settings icon
share icon
Swali

Ni nini kuomba katika ndimi? Je! kuomba katika ndimi lugha ya maombi kati ya muumini na Mungu?

Jibu


Kama mwanzo wa historia, tafadhali soma makala yetu juu ya karama ya kunena kwa lugha. Kuna vifungu vinne msingi vya maandiko kwamba ni mfano kama ushahidi kwa ajili ya kuomba katika ndimi: Warumi 8:26, 1 Wakorintho 14:4-17; Waefeso 6:18; na Yuda mstari wa 20. Waefeso 6:18 na Yuda 20 kutaja "kuomba katika Roho." Hata hivyo, ndimi kama lugha ya maombi si tafsiri ya "kuomba katika Roho."

Warumi 8:26 inatufundisha, "Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kougua kusikoweza kutamkwa." Hoja mbili muhimu huifanya isiwezekane pakubwa kuwa Warumi 8:26 inamaanisha ndimi kama lugha ya maombi. Kwanza, Warumi 8:26 inasema kwamba ni Roho ambaye "hujonzi," si waumini. Pili, Warumi 8:26 inasema kwamba "jonzi" ya Roho "hawezi kudhditiwa." Kiini hasa cha kuzungumza katikaa lugha ni kutamka maneno.

Hiyo inatuacha na 1 Wakorintho 14:4-17 na mstari wa 14 hasa: "..maana, nikisali kwa lugha ngeni roho yangu ndiyo inayosali, lakini akili yangu hubaki bure" Wakorintho wa Kwanza 14:14 dhahiri inataja "kuomba kwa lugha." Je, hii inamaanisha nini? Kwanza, kchunguza mazingira ni mhimu sana. Wakorintho wa Kwanza sura ya 14 kimsingi ni kulinganisha / Tofauti ya zawadi ya kunena kwa lugha na karama ya unabii. Mistari 2-5 hufanya hivyo wazi kwamba Paulo ana maoni kwa unabii kuwa kama zawadi bora kuliko lugha. Wakati huo huo, Paulo anashangaa thamani ya lugha na anatangaza kwamba ana furaha kwamba yeye anena lugha zaidi kuliko mtu yeyote (mstari 18).

Matendo 2 inaeleza tukio la kwanza la karama ya lugha. Siku ya Pentekoste, mitume walizungumza kwa lugha. Matendo sura ya 2 inaweka wazi kwamba mitume walikuwa wakisema kwa lugha ya binadamu (Matendo 2:6-8). Neno lilotafsiriwa "lugha" katika zote Matendo sura ya 2 na 1 Wakorintho sura ya 14 ni glossa/ndimi ambalo lina maana ya "lugha." Ni neno kutokana kwalo ambalo sisi hupata neno la Kiingereza chetu sasa "glossary/ndimi." Kuzungumza katika lugha ilikuwa ni uwezo wa kuongea katika lugha ambayo msemaji hajui, ili kutangaza injili kwa mtu ambaye anazungumza lugha hiyo. Katika eneo la kitamaduni la Korintho, inaonekana kwamba Karama ya lugha ilikuwa hasa thamani na maarufu. Waumini Wakorintho walikuwa na uwezo bora wa kuwasiliana injili ya neno la Mungu kama matokeo ya karama ya lugha. Hata hivyo, Paulo aliiweka wazi kwamba hata katika matumizi ya hii lugha, ilikuwa ya kutafsiriwa au "imetafsiriwa" (1 Wakorintho 14:13, 27). Muumini Mkorintho atanena kwa lugha ngeni, kutangaza ukweli wa Mungu kwa mtu ambaye alizungumza lugha hiyo, na pia huyo muumini, au muumini mwingine katika kanisa, alikuwa atafsiri yale aliyosemwa ili mkutano wote uweza kuelewa kile ambacho alisema.

Basi, ni nini kuomba katika lugha, na ina tofauti gani kunena kwa lugha? Wakorintho wa kwanza 14:13-17 inaonyesha kwamba kuomba kwa lugha kunapasa pia kutafsiriwa. Matokeo yake, inaonekana kwamba kuomba katika lugha ilikuwa ya sadaka ya Sala kwa Mungu . Sala hii itahudumia mtu ambaye alizungumza lugha hiyo, lakini pia haja ya kutafsiriwa ili mwili mzima uweze kuwa umejengwa.

Tafsiri hii haikubaliani na wale ambao mtazamo wao dhidi ya kuomba katika lugha kama lugha ya maombi. Ufahamu huu mbadala unaweza kuwa muhtasari kama ifuatavyo: kuomba katika ndimi ni lugha ya maombi ya kibinafsi kati ya muumini na Mungu (1 Wakorintho 13:1) kwamba muumini anatumia kujisaidia mwenyewe (1 Wakorintho 14:4). Tafsiri hii ni ya kibiblia kwa sababu zifuatazo: 1) Ni jinsi gani kuomba kwa lugha kunaweza kuwa lugha ya maombi binafsi ikiwa inafaa kutafsiriwa (1 Wakorintho 14:13-17)? 2) Ni jinsi gani kuomba kwa lugha kunaweza kuwa kwa ajili ya kujijenga kibinafsi wakati maandiko inasema kwamba vipawa vya kiroho ni kwa uimarishaji wa kanisa, si binafsi (1 Wakorintho 12:7). 3) Ni jinsi gani kuomba kwa lugha kunaweza kuwa lugha ya maombi ya binafsi kama karama ya ndimi ni "ishara kwa wasioamini" (1 Wakorintho 14:22)? 4) Biblia inaeleza wazi kwamba si kila mtu ana karama ya lugha (1 Wakorintho 12:11, 28-30). Jinsi gani karama kuwa ni zawadi kwa ajili ya kujijenga kibinafsi kama si kila muumini anaweza kuimiliki? Je, sisi wote hatuitaji kujengwa?

Baadhi ya wengine wanaelewa kuwa kuomba katika lugha "ni ufunguo wa siri wa lugha" ambayo unamzuia Shetani na mapepo yake kutokana na kuelewa maombi yetu na hivyo kupata faida zaidi yetu. Tafsiri hii ni ya kibiblia kwa sababu zifuatazo: 1) Agano la Kale mara kwa mara inaeleza ndimi kama lugha ya kibinadamu. Kuna uwezekano kwamba Shetani na mapepo yake hawawezi kuelewa lugha za binadamu. 2) Biblia imenakili waumini kadhaa wakiomba katika lugha zao wenyewe, kwa sauti kubwa, na hakuna nafasi Shetani ataingililia maombi hayo. Hata kama Shetani / au mapepo yake wanasikia na kuelewa maombi tunayoomba, wao kabisa hawana uwezo wa kuzuia Mungu kujibu maombi kulingana na mapenzi yake. Tunajua kwamba Mungu anasikia maombi yetu, na ukweli huo unafanya lisiwe la manufaa kama Shetani na mapepo yake wanasikia na kuelewa maombi yetu.

Tuseme nini, basi, juu ya Wakristo wengi ambao wana uzoefu wa kuomba katika lugha na kupata kuwa ni wa kijijenga kibinafsi? Kwanza, ni lazima tuweke msingi imani yetu na utendaji wetu juu ya maandiko, si uzoefu. Sisi lazima tuangalia uzoefu wetu katika mwanga wa maandiko, si kutafsiri maandiko katika mwanga wa uzoefu wetu. Pili, wengi wa ibada za dini na dunia pia zanakili matukio ya kuongea katika lugha / kuomba kwa lugha. Ni wazi si Roho Mtakatifu unawakirimia watu hawa ambao si waamini. Kwa hiyo, inaonekana kwamba mapepo yana uwezo wa bandia wa kunena kwa lugha. Hii inatupasa kutufanya kulinganisha hata kwa makini zaidi uzoefu wetu kwa maandiko. Tatu, tafiti zimeonyesha jinsi kuzungumza / kuomba katika ndimi unaweza kuwa tabia ya kujifunza. Kwa kusikia na kuchunguza wengine kwa lugha ngeni, mtu anaweza kujifunza utaratibu, hata bila kujua. Haya ni maelezo yaliyo na uwezekano wa idadi kubwa ya matukio ya kuzungumza / kuomba katika lugha miongoni mwa Wakristo. Nne, hisia ya "kujijenga kibinafsi" ni ya asili. Mwili wa binadamu hutoa hisia wakati unagusa kitu kipya, kusisimua, hisia, na / au kukatolwa kutoka kwa mawazo ya busara.

Kuomba katika lugha ni dhahiri zaidi suala ambalo Wakristo wanaweza heshimu na kwa ihari kukubaliana au kutokubaliana. Kuomba katika lugha si kile ambacho huamua wokovu. Kuomba katika lugha si kitu kiinamtofautisha Mkristo kukomaa kutoka kwa Mkristo machanga. Kama kuna au hakuna jambo kama kuomba katika lugha kama lugha ya maombi ya kibinafsi si ya msingi wa imani ya Kikristo. Hivyo, wakati tunaamini tafsiri ya Biblia ya kuomba katika lugha inaongoza kutokana na wazo la lugha ya maombi ya binafsi kwa ajili ya kujijenga kibinafsi, sisi pia tunatambua kwamba wengi ambao ni wa mazoe kama hayo ni ndugu na dada zetu katika Kristo na wanastahili upendo na heshima.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni nini kuomba katika ndimi? Je! kuomba katika ndimi lugha ya maombi kati ya muumini na Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries