settings icon
share icon
Swali

Je, tunapaswa kumpenda mwenye dhambi lakini tuchukie dhambi?

Jibu


Wakristo wengi wanatumia maneno matupu "Penda mwenye dhambi, chukia dhambi." Hata hivyo, ni lazima tutambue kwamba hii inatushawishi kama binadamu wasiowakamilifu. Tofauti kati yetu na Mungu katika suala la kupendo na kuchukia ni kubwa. Hata kama wakristo, tunabakia kuwa wasio kamili katika ubinadamu wetu na hatuwezi kupenda kikamilifu, wala hatuwezi chuki kikamilifu (kwa maneno mengine, bila uovu). Lakini Mungu anaweza kufanya yote mawili kikamilifu, kwa sababu yeye ni Mungu. Mungu anaweza chukia bila dhamira yoyote ya dhambi. Kwa hivyo, anaweza kuchukia dhambi na mwenye dhambi katika njia kamilifu takatifu na bado kuwa na nia ya kumsamehe kiupendo kwa wakati wa toba na imani ya mwenye dhambi i (Malaki 1: 3; Ufunuo 2: 6, 2 Petro 3: 9).

Biblia inafunza wazi wazi kwamba Mungu ni upendo. 1 Yohana 4: 8-9 inasema, "Yeyote asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo. Hii ni jinsi gani Mungu alionyesha upendo wake kwetu: Yeye alimtuma Mwana wake wa pekee ulimwenguni, ili tuwe na uzima kwa njia yake "Kiajabu lakini ni kweli ni ukweli kwamba Mungu anaweza kikamilifu kupenda na kuchukia mtu wakati huo huo. Hii ina maana Yeye anaweza kumpenda kama mtu aliyemuumba na anaweza kumkomboa,vile vile amchukie e kwa sababu ya kutoamini kwake na maisha ya dhambi. Sisi, kama wanadamu wasio wakamilifu , hatuwezi kufanya hivi; hivyo, lazima tujikumbushe wenyewe kwa "penda mwenye dhambi, chukia dhambi."

Jinsi gani hakika hiyo inafanya kazi? Tunachukia dhambi kwa kukataa kushiriki kwayo na kwa kuilaani tunapoiona. Dhambi inapaswa kuchukiwa, si kuwiwa radhi au kuchukuliwa hivi hivi. Tunawapenda wenye dhambi kwa kuwa waaminifu katika kushuhudia kwao kuhusu msamaha unaopatikana kwa njia ya Yesu Kristo. Tendo la kweli la upendo ni kumhudumia mtu kwa heshima na wema hata kama yeye anajua hauthibitishi maisha yake na / au maamuzi. Si kupendo kwa kuruhusu mtu kubaki amekwama katika dhambi. Haichukizi kumwambia mtu kuwa ako katika dhambi. Kwa kweli, kinyume halisi ni kweli. Tunapenda mwenye dhambi kwa kusema ukweli katika upendo. Tunachukia dhambi kwa kukataa mzaha wake, kupuuza, au kuipa udhuru.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, tunapaswa kumpenda mwenye dhambi lakini tuchukie dhambi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries