settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu kuzini na mnyama?

Jibu


Biblia inataja kuzini na mnyama katika vifungu vinne tofauti. Kutoka 22:19, “Mtu yeyote aziniye na mnyama lazima auawe.” Walawi 18:23 inasema, “Usikutane kimwili na mnyama na kujitia unajisi kwake. Mwanamke asijipeleke kwa mnyama ili kukutana naye kimwili; huo ni upotovu.” Walawi 20:15-16 inaamrisha, “Kama mwanaume akikutana kimwili na mnyama, ni lazima auawe, na pia ni lazima mnyama huyo auawe. Kama mwanamke atamsogelea mnyama kukutana naye kimwili, muueni mwanamke huyo pamoja na mnyama pia. Lazima wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.” Kumbukumbu inakubaliana, “Alaaniwe mtu akutanaye kimwili na mnyama yeyote.” Kutokana na mistari hii, ni wazi kabisa kwamba, kulingana na Biblia, kuzini na mnyama ni dhambi ya kutisha, isiyo ya asili na ya kuchukiza.

Ni kwa nini kuzini na myanyama kunalaaniwa vikali hivyo? Kwanza, ni upotovu usio wa asili. Ni wazi kwamba wanadamu walikusudiwa kujamiana na wanadamu wengine, sio wanyama. Katika simulizi ya uumbaji, hakuna mnyama ambaye alimfaa Adamu (Mwanzo 2:20). Pili, kuzini na wanyama kunawakilisha kilele cha upotovu ngono. Ukweli kwamba mnyama huyo alipaswa kuuawa (Walawi 20:15-16), licha ya ukweli kwamba hakuwa na “hatia” inaonyesha jinsi usherati ulivyo mwovu. Tatu, pengine, la muhimu ziadi ni kwamba, kuzini na wanyama kunapinga upekee wa ubinadamu ambao Mungu aliumba kwa mfano wake (Mwanzi 1:27). Kuzini na wanyama hushusha ubinadamu chini ya mnyama, mnyama ambaye hawezi kutofautisha mema na mabaya, ya asili na yasiyo ya asili, upendo na tamaa

Hakuna mahali popote katika Agano Jipya linataja kuhusu kuzini na mnyama, lakini hiyo haipaswi kutafsiriwa kuwa inaruhusu ukatili huo au kushusha viwango vya Mungu vya maadili. Kwa ufafanuzi, kuzini na mnyama kumejumuishwa katika makatazo mengi ya Maandiko dhidi ya uasherati (1 Wakorintho 6:9; Wagalatia 5:19; Wakolosai 3:5; Waebrania 13:4).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu kuzini na mnyama?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries