settings icon
share icon
Swali

Je! Kutotubu ni nini? Je, inamaanisha nini kuwa mtu asiyetubu?

Jibu


Mtu asiyetubu anajua kwamba amefanya dhambi na anakataa kumwomba Mungu msamaha au kuacha dhambi. Wasiotubu hawaonyeshi majuto kwa ajili ya makosa yao na hawaoni haja ya kubadilika. Kutotubu ni dhambi ya makusudi ya kutaka kubaki mwenye dhambi.

Toba ni badiliko la nia ambalo huleta mabadiliko ya matendo. Toba huleta uzima (Matendo 11:18), na ni sehemu ya lazima ya wokovu. Mungu anaamuru kila mtu kutubu na kuwa na imani katika Kristo (Matendo 2:38; 17:30; 20:21). Kwa hivyo kutotubu ni dhambi kubwa yenye matokeo mabaya. Wasiotubu wanaishi katika hali ya kutomtii Mungu, na kutotii wito wake wa neema. Wasiotubu hubaki bila kuokolewa hadi wageuke kutoka kwa dhambi zao na kukumbatia dhabihu ya Kristo msalabani.

Mfalme Sulemani, mtu mwenye hekima zaidi aliyepta kuishi, aliandika, “Mtu anayeendelea kuwa na shingo ngumu baada ya maonyo mengi, ataangamia ghafula, wala hapati dawa” (Mithali 29:1). Kuwa na shingo ngumu ni kuwa na roho ya ukaidi, ambayo humfanya mtu asiitikie mwongozo au marekebisho ya Mungu. Wenye shingo ngumu, kwa ufafanuzi ni watu wasio na toba.

Mtume Paulo alionya kuhusu matokeo ya kutotubu: “Lakini kwa sababu ya ukaidi wenu na mioyo yenu isiyotaka kutubu, mnajiwekea akiba ya ghadhabu dhidi yenu wenyewe kwa siku ile ya ghadhabu ya Mungu, wakati hukumu yake ya haki itakapodhihirishwa. Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake. Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele. Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu. Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu wa Mataifa pia” (Warumi 2:5-9; linganisha Zaburi 62:12). Kuna hukumu inayokuja. Matokeo ya uadilifu yatakuwa mazuri, lakini matokeo ya kutotubu yatakuwa magumu.

Kitabu cha Ufunuo kinaonyesha jinsi mtenda-dhambi anavyoweza kuchochewa katika kutenda dhambi. Wakati wa dhiki, baada ya hukumu tatu tofauti za Mungu, wouvu bado watabaki bila kutubu, licha ya mateso yao makuu (Ufunuo 9:20-21; 16:8-11). Janga ni kwamba, hata kama baadhi ya watu wanapitia matokeo ya kutisha ya dhambi zao, wataendelea katika hali yao ya kutotubu.

Je, kunacho kitu kama Mkristo asiyetubu? Kibiblia, ili kuwa Mkristo, ni lazima mtu atubu na kuamini; anayeamini Kristo ni yule ambaye ametubu dhambi. Ni namna gani basi wale wanaodai kuwa wanaamini na wanaendelea kuishi katika dhambi hawajatubu? Kuna uwezekano mkubwa zaidi kuwa hawajaokolewa; wao wanakiri tu ile hali hawajaokolewa, na hamna kazi ya Roho Mtakatifu katika mioyo yao. Mtume Yohana anaeleza waziwazi: “Kama tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli” (1 Yohana 1:6). Uwezekano mwingine ni kuwa watu wanaodai kuwa wameokolewa ilhali wanaishi katika dhambi hawajaitubu wameokolewa lakini wanatembea katika uasi-ambapo kutotubu kwao ni ugumu wa moyo wa muda, na adhabu ya Mungu hatimaye itawarejesha katika ushirika (ona 1 Wakorintho 5:1-5).

Mtenda dhambi asiyetubu anapaswa kusikia habari njema ya wokovu wa Mungu. Wema wa Mungu huwaongoza watu kwenye toba (Warumi 2:4), na Yeye ni Mungu wa uvumilivu na ustahimilivu. Wakristo wanapaswa kuungama dhambi zao wenyewe, waombee wasiotubu, na kuhubiri Injili kwa wale ambao hawajaokoka: “Inampasa kuwaonya kwa upole wale wanaopingana naye, kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli, ili fahamu zao ziwarudie tena, nao waponyoke katika mtego wa ibilisi ambaye amewateka wapate kufanya mapenzi yake” (2 Timotheo 2:25-26).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Kutotubu ni nini? Je, inamaanisha nini kuwa mtu asiyetubu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries