settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini kila dhambi hatimaye huwa dhambi dhidi ya Mungu?

Jibu


Dhambi mara nyingi hudhuru mtu mwingine, na mwishoye dhambi zote zi kinyume na Mungu. Biblia in marejeo mengi ya watu wanakiri, “Nimetenda dhambi dhidi ya Bwana Mungu” (Kutoka 10:16; Yoshua 7:20; Waamuzi 10:10). Mwanzo 39:9 inatupa mtazamo wa karibu wa jambo hili. Yusufu alikuwa anajaribiwa kufanya uzinzi na mke wa Potifa. Katika kumpinga, alisema, “Bwana wangu hakunizuilia kitu chochote isipokuwa wewe, kwa kuwa wewe ni mke wake. Nitawezaje basi kufanya uovu huu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu?” inafurahisha kwamba Yusufu hakusema kwamba dhambi yake itakuwa dhidi ya Potifa. Hii haimaanishi kwamba Potifa hangeathirika. Lakini uaminifu mkuu wa Yusufu ulikuwa kwa Mungu na sheria zake. Ni Mungu hakutaka kuudhi.

Daudi alisema kitu kama hicho baada ya kufanya dhambi na Bathsheba (2 Samweli 11). Alipokabiliwa na dhambi yake, Daudi alitubu kwa huzuni kuu, akimwambia Mungu, “Dhidi yako, wewe peke yako, nimetenda dhambi” (Zaburi 51:4). Alikuwa ametenda dhambi waziwazi dhidi ya Bathsheba na mumewe, pia, lakini ilikuwa ni uvunjaji wa sheria ya Mungu uliomhuzunisha Daudi zaidi. Mungu anachukia dhambi kwa sababu ni kinyume cha asili yake na kwa sababu inatudhuru sisi wenyewe au mtu mwingine. Kwa kumtenda Mungu dhambi, Daudi alikuwa amewaumiza watu wengine pia.

Mtu anapofanya uhalifu, mtu ambaye aliumizwa na uhalifu huo si yule ambaye anamwadhibu mhalifu. Ni sheria ambayo inamhukumu mtu kuwa na hatia au hana hatai, sio mhasiriwa. Ni sheria iliyokiukwa. Bila kujali kustahili au kutokuwa na hatia kwa mhasiriwa, uhalifu wote hatimaye unafanywa kinyume na sheria iliyowekwa. Ukiiba kutoka kwa jirani yako, ni wazi umemdhulumu jirani yako, lakini si yeye anakuwajibisha. Ni sheria ya juu ambayo umekiuka. Serikali inabeba jukumu la kukutia hatiani na kukuadhibu; jirani yako, ingawa ameathiriwa na uhalifu wako, anatofautiana na serikali.

Vivyo hivyo, sheria zote za maadili huanza na Mungu. Kwa sababu tuliumbwa kwa mfano wa Mungu, tuna sheria yake ya maadili iliyoandikwa ndani ya mioyo yetu (Mwanzo 1:27). Adamu na Hawa walipokula tunda la mti waliokatazwa katika bustani mwa Edeni Mungu alisema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya” (Mwanzo 3:22). Wakati huo, hakukuwa na sheria andishi ilikuwa imetolewa, kadri tunavyojua. Lakini Mungu alikuwa amewasiliana waziwazi mapenzi yake kwa Adamu na Hawa, na walijua kwamba walikuwa wametenda dhambi na wakakimbia kujificha kutoka kwa Mungu (Mwanzo 3:10). Aibu yao baada ya kutenda dhmbi ilikuwa bayana kihisia.

Kihisia tunajua wakati tumefanya dhambi. Dhmbi ni upotoshaji wa mpango mkamilifu wa Mungu. Sisi sote tuna sura halisi ya Mungu Mwenyewe, na tunapotenda dhambi, tunaharibu mfano huo. Tuliumbwa ili tuwe vioo vya utukufu wa Mungu (Waefeso 2:10; 4:24; Waebrania 2:7). Dhambi ni uchafu mkubwa kwenye kioo, na inapunguza uzuri na utakatifu ambao tiliundwa kutafakari. Tunapotenda dhambi, tunatoka nje ya kusudi ambalo tiliumbwa kwalo, na hivyo kuvunja sheria ya maadili ya Mungu, na tunawajibika Kwake kwa kosa hilo. Warumi 3:23 inasema, “kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.” Dhambi ni kitu chochote kinachopungukiwa na mpango wa Mungu. Kwa hivyo, iwe inatudhuru sisi au mtu mwingine, kila dhambi ni dhidi ya Mungu mtakatifu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini kila dhambi hatimaye huwa dhambi dhidi ya Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries