Mwanzo 3), mfano huo uliharibiwa na kuharibika, hii ikiwa ni pamoja na dhamira. Kwa hivyo hata ingawa tunaijua sheria ya Mungu kupitia dhamira zetu, huwa tunajaribu kuibadili ili iweze kutunufaisha. Hiyo ndiyo maana tunahitaji ufunuo.

Biblia ambayo ina ufunuo wa mapenzi ya maadili ya Mungu katika sheria na amri Yake, ni ufunuo wake kwa watu wake. Kwa hivyo, Biblia inakua chanzo chetu cha maadili kwa sababu Biblia ni Neno lenyewe la Mungu lililoandikwa (2 Timotheo 3:16; 2 Petro 1:21). Ikiwa Mkristo anataka kujua mapenzi ya Mungu, anaigeukia Biblia ili apate amri ya Mungu kwake. Ikiwa Mkristo anataka kutambua mema na mabaya, anafungua maelezo ya Biblia juu ya uadilifu wa Mungu.

Je! ni nini hutokea ikiwa Mkristo hawezi kuiangalia Biblia kama chanzo chake cha maadili? Kunazo njia nyingi sana za kujibu swali hili, lakini la msingi ni, sisi wote huwa tunaamini dhamira yetu, iwe ni kwa njia iliyo wazi au isiyo ya wazi. Dhamira ya mwanadamu inaweza kulinganishwa na mfumo wa kengele; inatuonya wakati tunakiuka viwango vya maadili. Dhamira yetu ni nzuri tu ikiwa kiwango cha maadili inayokishikilia ni kizuri. Ikiwa si Biblia, basi bila shaka tunafahamisha dhamira yetu kwa njia zinginezo.

“Mshindani” mkuu anayetawala kwa sasa kwa maadili ya kibiblia katika jamii yetu ni makubaliano ya kijamii. Kwa maneno mengine, maadili yetu yanaundwa na kubadilishwa na utamaduni unaotuzunguka. Inapaswa iwe rahisi kuona kwamba ikiwa makubaliano ya kijamii ndio dira ya maadili yetu, basi tumejenga maadili yetu katika msingi hafifu. Makubaliano ya kijamii ni-makubaliano tu. Ni taswira ya matukio ya kiadili hii leo. Kizazi kimoja au viwili vilivyopita, usenge, talaka, au uzinzi havingeruhusiwa, vilihesabiwa kuwa dhambi. Siku hizi, ushoga na talaka ni matukio ya kawaida na uzinzi haunyapawi jinsi ulivyo kuwa hapo mbeleni. Kimsingi, kile tulicho nacho katika makubaliano ya kijamii ndicho kilifanyika kwa Waisraeli kwa vizazi vichache vilivyopita baada ya kuingia katika nchi ya Ahadi: “kila mmoja akafanya kama alivyoona vyema machoni pake mwenyewe” (Judges 17:6). Watu walimwacha Mungu, na katika vizazi viwili walikuwa wakifanya maovu machoni pa Mungu.

Basi ni kwa nini Biblia inapaswa kuwa chanzo chetu cha maadili? Kwa sababu bila Biblia, sisi ni kama meli zinazoelea baharini. Mwishoni mwa Mahubiri Mlimani, Bwana wetu alisema maneno haya: “Kwa hiyo kila mtu ayasikiaye haya maneno yangu na kuyatenda, ni kama mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba. Lakini haikuanguka; kwa sababu msingi wake ulikuwa kwenye mwamba” (Mathayo 7:24-25). Neno la Mungu, Biblia, ndio mwamba pekee ambamo tunaweza jenga maadili mema.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Biblia inafaa kuwa chanzo chetu cha maadili?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries