settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inasema nini kuhusu kushughulikia majuto?

Jibu


Majuto ni husuni au huruma juu ya kitu ambacho kimeshafanyika au tumefanya. Majuto pia yanaweza kuwa kiwango cha masikitiko kwa kitu ambacho kimekwisha tendeka, kama vile kujuta miaka ambayo ulipoteza. Kuwa na majuto ni kawaida ya mwanadamu kwa sababu kufanya makossa ni usoefu wa kila mahali. Biblia inatupa maagizo mengi ambayo ikiwa yatafuatwa kutakuwa na majuto kidogo. Amri ya Mungu na mipaka yake imeandikwa kwa ajili yetu katika Neno lake, na tunavyo zifuata zaidi, kadri tunavyokosa kujutia. Ingawa, katika neema na huruma za Mungu, ametoa njia ya kushughulikia majuto wakati tumekosa kuishi kwa busara jinsi anavyotutaka tuishi (ona Zaburi 51:12).

Katika kufikiria kile ambacho Biblia inasema kuhusu majuto, ni lazima tuanze na kweli kwamba katika mahali kwingi tunaambiwa kuwa Mungu “alijuta” kwa hatua Aliyoichukua. Shina la neno la Kiebrania “majuto” hakika linamaanisha “kutamani.” Kwa kuwa tunajua Mungu hafanyi makossa, dhana ya kutamani ni neno la kimaelezo jinsi Mungu alijuta. Mwanzo 6:7 inasema kwamba, baada ya kuona uovu duniani, Mungu alijuta kwa kumuumba mwanadamu. Hii haimaanishi kwamba Bwana alihisi kwamba lifanya makossa katika kuwaumba wanadamu, lakini kwamba moyo Wake ulikuwa na huzini aliposhuhudia mwelekeo waliochukua. Kwa kuwa Mungu anajua kila kitu kabla, tayari alijua kwamba dhambi ingeleta madhara, kwa hivyo hakushangazwa nayo (1 Petro 1:20; Waefeso 1:4; Isaya 46:9-11). Badala yake, mtazamo huu wa tabia ya Mungu unatuonyesha kwamba, ingawa tayari anajua kwamba tutatenda dhambi, bado inamhuzunisha tunapoichagua (Waefeso 4:30).

Majuto ya mwanadamu ni tofauti na majuto ya Mungu. Majuto ya mwanadamu hutokea kwa sababu hatujui mambo yote na huwa tunafanya makosa. Tunaposeeka, mara nyingi tunayaangalia maamuzi tuliyofanya katika ujana wetu na kujutia maamuzi yetu. Walakini, majuto hayo kawaida huanguka katika moja ya aina mbili. Majuto yetu hutokana na uchaguzi wa kipumbavu au uchaguzi wa dhambi, na kila moja linahitaji jibu tofauti.

Kwanza, tunaweza kujuta kwa sababu ya maamuzi ya kipumbavu, hali ambazo tulitamani zingekuwa tofauti hapo zama. Kwa mfano, hbut na tusema tulikuwa tumechagua kuhudhuria Chuo cha Z na kusomea X. Baada ya miaka bila mafanikio katika taaluma X, tunajutia uamuzi huo wa shuleni. Chaguo la masomo katika chuo haukuwa dhambi, na huenda katika wakati huo tulidhani kuwa ulikuwa uamuzi bora, lakini sasa tunagundua kwamba haukuwa. Tunaweza kushughulikia aina hiyo ya majuto kwa kukiri Warumi 8:28 na kumuuliza Bwana afanye kazi kwa wema wetu. Tunaweza amua kuzingatia sehemu chanya ya yote tuliyojifunza na kuamini kwamba ikiwa tulikuwa tunamtafuta Bwana wakati huo, hakuna kitu kilichoharibika na anaweza kutumia hata maamuzi yetu ambayo hayajakomaa kwa manufaa yetu ikiwa tunamwamini. Tunaweza kujisamehe wenyewe kwa uamuzi wetu ambao ahujakomaa na kusudi la kukua na hekima kutokana nay ale tuliyojifunza (Wafilipi 3:13).

Petro ni mfano mmoja wa kibiblia wamtu ambaye alijuta sana uamuzi wa kipumbavu. Ingawa Petro alikuwa amjitoa kwa Yesu, woga wake ulimfanya akimbie askari walipokuja kumkamata Yesu, na baadaye akamkana Bwana wake. Matendo yake hayakutokana na tamaa ya kutenda dhambi, bali kutokana na mhemko, kutokomaa kiroho, na woga. Alijutia sana matendo yake na akalia kwa uchungu (Luka 22:62). Yesu alijua kuhusu majuto ya Petro na aliomba hasa kumyona baada ya kufufuka kwake (Marko 16:7). Tunajifunza kutokana na hili kwamba majuto yetu hayajafichwa kwa Mungu na anatatamni kuturudisha tunapomrudia (Malaki 3:7; Yeremia 24:7).

Majuto mengine huwa ni kwa sababu ya chaguzi za dhambi ambazo zinaweza kuwa zimeacha kidonda na madhara. Baada ya maisha mapotovu ya ubinafsi, baadhi ya watu katika miaka yao ya baadaye wanalemewa sana na majuto na hawawezi kupata furaha. Matokeo ya dhambi yao kwao wenyewe na wengine yanaweza kuwatesa kwa miaka mingi. Maumivu ya majuto yanaweza kutusukuma kufanya maamuzi ambayo pengine hatungefanya. Yuda Iskariote ni mfano mmoja katika Biblia. Baada ya kutambua kwamba alikuwa amemsaliti Masihi, Yuda alijawa na majuto hata akajaribu kutendo yake kwa kurudisha pesa za damu. Wakati hilo halikufaulu alitoka na kujiua (Mathayo 27:3-5).

Majuto yanaweza kuongoza kwa maangamizi ya kibinafsi, lakini Mungu anataka kuyatumia ili kutuongoza kwenye toba. Ni muhimu kuelewa kwamba majuto si sawa na toba. Esau alijutia sana uamuzi wake wa kuuza haki ya mzaliwa wa kwanza, lakini kamwe hakutubu dhambi yake (Waebrania 12:16-17). Majuto huzingatia hatua ambayo imeleta huzini; toba inamlenga yule tuliyemkosea. Wakorintho wa Pili 7:10 inaelezea tofauti kati ya majuto tu na toba ya kweli: “Kwa maana huzuni ya kimungu huleta toba iletayo wokovu na wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti.” Badala ya kuruhusu majuto kushinda, tunaweza kumruhusu Yesu kutubadilisha ili kwamba maamuzi ya kidhambi yetu ya kale yanaweza kutukuza neema yake yenye nguvu. Tunapokuja Kwake kwa toba, tukiamini kwamba dhabihu Yake msalabani ilikuwa malipo ya kutosha kwa ajili ya deni tunalodaiwa na Mungu, tunaweza kusamehewa (2 Wakorintho 5:21; Warumi 10:9-10; Matendo 2:23).

Wanaume wawili walimsaliti Yesu usiku ule aliosulubiwa. Yuda alikuwa na huzuni ya kidunia (majuto), na maisha yake yakaisha. Petro alikuwa na huzini ya kimungu (toba), na maisha yake yakabadilishwa. Tuna chaguo sawia na hao wanaume. Tunapokabiliana na majuto, tunaweza kuyaacha yagubike maisha yetu, au tunaweza kuweka makosa yetu miguuni pa Yesu, tuyaache na aturejeshe (Zaburi 23; 2 Wakorintho 5:17).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inasema nini kuhusu kushughulikia majuto?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries