settings icon
share icon
Swali

Biblia inasema nini kuhusu kuvutiwa kimapenzi na jinsia zote bila kujali kama ni wa kike au ni wa kiume? Je! biblia inasema nini kuhusu kuvutiwa na jinsia zote ukiwa unatabua jinsia yao?

Jibu


Kuna uhusiano wa karibu kati ya mvuto wa jinsia zote bila kutambua jinsia yao na mvuto wa jinsia zote ukiwa unatambua jinsia yao. Kwa kweli, hakuna tofaufi kati ya hizi mbili. Katika hali zote mbili wapenzi wa jinsia zote wanavutiwa kingono na wanaume na wanawake wa jinsia tofauti, mashoga wanaume na wanawake, wanaume na wanawake wenye jinsia mbili, wanaume na wanawake waliobadili jinsia, wanaume na wanawake walio na jinsia tofauti, n.k. Tofauti ni kwamba kuna wale wanaovutiwa na jinsia zote wakidai hawatambui jinsia zao na kwa upande mwingine kuna wale wanaovutiwa na jinsia zote lakini hawajali. Kauli mbiu isiyo rasmi ya wote wawili inaonekana kuwa ya “mioyo na si sehemu za mwili”

Biblia haitaji kabisa hali hizo mbili. Lakini kwa kuwa hali hizi zote wakati mwingine huhusisha ngono na jinsia moja, shutuma za kibiblia za ushoga zinaweza kutumika kwa usawa kwa wale wanaofanya mapenzi ya jinsia zote au ujinsia (Walawi 18:22; 20:13; Warumi 1:26-27; 1Wakorintho 6:9). Aina pekee ya shughuli za ngono ambazo Biblia inaunga mkono ni ngono kati ya watu wa jinsia tofauti ndani ya mipaka ya ndoa (Matendo 15:20; 1 Wakorintho 6:13; Wagalatia 5:19; Waefeso 5:3; Wakolosai 3:5).

Mwenendo wa hivi punde wa kupuuza jinsia au hata kukataa kabisa sio kibiblia. Mungu aliumba mwanamume na mwanamke na kuwaumba ili wakamilishane, sio tu kimwili na kingono bali pia kihisia na kiroho (Mwanzo 2). Kukataa tofauti kati ya wanaume na wanawake na kukumbatia njia mbadala za ujinsia, kama vile kuvutiwa na watu wa jinsia zote, ni kukana uhalisia, na muhimu zaidi, kukataa Mungu kama Muumba na Mbunifu. Kuiweka kwa urahisi, kuvutiwa na watu wa jinsia zote ni dhambi.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Biblia inasema nini kuhusu kuvutiwa kimapenzi na jinsia zote bila kujali kama ni wa kike au ni wa kiume? Je! biblia inasema nini kuhusu kuvutiwa na jinsia zote ukiwa unatabua jinsia yao?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries