settings icon
share icon
Swali

Je ni nini maana ya kuomba bila kukoma?

Jibu


Amri ya Paulo katika 1 Wathesalonike 5:17 "kuomba bila kukoma," inaweza kuwa na utata. Ni wazi, haiwezi maanisha kuwa tunastahili kuinamisha kichwa, kufumba macho siku yote. Paulo hamaanishi kuzungumza mfurulizo, lakini badala yake nia ya fahamu ya uungu - na unyenyekevu wa uungu sisi huwa nao wakati wote. Kila uchao yafaa kuishi kwa ufahamu kwamba Mungu yu pamoja nasi na kwamba Yeye anashiriki kikamilifu katika mawazo na matendo yetu.

Wakati mawazo yetu hugeukia wasiwasi, hofu , kuvunjika moyo, na hasira, tinapaswa kwa uangalifu na haraka kurejesha kila wazo katika sala na kila maombi katika shukrani. Katika barua yake kwa Wafilipi, Paulo anatuamrisha tukome kuwa na shaka na badala yake, "Bal katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu" (Wafilipi 4:6 ). Alifundisha waumini wa Kolosai kujitoa wenyewe "Dumuni katika kuomba, mkikesha na kushukuru" (Wakolosai 4:2). Paulo aliwahimiza waumini wa Efeso kuona sala kama silaha ya kutumia katika kupambana na vita vya kiroho (Waefeso 6:18) . Tunapotembea katika siku, maombi lazima yawe jibu letu la kwanza kwa kila hali ya kutisha, kila wazo na wasiwasi, na kila kazi tusiyothamani ambayo Mungu antuamrisha. Ukosefu wa maombi utatufanya tujigemee wenyewe badala ya kutegemea neema ya Mungu. Sala isiyokoma kwa njia injia ingine ni kuendelea kutegemea daima ushirika na Baba.

Kwa Wakristo, maombi lazima yawe kama pumzi. Hauitaji kufikiria kupumua kwa sababu anga inazidisha nguvu kwa mapafu yako na hasa kukulazimisha kupumua. Hiyo ndio ni kwa nini ni vigumu zaidi kwa kushikilia pumzi yako zaidi kuliko kupumua. Vile vile, wakati sisi huzaliwa katika familia ya Mungu, sisi huingia katika anga ya kiroho ambapo uwepo wa Mungu na neema watushinikiza, au kutushawishi, katika maisha yetu. Maombi ni majibu ya kawaida kwa shinikizo kama hilo. Kama waumini, zote tumeingia katika anga ya Mungu na kupumua hewa ya sala.

Hata hivyo, waumini wengi hushikilia "pumzi ya kiroho" kwa muda mrefu, wakifikiri wakati mfupi na Mungu unatosha kuwaruhusu kuishi. Lakini uzuizi huo wao wa ulaji kiroho unasababishwa na tamaa mbaya. Ukweli ni kwamba kila muumini lazima aendelee daima kuwa mbele za Mungu, daima kupumua katika ukweli wake, ili tuwe wa watendaji kikamilifu.

Ni rahisi kwa Wakristo kujisikia salama kwa kudhani badala ya kutegemea neema ya Mungu. Waumini wengi mno huridhika na baraka za kimwili na kuwa na hamu kidogo kwa ajili ya zile za kiroho. Wakati mipango, mbinu, na fedha huzalisha matokeo ya kuvutia, kuna uepesi wa kufikiria kwamba mafanikio ya binadamu ndi baraka ya Mungu. Wakati hayo yanapotokea, hamu ya kumtamani Mungu na kuihitaji msaada wake itakosekana. Kuendelea kudumu katika maombi ni sehemu muhimu ya maisha ya Kikristo na yatokana na unyenyekevu na kumtegemea Mungu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kuomba bila kukoma ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries