settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu jaribio la kutengana kwa muda katika ndoa?

Jibu


Wanandoa wanapoingia katika agano la ndoa, Biblia inatuambia kwamba Mungu huwaunganisha pamoja na kuwa mwili mmoja. “Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” (Mathayo 19:6). Ndoa inakusudiwa kuwa ahadi ya maisha, si suluhisho la muda la upweke au mahitaji mengine ya kihisia-moyo. Mungu anachukia talaka (Malaki 2:16) na hataki wanandoa kutengana pindi tu baada ya kufunga ndoa (Mathayo 19:8).

Kwa sababu kutengana, kuwe ni halali au wa kimwili, kunahusisha mgawanyiko wa wenzi wa ndoa, na hiyo inamchukiza Mungu. Wakorintho wa kwanza 7:10-11 inasema, “Mke asitengane na mumewe. Lakini akitengana, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Wala mume asimpe mkewe talaka.” Kutengana kamwe sio hali bora, lakini kwa sababu ya dhambi, wakati mwingine ni muhimu. Ikiwa mwenzi au mtoto ananyanyaswa kimwili, kwa mfano, anapaswa kutafuta msaada mara moja nje ya kwao na kujitenga na mnyanyasaji hadi usaidizi ufaao na matibabu yawe yametolewa kwa wahusika wote (ona Makala yetu “Ni nini mtazamo wa kibiblia kuhusu unyanyasaji wa nyumbani?” kwa mengi kuhusu hili). Maombi na ushauri kutoka kwa mchungaji ni muhimu sana katika kurejesha ndoa na familia.

Nadhiri za ndoa hazipaswi kuchukuliwa kirahisi, na kutengana kusifanywe kwa kawaida. Wanandoa wengi sana huamua kuwa na “jaribio la kutengana” ili kugundua kile wanachotaka kweli maishani, lakini hufanya hivyo bila jaribio lolote la kujenga upya ndoa wakati huu. Badala ya kuijenga upya familia katika msingi wa imani katika Kristo, wanaenda mbali zaidi hadi wanatalikiana. Hili haliko katika mpango kamili wa Mungu wa ndoa na familia, hata kama umekubalika katika tamaduni fulani. “Furahia maisha na mke wako, umpendaye, siku zote za maisha ya ubatili uliyopewa na Mungu chini ya jua, siku zote za ubatili. Kwa maana hili ndilo fungu lako katika maisha na katika kazi yako ya taabu chini ya jua” (Mhubiri 9:9).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu jaribio la kutengana kwa muda katika ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries