settings icon
share icon
Swali

Je ninapaswa kuangalia nini kwa mke?

Jibu


Uhusiano muhimu zaidi wa binafsi kwamba mume anaweza kuwa nao, nje ya uhusiano wake wa kiroho na Mungu kwa njia ya Bwana Yesu Kristo, ni uhusiano wake na mke wake. Katika harakati ya kumtafuta mke, kanuni kuu ni kumtafuta mwanamke mwenye imani ya kibinafsi kwa Yesu Kristo. Mtume Paulo anatuambia kuwa "tusitiwe nira" pamoja na wasioamini (2 Wakorintho 6:14). Ijapokuwa tu kama mume na mke wako katika mkataba kamili juu ya suala hili muhimu zaidi, ndoa ya uungu na ya uridhisho hauwezi kufanyika.

Hata hivyo, kuoa muumini mwenzetu haina dhamana kamili ya "kutiwa nira pamoja." Ukweli ni kwamba mwanamke ni Mkristo haimaanishi kuwa yeye ni mwenzi sawia kiroho. Je, yeye ana malengo sawia ya kiroho kama wewe? Je, yuu na mafundisho sawia na wewe ya imani? Je, yeye yuu na hisia kali kwa Mungu? sifa za mke mwema ni muhimu sana. Wanaume wengi mno huoa kwa hisia au mvutio wa mwili pekee, na hiyo inaweza kuwa kichocheo cha kushindwa.

Ni baadhi gani ya sifa za uungu mume anaweza kuangalia katika mke? Maandiko yanatupa baadhi ya kanuni tunaweza kutumia ili kuwa na picha ya mwanamke mcha Mungu. Yeye lazima awe mtiivu katika uhusiano wake mwenyewe wa kiroho na Bwana. Mtume Paulo anaelezea kuwa mke anastahili kumtii mumewe kwa Bwana (Waefeso 5:22-24). Kama mwanamke si mtiivu kwa Bwana, yeye hawezi ona utiivu kwa mume wake kama jambo muhimu kwa manufaa yake mwenyewe kwa ustawi wa kiroho. Hatuwezi kutimiza matarajio ya mtu mwingine bila kwanza kuruhusu Mungu kutujaza na utu wake. Mwanamke ambaye Mungu ndiye chanzo cha maisha yake ni mhitimu mzuri kuwa mke.

Paulo pia anatoa baadhi ya sifa za tabia kwa mwanamke katika maelekezo yake kuhusu viongozi katika kanisa. "Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote" (1 Timotheo 3:11). Kwa maneno mengine, huyu ni mwanamke ambaye amaejawa na kiburi, anajua wakati nafasi ya kuzungumza na wakati wa kuwa kimya, na ana uwezo wa kuchukua nafasi yake karibu na mume wake kwa kujiamini. Yeye ni mwanamke ambaye kwanza lengo ni uhusiano wake na Bwana na ukuaji wake mwenyewe kiroho.

Majukumu ya ndoa ni makubwa kwa mume, mpango wa Mungu humuweka kuwa kichwa cha mke wake na familia yake. Uongozi unafuata ule wa uhusiano kati ya Kristo na Kanisa (Waefeso 5:25-33). Ni uhusiano msingi waake uu katika upendo. Tu kama viel Kristo alivyolipenda kanisa, akajitoa nafsi yake kwa ajili yake, vivyo hivyo mume anafaa kumpenda mke wake kama anavyojipenda mwenyewe. Kwa hiyo, uhusiano wa mume binafsi kiroho na Bwana ni wa umuhimu mkuu katika mafanikio ya ndoa yake na familia yake. Sadaka ya hiari na nguvu ya kuchagua kuwa mtumishi bora katika ndoa yake ni alama ya ukomavu wa kiroho ambaye anamheshimu Mungu. Kwa busara kuchagua mke kwa msingi wa sifa ya Biblia ni muhimu, lakini umuhimu bali la muhimu zaidi ni mume kuendelea kukua mwenyewe kiroho na kujisalimisha kwake kwa mapenzi ya Mungu katika maisha yake. mtu ambaye anatafuta kuwa mume ambaye Mungu anamtaka awe atakuwa na uwezo wa kusaidia mke wake kuwa mwanamke Mungu anatamani yeye awe na atakuwa na uwezo wa kujenga ndoa katika muungano ambao Mungu anawataka yeye na mke wake wawe.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je ninapaswa kuangalia nini kwa mke?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries