settings icon
share icon
Swali

Je! Inamaanisha nini kuwa mtu asiyemcha Mungu? Kutomcha Mungu ni nini?

Jibu


Biblia inazungumza kuhusu “wasiomcha Mungu” kuwa wale waliotengwa na Mungu. Kutomcha Mungi ni hali ya kuchafuliwa na dhambi. Kukosa kumcha Mungu ni kutenda kwa njia ambayo ni kinyume na asili ya Mungu, kumpinga Mungu kikamilifu katika uasi au kutojali kumcha Mungu. Mara nyingi Biblia husema kuhusu “mwili” inaporejelea mambo yanayotokana na asili yetu ya dhambi. Matendo ya mwili na matamanio ya dunia yanaanguka chini ya kundi la kutomcha Mungu.

Waraka wa Pili wa Petro 3:7 inasema kwamba wasiomcha Mungu watahukumiwa. Ufunuo 20:14-15 inasema, “Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto.” Hatimaye wale watakao mkataa Mungu-wasiomcha Mungu- watatengwa Naye milele.

Yuda anawarejelea walimu wa uongo kuwa wasiomcha Mungu. Maelezo yake yana sifa hizi za kutomcha Mungu: wanageuza neema ya Mungu na kuwa kibali cha uasherati, na wanamkana Yesu Kristo kuwa si Mwenye Enzi Kuu na Bwana (Yuda 1:4). Baadaye, Yuda anataja “matendo ya wasiomcha Mungu” ya waovu na “maneno ya dhaarau” ambayo watu wasiomcha Mungu husema dhidi ya Mungu (mstari wa 15). Watu wasiomwogopa Mungu pia wanajulikana kuwa “wanung’unikaji na wenye kutafuta makosa” ambao kwa ubinafsi hufuata “tamaa zao mbaya,” hujisifu na kujipendekeza (mstari wa 16). Watu wasiomcha Mungu hudhihaki ukweli wa Mungu na kujaribu kugawanya makanisa (mistari ya 18-19).

Cha ajabu Yesu alijitoa kwa ajili ya watu wasiomcha Mungu. Warumi 5:6 na 8 inasema, “Kwa maana hata tulipokuwa dhaifu, wakati ulipowadia, Kristo alikufa kwa ajili yetu sisi wenye dhambi…. Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.” Mungu huwahesabia waovu haki (Warumi 4:5), akiwavisha haki ya Kristo na kuwawezesha “kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna” (Wakolosai 1:10).

Utakaso wetu ni wa kuendelea. Hiyo hata kama tumeokolewa na kutakaswa katika Kristo, wakati mwingine bado tunatenda kwa njia zisizo za Mungu. Bado tuko katika mchakato wa kubadilishwa na kuwa mfano wake (Warumi 8:29-30; 2 Wakorintho 3:18; Wafilipi 1:6). Tunatangazwa kuwa wenye haki mbele za Mungu lakini bado tunafanywa watakatifu kwa halisi. Kwa ufupi, bado tunatenda dhambi. Maandiko yanasema tunapaswa kuungama dhambi zetu na kutumaini msamaha wa Mungu (1 Yohana 1:8-9). Hakuna kinachoweza kututenganisha na upendo wa Mungu kwetu katika Kristo (Warumi 8:31-39). Hatumo tena miongoni mwa watu wasiomwogopa Mungu, ingawa bado tunapambana na tamaa zetu za kimwili na nyakati fulani tunatenda kwa njia zisizo za kimungu.

Kwa ujumla waovu ni wale wasiomjua Mungu kupitia Yesu Kristo. Wamemkataa Mwana wa Mungu na kubaki katika dhambi zao. Wale walio ndani ya Kristo wamesamehewa dhambi zao na wanazidi kuwa wacha Mungu. Waumini kwa kawaida hutafuta kuondoa uovu wote maishani mwao (1 Yohana 3:9).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Inamaanisha nini kuwa mtu asiyemcha Mungu? Kutomcha Mungu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries