settings icon
share icon
Swali

Je! Kutuma ujumbe wa maneno ya mahaba ni dhambi?

Jibu


“Ujumbe wa kingono” ni kutuma ujumbe chafu. Ni kitendo cha kutuma ujumbe au picha za ngono hadharani, kwa kawaida kutoka simu moja hadi nyingine. Watu wengine huona kutuma ujumbe wa ngono kuwa sio jambo la kudhuru. Baada ya yote kuna maneno machache tu na labda na picha chache zinazohusika. Sio kana kwamba watu wanafanya uzinzi au uasherati.

Mathayo 5:28 inasema, “Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.” Dhana hii kimaadili pia inatumika kwa jinsi wanawake wanavyowatazama wanaume, na Yesu kwa uwazi analinganisha tamaa na uzinzi. Kwa hiyo ukweli kwamba “maneno au picha pekee ndizo zinazohusika” ni wazi kuwa si jambo la maana kwa Mungu. Kilicho muhimu ni kile kilicho ndani ya mioyo yetu. Andiko la Wakolosai 3:5 linatuonya “tuue” chochote ambacho ni cha asili yetu ya kidunia, hii ikiwa ni pamoja uasherati, uchafu, tamaa, na nia mbaya.

Wagalatia 5:19-21 inaonyesha madhara makubwa ya kutotii katika hili jambo: “Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: Uasherati, uchafu, … na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha kuwaonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama hayo, hawataurithi Ufalme wa Mungu.”

Je! itakuaje katika kutuma ujumbe wa ngono kati ya wanandoa? Kutumiana ujumbe kati ya mume na mke haitakuwa dhambi, kwa kuwa ngono yenye kuridhisha ni zawadi ambayo Mungu huwapa wenzi wa ndoa. Walakini, ushauri kama huo ni potovu. Hatujui ni nani anayeweza kusoma jumbe zetu au kutazama picha tunazaotuma. Inawezekana kwamba mtu anaweza kuona picha za uchi za mwenzi wako akichungulia simu zetu mabegani, na hii inaeza msababishia mtu huyo tamaa. Hii inaonekana kutowezekana? Yakobo 1:14-15 inasema, “Lakini kila mtu hujaribiwa wakati anapovutwa na kudanganywa na tamaa zake mwenyewe zilizo mbaya. Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba, huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa, huzaa mauti.”

Kwa kuzingatia ufunuo wa hivi majuzi kuhusu upekusi wa serikali wa simu za rununu na mitandao, vile vile na uwezo wa wadukuzi kuingilia mawasiliano ya kibinafsi, tunapaswa kuwa waangalifu katika matumizi yetu ya simu na vifaa vinavyoweza tumia tuvuti. Hata kama hatutumi ujume mfupi, bado tunakabiliwa na matatizo ya utambulisho wetu na data ya kibinafsi kuibwa.

Ni vyema kufuata ushauri wa 1 Wakorintho 10:31, “Basi, lolote mfanyalo, kama ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kutuma ujumbe wa maneno ya mahaba ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries