settings icon
share icon
Swali

Je, kushahawa ndotoni / shahawa usingizini ni dhambi?

Jibu


Ndoto chuchulia/kushahawa usiku ni kitu cha kawaida katika maisha ya mwanaume. Biblia inajataja “kushahawa” katika maeneo chache (Walawi 15:16, 18,32; 22:4; Kumbukumbu 23:10). Haswa zinarejelea kushahawa: “Wakati mtu akitokwa na shahawa, ni lazima aoge mwili mzima kwa maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.” Vijana wengi (na wanaume wazee) hupambana na dhana hii. Je! Ndoto chuchulia/kushahawa usiku ni dhambi? Je! Ni namna gani inaweza kuwa dhambi ikiwa hatuwezi kuizuia?

Hatimaye, hatuwezi kudhibiti kile tunachoota au kile kinachotokea kwa miili yetu tukiwa tumelala. Walakini, ikiwa tunajaza akili zetu na mambo ya ashiki/dhambi wakati wa mchana, kuna uwezekano kwamba yatatokea katika ndoto zetu. Ushahawa nyakati za usingizi ni kazi asili ya mwili ambayo hufanyika mara kwa sababu ya nyege kupita kiasi. Ushahawa usiku si dhambi, lakini inaweza kuwa ni matokeo ya mawazo ya dhambi, tamaa, na michango yetu. Ikiwa unashahawa usiku chunguza mawazo yako. Chunguza aina ya picha unazotazama. Ikiwa utapata kuwa umejiruhusu “kuibua hisia” kwa tamaa, kiri hilo kwa Bwana na uliza usaidizi wake katika kushinda jaribio hilo. Katika hali kama hiyo, ndoto ya shahawa/kujichuchulia usiku ni matokeo ya dhambi, lakini katika kitendo chenyewe sio cha dhambi. Fuata maneno ya Wafilipi 4:8, “Hatimaye, ndugu zangu, mambo yote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo na sifa njema, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote ya kupendeza, yoyote yenye staha, ukiwepo uzuri wowote, pakiwepo chochote kinachostahili kusifiwa, tafakarini mambo hayo.”

Ikiwa unapata kuwa kushahawa usiku/ndoto za kucjihuchulia kiasili ni matokeo ya mwili “kujipunguzuia hisia,” haupaswi kukiri chochote kwa Bwana. Sheria ya Agano la Kale ilikuwa ya kiitikadi katika kutibu ushahawa wowote kwa wanaume na wanawake. Kwa bahati nzuri, hatufungwi na kanuni hizi. Mwanamume ambaye amaekuwa na ndoto ya kushahawa sio “unajisi.” Vile vile, jambo ni kile kinachoendelea katika akili yako. Mwitikio wa miili yetu ni matokeo ya kile kinachotokea katika akili zetu (Mathayo 12:34-35).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kushahawa ndotoni / shahawa usingizini ni dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries