settings icon
share icon
Swali

Je, mtazamo wa Kikristo wa kustaafu ni upi?

Jibu


Wakristo wanapokaribia umri wa kustaafu, wao mara nyingi hustaajabu ni nini Mkristo anapaswa kufanya katika miaka ya kustaafu. Je, Wakristo hustaafu kutoka huduma ya Kikristo wakati wao hustaafu kutoka mahali pa kazi?

Jinsi gani Mkristo anapaswa kutazama kustaafu?

1) Ingawa hakuna kanuni za Biblia kwamba mtu anatakiwa kustaafu kutokana na kazi yake wakati yeye hufika umri fulani, kuna mfano wa Walawi na kazi zao katika hema. Katika Hesabu 4, wanaume Walawi wemehesabika kwa ajili ya huduma katika hema kuanzia umri na umri wa miaka 25-50, na baada ya umri wa miaka 50, walikuwa wanastaafu kutoka huduma ya mara kwa mara. Waweze kuendelea na "kuwasaidia ndugu zao" lakini hawakuweza kuendelea kufanya kazi (Hesabu 8: 24-26).

2) Hata ingawa tunaweza kustaafu kutoka wito wetu (hata "ya muda" huduma ya Kikristo), sisi kamwe hustaafu kutoka kumtumikia Bwana, ingawa njia sisi humtumikia inaweza kubadilika. Kuna mfano wa watu wawili wa zamani sana katika Luka 2: 25-38 (Simeoni na Anna) ambao waliendelea kumtumikia Bwana kwa uaminifu. Anna ambaye ni mjane mzee ambaye alihudumu katika hekalu kila siku na kufunga na kuomba. Tito 2 inasema kwamba wanaume wazee na wanawake wanapaswa kufundisha, kwa mfano, wanaume vijana na wanawake jinsi ya kuishi.

3) Miaka ya uzee ya mmoja haipaswi kutumika kwa kutafuta raha. Paulo anasema kwamba mjane ambaye anaishi kwa anasa, amekufa ingawa yeye bado anaishi (1 Timotheo 5: 6). Kinyume na mafundisho ya Biblia, watu wengi hulinganisha kustaafu kwa "kutafuta furaha" kama inawezekana kwa vyovyote vile. Huku si kusema kwamba wanaostaafu hawawezi kufurahia kikamilfiu, burudani za sherehe, au shughuli za furaha. Lakini hizi hazipaswi kuwa lengo la msingi la maisha ya mtu katika umri wowote.

4) Wakorintho wa Pili 12:14 inasema kwamba mzazi anapaswa kuweka akiba kwa ajili ya watoto. Lakini la muhimu zaidi la "kueka akiba" ni urithi wa kiroho wa mtu, ambao unaweza kupitashwa kwa watoto, wajukuu, na vitukuu. Vizazi vya wana vimeathiriwa na sala za mzee mwaminifu wa familia awe wa upande wa "baba" au "mama." Maombi labda ndoo matunda zaidi ya huduma kwa wale ambao wamestaafu.

Mkristo kamwe haastaafu kutoka huduma ya Kristo; yeye anabadilisha mahali pa kazi yake. Kwa muhtasari, mmoja anapofika "umri wa kustaafu" (chochote kile) wito unaweza kubadilika lakini maisha ya mtu ya kuhudumia Bwana hayabadilik. Mara nyingi ni hawa "watu andamizi" ambao, baada ya maisha ya kutembea na Mungu, wana uwezo wa kutangaza ukweli wa Neno la Mungu kwa kuhusisha jinsi Mungu amefanya kazi katika maisha yao. Sala ya mtunzi wa zaburi lazima iwe maombi yetu kama tunapokuwa wazee: "Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, na kila atakayekuja uweza wako" (Zaburi 71 : 18).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, mtazamo wa Kikristo wa kustaafu ni upi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries