settings icon
share icon
Swali

Je, kunayo msingi wowote wa kimaandiko wa kuombea ambao hawajaokoka?

Jibu


Wakristo ni watu wa maombi (1 Wathesalonike 5:17), na baadhi ya maombi yetu yanahusu hali ya kiroho ya marafiki na jamaa ambao hawajaokoka. Tunataka waokolewe, na tunasali kwa ajili hiyo. Katika hili tunakubaliana na Charles Spurgeon, aliyesema, ”Ikiwa wenye dhambi watahukumiwa, angalau waruke kuzimu juu ya miili yetu iliyokufa. Na ikiwa wataangamia, wacha waangamie na huku mikono yetu ikiwa imefungwa kwenye magoti yao, tukiwasihi wabaki. Ikiwa Jahannamu lazima ijazwe, naijae baada ya bidii meno yetu, na mtu yeyote asiende bila kuonywa na bila kuombewa.”

Tunapaswa kuwaombea wale ambao hawajaokoka. Mwokozi wetu alikuja kutafuta na kuokoa waliopotea (Luka 19:10), na mada kuu ya Injili ya Luka ni rehema ya Kristo kwa wale ambao mara nyingi wanachukuliwa kuwa watu waliotengwa katika Israeli. Mwokozi wetu “anayetaka watu wote waokolewe na wafikie kujua kweli” (1 Timotheo 2:4), kwa hiyo tunaposali kwa ajili ya wokovu wa mtu ambaye hajaokolewa, tunahsiriki nia ya Yesu iliyotajwa.

Tunapaswa kuwaombea ambao hawajaokolewa kwa sababu, ukweli ni kwamba, haiwezekani kwetu wanadamu kujua wateule wa Mungu ni akina nani kabla hawajaokolewa (fikiria Sauli wa Tarso). Spurgeon mara moja alijibu kwamba itakuwa vyema ikiwa wateule wangekuwa na alama E kubwa sana imechapishwa katika mgongo wao, lakini , bila shaka, hawana. Tunajua kwamba wateule wote wa Mungu hakika wataokolewa wakati mmoja katika safari yao duniani (soma Yohana 6:37, 39), lakini hilo linawezakosa kufanyika hadi siku watakapoitwa nyumbani kuwa na Bwana (kama vile, mwizi msalabani). Ni kupitia watu wenye “miguu iliyo mizuri” wanaoleta injili ambayo Mungu hutumia kama njia ya kuwafikia wateule wake (Isaya 52:7).

Katika nyanja zetu sisi sote tuna watu ambao hawajaokolewa, na tunastahili kuwaombea kwa sababu tunawajali sana na kwa sababu Mungu anawajali sana na hataki yeyote kati yao aangamie- haja Yake ni kuwa wote waje kwa Kwake kwa toba (2 Petro 3:9). Ni kawaida kuombea wale wanaotujali. Fikiria huruma ambayo kijakazi huyo alimwonyesha mtekaji nyara wake Mwaramu: “Kama bwana wangu angelimwona nabii aliyeko Samaria! Angemponya ukoma wake” (2 Wafalme 5:3). Tukiichukulia kuwa alimwombea Naamani, sala yake ilikuwa kwa niaba ya wale ambao hawajaokolewa. Fikiria huruma ambayo Paulo alihisi kwa ndugu zake Wayahudi waliopotea: “Nina huzuni kuu na uchungu usiokoma moyoni mwangu. Kwa maana ningetamani hata mimi nilaaniwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu hasa, wale walio wa kabila langu kwa jinsi ya mwili” (Warumi 9:2-3). Mtumishi mwingine mcha Mungu alikuwa -Musa, kama Paulo alikuwa tayari kuyatoa maisha yake kwa ajili ya watu wake (angalia Kutoka 32:32).

Yesu alituamuru tuwaombe wale ambao hawajaokolewa kwa namna hii: “mwombeni Bwana wa mavuno, ili apeleke watendakazi katika shamba lake la mavuno” (Luka 10:2). Ombi hili “mavuno shambani” mwa uinjilisti katika ulimwengu. Ni ombi kuwa watu wataokolewa na Mungu atatukuzwa.

Tuko na amri nyingine ya kibiblia ya kuwaombea wenye hawajaokolewa: “Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote… ambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu” (1 Timotheo 2:1, 3). Kanisa la Efeso (ambapo Timotheo alihudumu) lilikuwa limekoma kuombea wenye hawajaokoka, na Paulo alikuwa anawahimiza kuifanya kuwa kitu chao cha kwanza. Nia yake ilikuwa kwamba Wakristo wa Efeso wawe na huruma kwa waliopotea. Kwa mara nyingine tena, hatuna njia ya kujua wateule ni akina nani hadi waitikie. Na kama vile John MacArthur anavyoonyesha kwa usahihi, “Upeo wa juhudi za uinjilisti wa Mungu ni mpana kuliko uchaguzi” (Mathayo 23:14).

“Maombi ya mwenye haki yana nguvu tena yanafaa sana” (Yakobo 5:16). Na “macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza maombi yao” (1 Petro 3:12; rejelea Zaburi 34:15). Kwa kweli Mungu husikia kilio cha Wanawe. Tunajua kile huwapata wale ambao hufa katika dhambi zao, na ufahamu huo pekee unafaa kutusukuma kuomba bila kukoma kwa ajili ya wale ambao tunawajua na hawajaokolewa kwa imani kuwa wao pia, wataitikia wito wa Mungu na kuungana nasi mbinguni.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, kunayo msingi wowote wa kimaandiko wa kuombea ambao hawajaokoka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries