settings icon
share icon
Swali

Watu walikuwa wanaokolewa namna gani kabla Yesu afe kwa ajili ya dhambi zetu?

Jibu


Tangu kuanguka kwa mwanadamu, mzingi wa wokovu umekua juu ya kifo cha Kristo, pengine kabla ya msalaba au tangu msalaba, hatunguweza kuokolewa kama si tukuo hilo la ubadilisho kataka historia ya ulimwengu. Kifo cha Yesu kililipa deni ya dhambi ya watakatifu wa Agano la Kale na zile dhambi zijao za Agano Jipya.

Vinavyohitajika katika wokovu katika vizazi vyote imekuwa imani. Mungu amekuwa sehemu ya wokovu wa mtu kila wakati. Mwandishi wa Zaburi aliandika, ”Heri wote wanaomkimbilia” (Zaburi 2:12). Mwanzo 15:6 yatuambua kwamba Abrahamu alimwamini Mungu, hiyo ilitosha Mungu akamhesabia jambo hili kuwa haki (pia angalia Warumi 4:3-8). Njia za dhabihu katika Agano la Kale haikutoa dhambi, vile Waebrania 10:1-10 vile yafunza, ingawa haikulenga siku ambayo Mwana wa Mungu atamwaga damu kwa sababu ya kizazi kiovu cha mwanadamu.

Chenye kimebadilika katika miaka ni ujumbe wa imani ya muumini. Anachokihitaji Mungu chenye kinastahili kuaminiwa kimewekwa juu ya misingi ya ufunuo. Adamu aliamini ahadi Mungu aliyoitoa katika Mwanzo 3:15 ya kwamba uzao wa mwanamke utamshinda Nyoka. Adamu alimwamini kupitia jina alilompa Hawa (aya 20) na Bwana akaonyesha kubali yake kwa kuifunika mili yao kwa ngozi (aya ya 21). Wakati huo hayo ndio Adamu alikua anajua lakini aliyaamini.

Abrahmau alimwamini Mungu kuwa katika ahadi zake na ufunuo mpya ambao Mungu alimpa katika Mwanzo 12 na 15. Kabla ya Musa, hakuna Bibilia aliandikwa, lakini mwanadamu aliwajibika kwa yale Mungu alikuwa amefunua. Katika Agano la Kale lote, waumini waliokoka ni kwa sababu walimwamini Mungu kuwa siku moja atawaondolea shida ya dhambi. Leo hii, tunaangalia nyuma, na kuamini kwamba tayari amekwisha shughulikia dhambi zetu msalabani (Yohana 3:16; Waebrania 9;28).

Je! Kulikuwaje kwa waumini wakati wa Kristo kabla ya msalaba na kufufuliwa kwake? Waliamini nini? Je waliielewa picha kamili ya Yesu kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zao? Baadaye katika historia “Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka. Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, hasha, Bwana, hayo hayatakupata” (Mathayo 16:21-22). Je wanafunzi wake walijibu namna gani kuhusu ujumbe huu? “Petero akamchukua kando, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana hayo hayatakupata.” Petero na wanafunzi wengine hawakuujua ukweli kamili, na bado waliokolewa kwa sababu waliamini kwamba Mungu atashughulikia hali ya dhambi. Hawakujua kabisa jinsi Mungu angefanya hivyo zaidi kuliko Adamu, Abrahamu, Musa au Daudi vile hawakujua ni namna gani Mungu angefanya hivyo, lakini walimwamini Mungu.

Leo hii tuko na ufunuo mwingi kuliko watu walioishi kabla ya kufufuka kwa Yesu; twaijua picha kamili. “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu” (Waebrania 1:1-2). Wokovu wetu bado upo katika misingi ya kifo cha Yesu, imani yetu bado ingali inaitajika kwa wokovu wetu, na chombo cha imani yetu ni Mungu. Leo hii, kwetu sisi ujumbe wa imani yetu ni kwamba, Yesu Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Alizikwa, na akafufuka siku ya tatu (1Wakorintho 15:3-4).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Watu walikuwa wanaokolewa namna gani kabla Yesu afe kwa ajili ya dhambi zetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries