settings icon
share icon
Swali

Je, ni makosa kumswali Mungu?”

Jibu


Suala kuu siyo kuwa hatupaswi kumhoji Mungu, lakini kwa namna gani au kwa sababu gani tunamswali. Hamna makosa katika kumswali Mungu. Nabii Habakuki alikuwa na maswali kwa Mungu kuhusu wakati na shirika la mpango wa Bwana. Habakuki, badala ya kukemewa kwa maswali yake, anajibiwa kwa uvumilivu, na nabii mwisho wa kitabu chake anamaliza kwa wimbo wa sifa kwa Bwana. Mungu anaulizwa maswali mengi (Zaburi 10, 44, 74, 77). Hivi ni vilio vya anayeteswa akitamani Mungu aingilia kati kwa wokovu. Ingawa Mungu wakati mwingine hajibu maswali yetu kwa njia tunataka, tunahitimisha kutoka katika vifungu hivi kwamba swali dhati kutoka kwa moyo limekaribishwa na Mungu.

Maswali ya unafiki, au maswali kutoka kwa moyo wa wanafiki, ni jambo tofauti. “Na pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa sababu mtu yeyote ambaye huja kwake ni lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba yeye huwapa tuzo wale wanaomtafuta kwa kweli” (Waebrania 11:6). Baada ya Mfalme Sauli hakumtii Mungu, maswali yake hayakujibiwa (1 Samweli 28:6). Ni tofauti kabisa kushangaa ni kwa nini Mungu aliruhusu tukio fulani zaidi kuliko kuswali wema wa Mungu. Kuwa na mashaka ni tofauti na kuhoji utawala wa Mungu na kushambulia tabia yake. Kwa kifupi, swali aminifu sio dhambi, bali nikuwa na uchungu, shauku, au waasi moyo ndio dhambi. Mungu sio wa kutishwa na maswali. Mungu anatualika kufurahia ushirika wa karibu naye. Wakati “tunamswali Mungu”,ni lazima tuulize kutoka kwa roho ya unyenyekevu na nia ya wazi. Tunaweza swali Mungu, lakini hatupaswi kutarajia jibu kama nia yetu si ya dhati na jibu lake. Mungu anajua mioyo yetu, na anajua kama sisi tu dhati kwa kumtafuta ili atuelimishe. Tabia ya moyo wetu ni ndio inaamua kama tu sahihi au makosani kwa kumswali Mungu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni makosa kumswali Mungu?”
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries