settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kwamba mtu hatarithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9-11)?

Jibu


Kutajwa mara ya kwanza ya kutourithi ufalme wa Mungu kunapatikana katika barua ya kwanza ya Pualo kwa kanisa la Korintho. “Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyangʼanyi hawataurithi Ufalme wa Mungu. Baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu” (1 Wakorintho 6:9-11).

Kwa kusema waovu hawataurithi ufalme wa Mungu, Paulo anaeleza kwamba waovu si watoto wa Mungu, wala si warithi wa uzima wa milele (Warumi 8:17). Hii haimanishi kwamba mtu yeyote ambaye amewahi kutenda mojawapo ya dhambi hizi atanyimwa kuingia mbinguni. Kunachotofautisha maisha ya Mkristo na yale ya asiye Mkristo ni pambano dhidi ya dhambi na uwezo wa kuishinda. Mkristo wa kweli daima atatubu, hatimaye atarudi kwa Mungu na daima ataanzisha tena mapambano dhidi ya dhambi. Lakini Biblia haiungi mkono wazo la kwamba mtu anayefanya dhambi daima na bila kutubu anaweza kuwa Mkristo. Kifungu cha 1 Wakorintho kinaorodhesha dhambi ambazo, zikifanywa kila mara, zinamtambulisha mtu kuwa hajakombolewa na Kristo.

Itikio la Mkristo kwa dhambi ni kuichukia, kuitubu, na kuiacha. Bado tunapambana na dhambi, lakini kwa uwezo wa Roho Mtakatifu anayeishi ndani yetu, tunaweza kupinga na kushinda dhambi. Sifa moja ya Mkristo wa kweli ni kupungua kwa uwepo wa dhambi katika maisha yake. Kadiri Wakristo wanavyokua na kukomaa katika imani, dhambi inapungua sana kutushikilia. Bila shaka, ukamilifu usio na dhambi hauwezekani katika maisha haya, lakini chuki yetu kwa dhambi inakuwa kubwa zaidi tunapokomaa. Kama Paulo, tunahuzunishwa kwamba dhambi ingali ndani ya miili yetu, ikitufanya nyakati zingine kufanya yale ambayo hatutaki kufanya na kumtazamia Kristo kupata kitulizo katika “mwili huu wa mauti” (Warumi 7:18-25).

Ikiwa mtu ataendelea kuishi maisha ushoga, maisha ya wizi bila kutubu, maisha ya ulafi, maisha ya ulevi, n.k., mtu huyo anajionyesha kuwa hajaokolewa, na mtu kama huyo hakika hatarithi ufalme wa Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kwamba mtu hatarithi ufalme wa Mungu (1 Wakorintho 6:9-11)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries