settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu kuwepo kwa nafsi kabla ya mtu kuzaliwa?

Jibu


Biblia haisemi chochote kuhusu kuwepo kwa nafsi kabla ya mtu kuzaliwa kwa sababu hii ni dhana iliyobuniwa na mwanadamu isiyo na msingi wa kweli. Biblia imeweka wazi kuwa kila mtu ni kiumbwe cha kipekee cha Mungu (Mwanzo 2:7; Zekaria 12:1; Yeremia 1:5). Kila nafsi ya kipekee huanza wakati wa kutungwa mimba (Zaburi 139:13–16; Isaya 44:24) na itaendelea milele kwa sababu tumeumbwa kuwa viumbe wa milele (Mwanzo 9:6, Isaya 40:28; Mathayo 25:46).

Dhana ya kuwepo kwa nafsi kabla ya mtu kuzaliwa haiwezi kufuatwa hadi hitimisho lake la kimantiki. Kuwepo kabla ya mtu kuzaliwa kunamaanisha mojawapo ya mambo matatu: (1) nafsi imekuwepo siku zote, (2) nafsi iliumbwa hapo kabla ya mtu kuzaliwa na kusubiri, bila mwili, hadi wakati itakapokaa katika mwili duniani, au (3) nafsi ilikaa kakita mwili mwingine hapo zamani na kuhamishwa kwa mwili wake wa sasa. Ikiwa (1) ni kweli na daima nafsi zimekuwepo, basi wanadamu pia ni sehemu ya Mungu, na hawajaumbwa na wamejiyakinisha. Dhana hii ni kinyume kabisa na madai ya Biblia kwamba hakuna Mungu mwingine ila Yahweh (Mwanzo 5:1; 1 Timotheo 2:5; 1 Yohana 4:12; Malaki 2:10; 1 Wakorintho 8:5-6). Ikiwa (2) ni kweli na nasfi ilisubiri katika kitalu cha mbinguni kabla kuzaliwa duniani, basi Mwanzo 2:7 sio sahihi: “Bwana Mungu alimuumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake, naye mtu akawa kiumbe hai.” Maneno “mtu akawa” yanaonyesha mwanzo halisi ambapo nafsi na mwili wa Adamu vilikuja kuwa hai wakati ule ule. Ikiwa (3) ni kweli, na nafsi ilikaa katika mwili mwingine hapo zamani, basi nafsi iliumbwa wakati gani na kwa kusudi gani? Biblia iko wazi kwamba kila mtu atajibu kwa ajili ya maisha yake (Ufunuo 20:13; Warumi 2:6; Yeremia 32:19). Wakati mwili wa hapo awali ulipokufa, nafsi ilienda wapi? Waebrania 9:27 inasema, “Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu.” Hii inafanyika kwa kila mtu.

Biblia inarejelea kifo kuwa wakati ambapo mtu “alikusanyika pamoja na watu wake” (Kumbukumbu 32:50; Hesabu 20:24). Hii inaonyesha kwamba mtu anapokufa, nafsi yake huondoka mwilini na kuungana na waliomtangulia. Katika mfano wa Yesu wa tajiri na Lazaro (Luka 16:19–31), nafsi ya Lazaro iliondoka kwenda “kifuani mwa Abrahamu” (mstari wa 22). Nafsi ya tajiri ilikuwa inateseka (mstari 23). Hakuna nafsi yoyote kati ya hizi iliyokaa tena kwa mwili mwingine, wala hakuna ishara kwamba nafsi zao zilikuwepo kabla ya mtu kuzaliwa. Kila mmoja wao alipokea matokeo ya uchaguzi wao maishani (mstari 25). Wakati wa ufufuo tutaunganishwa na miili yetu ya asili katika umbo la utukufu (1 Wakorintho 15:42; Wafilipi 3:21). Ikiwa kuna uwezekano wa nafsi kuwepo katika mwili mwingine, nafsi ingekaa kwa mwili mgani?

John was conceived six months before Jesus (Luke 1:26, 36), yet he indicated that Jesus existed before he did. If John had pre-existed, he could not have made that claim. Jesus, as God, existed as one with the Father since the beginning. He told the Jewish authorities, “Before Abraham was born, I am!” (John 8:57–58). His human birth was a unique event never replicated on any level. God did know our names before we were created, because He is omniscient and dwells outside of time (Ephesians 1:4; Revelation 13:8). But we are each individuals; we are unique souls placed in unique bodies, and we will all stand before God to give an account of the unique earthly lives we were given (Romans 14:10; Revelation 22:12).

Yesu ndiye mtoto pekee aliyezaliwa katika ulimwengu huu ambaye alikuwepo kabla ya kuzaliwa kwake (Yohana 1:1; 17:5; Wakolosai 1:17). Wakati Yohana Mbatizaji aliona Yesu, alisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuniliko mimi, kwa kuwa alikuwepo kabla yangu’” (Yohana 1:30). Yohana alitungika miezi sita kabla ya Yesu kutungika (Luka:26, 36), hata hivyo aloinyesha kwamba Yesu alikuwepo kabla yake. Ikiwa Yohana angeluwapo hapo awali, hangeweza kutoa madai hayo. Yesu, kama Mungu alikuwepo kama mmoja na Baba tangu mwanzo. Aliwaambia viongozi wa Kiyahudi, “Kabla Ibrahiu hajazaliwa, mimi nipo!” (Yohana 8:57-58). Kuzaliwa kwake kwa kama binadamu ilikuwa tukio la kipekee ambalo halijawahi kuigwa kwa kiwango chochote. Mungu alijua majina yetu kabla hatujaumbwa, kwa sababu yeye anajua yote na anaishi nje ya wakati (Waefeso 1:4; Ufunuo 13:8).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu kuwepo kwa nafsi kabla ya mtu kuzaliwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries