settings icon
share icon
Swali

Kwani nini nibatizwe?

Jibu


“Kwa nini nibatizwe?” ni swali muhimu ambalo Wakristo wanafaa kujibu. Tangia siku za mwanzo za kanisa la Kikiristo, ubatizo umekuwa hatua muhimu ya imani ambayo imefuatwa na waamuni wote baada tu ya wokovu (Matendo ya Mitume 2:38, 41; :12, 38 ).

Kitendo cha ubatizo kwa kuzamishwa ndani ya maji kinaonyesha wazi kwa nje uzoefu wa ndani wa mabadiliko yanayotokea katika maisha ya kila muumini wakati wa wokovu. Inaonyesha kuwa mienendo ya zamani ya maisha ya mtu imeisha, na maisha mapya ya imani katika Yesu Kristo yameanza (2 Wakorintho 5:17). Ubatizo ni muhimu kwa sababu unatoa ushuhuda wa wazi- tangazo la hadharani kwa ulimwengu linaloidhinisha na kutambulisha muumini mpya na kifo chake, kuzikwa kwake, na ufufuo wa Yesu Kristo.

Biblia inatoa sababu kadhaa kwa nini ubatizo ni hatua muhimu katika maisha ya Mkristo:

Ubatizo ni ishara ya imani ambayo inaokoa. Kama muhuri wa kudhibitisha, ubatizo unawakilisha uzoefu wetu wa wokovu na kazi nzuri ya Yesu Kristo kwa kufa kwa ajili ya dhambi zetu na kufufuka kwa ajili ya haki yetu: “mkiwa mmezikwa pamoja naye katika ubatizo, na kufufuliwa pamoja naye kwa njia ya imani yenu katika uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu” (Wakolosai 2:12).

Ubatizo ni agizo la Mungu na amri ya Yesu. Kama sehemu ya amri yake kubwa kwa kanisa, Yesu alipeana maagizo haya: “Kwa sababu hii, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati” (Mathayo 28:19-20). Ubatizo ni sehemu muhimu ya kuwa mwanafunzi wa Kikristo na unakusudiwa kuwa hatua endelevu ya kanisa.

Ubatizo ni tendo la utii kwa Mwokozi wetu, likiashiria hamu yetu ya kumfurahisha Mungu. Neno Ukristo linamaanisha “mfuasi wa Kristo.” Kwa kuwa Kristo alituita kubatizwa na kuweka mfano kwa kubatizwa kwake Mwenyewe (Mathayo 3:16), kukataa kubatizwa ni kukiuka amri ya Kristo.

Ubatizo unatuunganisha na Kristo kwa kututambulisha na kifo chake, kuzikwa kwake, na ufufuo wake: “Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima” (Warumi 6:3-4). Tunapodhubu dhambi zetu na kumwamini Yesu Kristo, ubatizo unatoa ushuhuda wa umoja wetu naye.

Vivyo hivyo, ubatizo unawakilisha kifo chetu kwa maisha ya zamani ya dhambi na kuzaliwa kwetu upya katika maisha ya ufufuo na uhuru kutoka utumwa wa dhambi: “ Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi” ( Warumi 6:5-7).

Ubatizo pia unatutambulisha na mwili wa Kristo (1 Wakorintho 12:12-13). Ni ishara inayosema kwamba sasa tunamilikiwa na Yesu Kristo na watu wake: “Kwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmevaa Kristo” (Wagalatia 3:26-27).

Ubatizo unatoa ushuhuda wa hadharani wa kazi ya ndani ya Roho Mtakatifu ya kuosha dhambi zetu: “Mfano wa mambo hayo ni ubatizo , unaowaokoa ninyi pia siku hizi; ( siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), Kwa kufufuka Kwake Yesu Kristo” (1 Petro 3:21; angalia pia Matendo ya Mitume 22:16; 1 Wakorintho 6:11).

Kuelewa kwa usahihi maana ya ubatizo kunamaanisha kufahamu kwamba ni zaidi ya utaratibu wa kidini au mapokeo ya kanisa. Maana ya ubatizo inaanzia katika kifo cha Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ambaye alikufa kwa sababu yetu ili kulipa dhambi zetu, na ambaye alishinda mauti kwa ufufuo wake,na kutupatia maisha mapya kwa Roho na uzima wa milele pamoja na Mungu milele.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwani nini nibatizwe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries