settings icon
share icon
Swali

Je! Ni dhambi kutazama ponografia na mwenzi wangu?

Jibu


Kwa kuenea kwa mtandao na kupungua kwa viwango vya maadili ya jamii, ponografia inashudiwa kila wakati na watu wengi. Hata wenzi wa ndoa Wakristo nyakati zingine hujiuliza ikiwa ponografia inaweza kuwa na sababu ya kusaidia ikiwa inatazamwa na mwenzi wa ndoa kama sehemu ya uhusiano wao wa kibinafsi. Baadhi ya wanandoa wanahisi hitaji la kufanya uhusiano wao wa kingono kusisimuka zaidi na wanaamini kwamba kutazama ponografia pamoja huongeza kufurahia kwa uhusiano wao wa kingono. Ponografia huvutia tamaa ya macho na tamaa ya mwili. Tunajua kwamba tamaa imehukumiwa katika Maandiko (Ayubu 31:1 Mathayo 5:28), lakini ikiwa uhusiano wa ngono ni wa mume na mke tu, je kutazama ponografia na mwenzi ni kosa?

Naam, kutazama ponografia ni dhambi kwa sababu nyingi, hata inatazamwa pamoja na mwenzi wa ndoa. Kwanza kabisa, ponografia ya kutizamwa huchukua nafasi ya muungano wa kipekee, wa karibu na kuifanya kuwa mchezo wa kushabikiwa. Kwa ufafanuzi, ponografia inahusisha angalau watu wawili ambao hawajafunga ndoa wanaojihusisha na tabia haramu ya ngono mbele ya kamera. Mungu alipanga urafiki huu kwa mume na mke pekee (Mathayo 19:5; Waefeso 5:31). Matendo ya ngono, kwa asili, ni ya faragha. Wale wanaofanya mioyo yao kuwa migumu kiasi kwamba wanaweza kufanya vitendo hivyo vya faragha mbele ya watazamaji wanatumia vibaya mpango wa Mungu. Na wale wanaofurahia kutazama ponografia wanashiriki katika utumizi huo mbaya. Andiko la Warumi 1:32 linaweza kutumika hapa, kwa vile linafafanua hali ya kushuka kwa maadili ya wale wanaompinga Mungu: “Ingawa wanafahamu sheria ya haki ya Mungu kwamba watu wanaofanya mambo kama hayo wanastahili mauti, si kwamba wanaendelea kutenda hayo tu, bali pia wanakubaliana na wale wanaoyatenda.”

Sehemu nyingine mbaya ya kutazama ponografia na mwenzi ni kwamba kufanya hivyo huwaalika wageni kwenye chumba chako cha kulala. Inaunda utatu halisi; ilhali huenda usifikirie kamwe kuwa ni kushiriki kimwili katika mpangilio wa ngono kati ya watu watutu, unafanya hivyo katika akili zao. Kutazama ponografia na mwenzi wako ni aina fulani ya uzinzi. Ni kana kwamba mtu anasema, “Mwenzi wangu hapendezi vya kutosha, kwa hiyo nimemwalika mgeni wa ngono kutusaidia tunapofanya ngono.” Wenzi wa ndoa wanaweza kuwa wananapapasana kimahaba, lakini kiakili wanapapasa miili ya wageni wazinzi. Hakuna kitu kuhusu hilo kinachompendeza Bwana kwa njia yoyote ile. Yesu alisema, “Heri walio na moyo safi, maana hao watamwona Mungu.” Hakuna vile unaweza kuhurusu moyo wako kula kutoka kwa uchafu, picha za ponografia na ubaki kuwa msafi ya kutosha kumwona Mungu.

Sababu ya tatu na ya wazi kwamba kutazama ponografia nyakati zote ni mbaya, iwe uko na mwenzi wako au uko pekee yako, ni kwamba, msukumo wa kufanya hivyo ni tamaa (Wakolosai 3:5; Mathayo 5:28). Tamaa ni haja nzito sana ya kitu ambacho Mungu amekataa (Mithali 6:25). ikiwa kuona uchi wa watu wengine kunahitajika ili utamani ngono na mwenzi wako, basi hiyo ni tamaa. Kutazama ponografia ni kumpa Shetani nafasi kuingia akilini mwetu, kuharibu mioyo yetu, na kukiita kuwa “uchafu” kile ambacho Mungu amekiita “kizuri” (Mwanzo 1:26-31).

Mipaka ya Mungu ya ngono ni kwa usalama na ustawi wetu. Ipo ili kulinda familia zetu na mioyo yetu wenyewe. Mungu anatazamia tujidhibiti katika Nyanja zote za maisha, pamoja na ngono (Mithali 25:28; 1 Wakorintho 7:9). Tunaporuhusu tamaa, ujinsia, au tamaa yoyote kututawala, tunakabidhi ubwana wa maisha yetu kwa kitu kingine isipokuwa Yesu.

Tamaa ya kutizama ponografia ni ishara dhahiri kwamba vipaumbele vimeenda mrama. Msisimko wa kijinsia umekuwa muhimu ziadi kuliko urafiki wa kiroho, uhusiano wa kihisia, au kuheshimiana. Mara nyingi, mwenzi mmoja husukuma wazo la kutazama ponografia, ambalo mwenzi mwingine anakubali tu ili kudumisha amani. Lakini hii ni ukiukaji wa amri ya Mungu ya kunyenyekeana kwa heshama kwa Kristo (Waefeso 5:21). Kristo hatawahi kumwomba mtu kufurahia na kushiriki katika dhambi ile ile aliyokufa ili kuisamehe (Waefeso 5:22). Upendo “haufurahii uovu” (1 Wakorintho 13:6). Kuna njia bora zaidi za kuungana tena na mwenzi kuliko kukaribisha dhambi katika uhusiano. Kutazama ponografia peke yako au na mtu mwingine yeyote, ikiwa ni pamoja na mwenzi wa ndoa, ni dhambi.

Wathesalonike wa kwanza 4:3-7 ni muhimu leo hii kama vile ilivyokuwa wakati ilipoandikwa, na tunaweza kutumia ukweli wake kwa dhana ya kutazama ponografia na mwenzi wa ndoa: “Mapenzi ya Mungu ni kwamba ninyi mtakaswe, ili kwamba mjiepushe na zinaa, ili kwamba kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu. Katika jambo hili mtu asimkosee ndugu yake wala kumlaghai. Kwa kuwa Bwana ni mlipiza kisasi katika mambo haya yote, kama vile tulivyokwisha kuwaambia mapema na kuwaonya vikali. Kwa maana Mungu hakutuitia uchafu, bali utakatifu.” Mungu anatuita kwa utakatifu, na ponografia si takatifu; kwa hiyo, sio makusudi ya Mungu kamwe kwetu kujihusisha na ponografia kwa sababu yoyote ile.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni dhambi kutazama ponografia na mwenzi wangu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries