settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini umuhimu wa lango la Mashariki la Yerusalemu?

Jibu


Mji wa kale wa Yerusalemu umezungukwa na ukuta wenye milango minane mikubwa. Milango inayosonga kinyume na saa kutoka lango la kazikazini ni, Lango la Herode, Lango la Damasko, Lango Jipya, Lango la Yafa, Lango la Sayuni, Lango la Samadi, Lango la Mashariki, na Lango la Simba. Lango la Mashariki linaloangalia Mlima wa Mizeituni ngamboni mwa bonde la Kidroni, ni la kipekee kwamba limesitiriwa kabisa. Wadadisi wengine wanaona uzuiliaji wa Lango la Mashariki kuwa utimilifu wa unabii wa kibiblia.

Lango la Mashariki la Yerusalemu pia linaitwa Lango la Dhahabu au Lango Zuri (Matendo 3:2). Katika Kiebrania linaitwa Sha’ar Harahamim, “Lango la Rehema.” Kwa sasa ndilo lango kongwe katika mji wa kale wa Yerusalemu, likiwa lilijengwa mnamo kati ya karne ya 6 au 7 AD. Pia, ni lango ambalo linatoa nafasi ya kuingia katika mlima wa hekalu- iwapo mtu angepita katika vitundu vya Lango la Mashariki, angekuwa karibu sana na pale hekalu la Wayahudi lilikuwa limesimama. Wakati Yesu aliingia Yerusalemu akitokea upande wa Mlima wa Mizeituni katika Matayo 21, alitumia lango ambalo pia kwa sasa hivi ndilo lango la Mashariki au Lango la Dhahabu.

Lango la Mashariki lilifungwa mnamo mwaka wa AD 1540-41 kwa amri ya Suleiman Mkuu, Mtawala wa himaya ya Dola ya Waturuki. Inaaminika kwamba sababu ya Lango la Mashariki kufungwa ilikuwa ni kumzuia Masihi wa Kiyahudi asipate nafasi ya kuingia Yerusalemu. Tamaduni la Kiyahudu lakauli kwamba Masihi atapitia katika Lango la Mashariki wakati atakapokuja kutawala. Suleiman Mwislamu alijaribu kubadili mipango ya Masihi kwa kujenga mnara wa saruji futi kumi na sita. Lango la Mashariki limebaki kufungwa takribani miaka 500.

Huku kuzibwa kwa Lango la Mashariki ndio kumesababisha wengi wa wanafunzi wa unabii kuketi na kumakini. Kitabu cha Ezekieli lina nakuu nyingi zinazorejelea lango ambalo linaangalia mashariki. Katika Ezekieli 10:18-19, nabii anaona utukufu wa Bwana ukiondoka hekaluni kupitia “ingilio la lango la mashariki la nyumba ya Bwana”; utukufu ukapaa juu na kuelekea upande wa mashariki wa Mlima wa Mizeituni (Ezekieli 11:23). Baadaye, Ezekieli anaona utukufu wa Bwana ukirejea hekaluni kupitia “ingilio lanaloelekea mashariki” (Ezekieli 43:1-5).

Kisha, katika Ezekieli 44:1-2 tunasoma kuhusu mlango ukiwa umefungwa: “Ndipo yule mtu akanirudisha mpaka kwenye lango la nje la mahali Patakatifu, lile linaloelekea upande wa mashariki, nalo lilikuwa limefungwa. 2 Bwana akaniambia, “Lango hili litabaki limefungwa. Haliruhusiwi kufunguliwa, wala hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingilia kwenye lango hili. Litabaki limefungwa kwa sababu Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa kupitia lango hili.” Mwisho katika Ezekieli 46:12 tunasoma kwamba kuna mtu mmoja, “mwana mfalme,” ambaye anaweza kuingililia mlango wa mashariki: “

Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa Bwana… lango linaloelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake... Kisha atatoka nje, naye akisha kutoka nje, lango litafungwa.”

Wengine wanatafsiri vifungu katika Ezekieli kuwa vinarejelea Bwana Yesu Kristo. Utukufu wa Bwana unaokuja hekaluni unaashiria ule kuingia kwa ushindi Yerusalemu (Ezekieli 43:2; Matayo 21:1-11). Amri ya kuufunga mlango milele kwa sababu Bwana alikuwa ameingia (Ezekieli 44:2) inaonekana kuwa utabiri wa Waislamu kufunga Lango la Mashariki mnamo mwaka wa AD 1540. Na hatimaye, “mwana mfalme” ambaye atafunguliwa lango (Ezekieli 46:12) anaonekana kuwa Kristo mwenyewe na ujio wake mara ya pili-Mfalme wa Amani atarudi katika Mlima wa Mizeituni (Zekaria 14:4) na kuingia Yerusalemu kwa njia ya Lango la Mashariki lililofunguliwa.

Tafsiri hii inajulikana sana na inasababisha uvumi mwingi juu ya ni jinsi na ni lini Lango la Mashariki litafunguliwa. Ijapokuwa, kunalo tatizo la kimuktadha kwa tafsiri kama hii.

Kwanza, kuna ugumu katika kuunganisha ”lango linaloelekea Mashariki” katika Ezekieli na Lango la Mashariki la mji wa kale wa Yerusalemu. Ezekieli haswa anasema kwamba lango aliloliona ni “lango la nje la patakatifu” (Ezekieli 44:1); yaani ni lango la ua la hekalu, na sio lango la mji.

Pili, Lango la Mashariki mwa Yerusalemu sio sawia na lile ambalo Yesu aliingilia katika kule kuingia kwake kwa ushindi Yerusalemu. Lango la Mashariki la sasa, halikujengwa hadi pale baada ya karne nyingi baada ya Kristo. Lango la asili ambalo Nehemia alilijenga (na pengine lilijengwa wakati wa Suleimani) liko chini ya lango lililoko sasa, kama vile imenakiliwa na mdadisi wa vivusi Yakobo Fleming katika mwaka wa 1969. Ilikua ni katika lango la chini (ambalo kwa sasa liko chini la lile la sasa) ambalo Yesu aliingilia Yerusalemu katika mwaka wa AD 30.

Tatu, hekelu ambalo Ezekieli analiona katika mlango wa 40-47 sio hekalu sawia ambalo Yesu aliingia, na Yerusalemu anayoielezea vile vile ni tofauti na mji wa kale wa Yerusalemu ambao tunaujua hii leo. Hekalu la miaka elfu moja (hekalu la tatu) katika Ezekia likipimwa kwa kadri ni kubwa kuliko hekalu mbili za kwanza, na Yerusalemu ya milenia itakua na malango kumi na mbili wala sio nane (Ezekieli 48:30-35).

La mwisho na la muhimu, “mwana wa ufalme” katika Ezekieli 46 sio Masihi. Badala yake ni yeye ni mwangalizi wa Yerusalemu wakati wa ufalme milenia. Yeye sio Yesu, lakini anahudumu chini ya mamlaka ya Yesu. Tunajua kwamba huyu mwana wa ufalme sio Bwana kwa sababu lazima atoe dhabihu kwa ajili yake mwenyewe na vile vile kwa ajili ya watu: “Katika siku hiyo mkuu anayetawala atatoa fahali kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote wa nchi” (Ezekieli 45:22).yeyote yule mwana wa ufalme atakua, yeyé ni mwanadamu aliye na hali ya dhambi ambayo ni lazima ipate upatanishwo.

Kwa muhtasari, “lango linaloelekea mashariki” ambalo Ezekieli analielezea ni tofatuti na lile Lango la Mashariki linaloonekana hii leo katika mji wa Yerusalemu ya kale. Lango la sasa (lililofungwa) halikuwepo wakati wa Kristo, kwa hivyo Bwana hakuwahi kuingia humo. Eneo la Lango la Mashariki la awali (lile ambalo Yesu aliingia) liko chini ya kiwacngo cha ardhi cha kisasa na sio sawia na maelezo ya hekalu la baadaye vile ilivyoelezwa katika Ezekieli 40-42.

Basi tunakisia kwamba lango la mashariki katika Ezekieli 44 litakuwa sehemu ya hekalu la milenia siku za usoni. Bado halijajengwa.

Je! tunawezaje kutafsiri kukuja na kuondoka kwa utukufu wa Mungu na kufungwa kwa lango la mashariki katika unabii wa Ezekieli? Kama hivi: nabii anaona utukufu wa Bwana ukiondoka hekaluni katika sura ya 10 kwa sababu ya uovu mwingi wa watu- hili ndilo hekalu la kwanza ambalo liliharibiwa na Wababeli mwaka wa 586 Kabla Kristo azaliwe. Baadaye katika sura ya 43, Ezekieli anauona utukufu ukirejea hekaluni-hili ni hekalu jipya lililopanuliwa la ufalme wa milenia. Katika sura ya 44, Ezekieli anaambiwa kwamba lango la mashariki la hekalu “Litabaki limefungwa kwa sababu Bwana, Mungu wa Israeli, ameingia kwa kupitia lango hili” (aya ya 2). Kwa maneno mengine, katika wakati wa milenia, utukufu wa Bwana hautaondoka katika hekalu. Njia ile uliondokea hapo awali (kwelekea mashariki) imefungwa, hii ikiashiria uwepo wa kudumu wa Bwana kati ya watu wake. Lango la mashariki litafunguliwa tu siku ya sabato na Mwezi Mpya ili kuruhusu huduma ya ukuhani ya mwana wa ufalme (Ezekieli 46:1-2)

English

Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini umuhimu wa lango la Mashariki la Yerusalemu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries