settings icon
share icon
Swali

Je, ninawezaje kuwa na matumaini wakati kupata kazi nzuri inaonekana kuwa haiwezekani?

Jibu


Cha muhimu kutambua katikati ya hali ambazo zinaonekana kuwa haziwezekani-kama vile kupata kazi nzuri-ni kwamba, tunaposalimisha tatizo kwa udhibiti wa Mungu, linaingia moja kwa moja katika ulimwengu wa yanayowezekana, kwa sababu kwa Mungu yote yanawezekana (Mathayo 19:26).

Neno la Mungu linapita hali zote. Haijalishi tunakabiliana na nini katika maisha yetu, bado tunaweza kuamini kile ambacho Mungu anasema kuhusu Yeye Mwenyewe. Jambo moja tunalojua kuhusu Mungu ni kwamba Yeye husikia maombi yetu na anajua tunachohitaji hata kabla hatujamwomba (Mathayo 6:7-8). Tumeamriwa tusiwe na wasiwasi juu ya siku zijazo kwa sababu hizo hizo: Mungu anajua mahitaji yetu, na Yeye ndiye mtoaji wetu (Mathayo 6:25-34). Kutokuwa na wasiwasi haimaanishi kutochukua hatua, lakini kutambua tu kwamba Mungu ndiye anayetawala na kwamba ana nia nzuri kwetu (Warumi 8:28). Hata wakati hatuoni chochote kikitendeka, tunaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu anafanya kazi kwa bidii kwa niaba yetu. Yeye hajakaa bila kufanya kazi (ona Ruthu 3:18).

Kutambua kwamba Mungu alisema atatuandalia ni jambo moja, hata wakati hatuwezi kupata ajira. Ni jambo lingine kabisa kuweza kupata amani na tumaini iliyogubikwa katika ukweli huo.

Kukata tamaa mara nyingi huwa ni suala la moyo. Swali zuri la kujiuliza ni je, ninaelekeza akili yangu na mawazo kwa: shida au kwa Mungu? Huku haja yetu kuu huenda ikawa kupata kazi nzuri, Mungu anajali zaidi ya kuhusu hali ya mioyo yetu (ona 1 Samweli 16:7). Wafilipi 4:4-7 inasema, “Furahini katika Bwana siku zote, tena nasema furahini! Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.” Tunapochagua kumsifu na kumshukuru kwa hiari katikati mwa kutafuta kwetu ajira, tunafungua mioyo yetu na akili zetu kupokea amani Yake.

Ni muhimu pia kutambua kwamba, ingawa Mungu ana mipango miema kwa kila mmoja wetu (Yeremia 29:11), sisi pia tuna adui Shetani ambaye hatapenda chochote zaidi ila kutuvunja moyo kutoka kwa kumwamini Mungu kutimiza mipango hiyo kwa maisha yetu. Biblia inamfafanua Shetani kuwa “huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza” (1 Petro 5:8). Njia rahisi ya simba kumwinda mnyama kwanza anamtenga kutoka kwa kundi. Ni rahisi mno kwa Shetani kutuvunja moyo wakati tumetengana na Mwili wa Kristo. Kuwa na watu wacha Mungu katika maisha yetu ambao wanajua kile tunachopitia na wanaoweza kuomba nasi na kutuombea wakati hali ni ngumu inatia moyo sana (ona Waebrania 10:24-25; Yakobo 5:16).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ninawezaje kuwa na matumaini wakati kupata kazi nzuri inaonekana kuwa haiwezekani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries