Swali
Kumuishia Mungu—ni kwa nini ni vigumu kumuishia Mungu?
Jibu
Yesu alizungumza na wale ambao wangemfuata kuhusu kubeba msalaba, kuhesabu gharama, na kuacha kila kitu (Luka 14:25-33). “njia ni finyu ielekeayo kwenye uzima” alisema (Mathayo 7:14). Maandiko yanataja watu wengi wa Mungu ambao wametembea katika njia hiyo ngumu-Danieli, Eliya, Yusufu, na Yohana Mbatizaji ni baadhi ya wengi.
Warumi 7 inaonyesha kwamba kumuishia Mungu sio rahisi kwetu sisi wote. Mtume Paulo aliandika juu ya kuteseka kwake mwenyewe “Lakini ninaona kuna sheria nyingine inayotenda kazi katika viungo vya mwili wangu inayopigana vita dhidi ya ile sheria ya akili yangu. Sheria hii inanifanya mateka wa ile sheria ya dhambi inayofanya kazi katika viungo vya mwili wangu” (aya ya 22-23).
Kabla hatujamjua Kristo, hatukuweza kutenda lolote ila dhambi. Hatukuwa na uamuzi katika suala hilo. Msukumo wetu ulikuwa wa kujifurahisha. Hata matendo mema tuliyoyafanya yalikuwa na nia ya ubinafsi: tulifanya mambo mema ili kibinafsi tuhisi vyema, tutulize hatia, au kuboresha sifa yetu kwa wengine. Katika wokovu, Roho Mtakatifu huingia ndani ya roho zetu. Anavunja nguvu ya dhambi iliyokandamiza maisha yetu na kutuweka huru kumtii Mungu. Sasa hivi tumetiwa nguvu na upendo badala ya hatia.
Lakini bado tunakabiliana na majaribu kutoka nje na kutoka ndani (2 Wakorintho 7:5). Biblia inaita asili yetu ya zamani ya dhambi “mwili” na inaonya kwamba wale walio “katika mwili” hawawezi kumpendeza Mungu (Warumi8:8). Hata Wakristo wanaweza kuwa wa “kimwili.” Hata ingawa Roho Mtakatifu anadumu ndani ya moyo wa kila muumin (1 Wakorintho 3:16; 6:19), ni wajibu wa kila mtu kuamua kiwango watamuruhusu kuwatawala. Tumeamrishwa “enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili” (Wagalatia 5:16,25). Ni katika kujiona sisi wenyewe “kusulibiwa na Kristo” (Wagalatia 2:19-20) kwamba tunaweza kutembea katika Roho.
Yesu hakukuja kugeuza mwili wetu, bali alikuja kuusulibisha (Warumi 6:6-7). Lakini mwili hautaki ufe. Haja kubwa sana ya kutaka kujifurahisha wenyewe na kuwa na maafikiano na ulimwengu haufi kifo rahisi. Wakati tunashikilia haki zetu, maoni yetu, na ajenda yetu, tunabaki kuwa watawala wa maisha yetu wenyewe. Wakati tunayatoa mapenzi yetu katika madhabau ya Mungu na kuyaachilia, tunakufia nafsi zetu. Kisha tunaweza ”kujazwa kwa Roho Mtakatifu,” tukiongozwa naye kabisa (Matendo 4:8; 13:52; Waefeso 5:18). Ni kupitia kwa nguvu za Roho Mtakatifu ambapo tunaweza kuishi maisha yanayomheshimu Mungu. Ni nguvu ya Roho pekee ndiyo inayoweza kuzalisha matendo mema ndani yetu bila kuhalalisha sheria na kiburi.
Hamu ya kutaka kukubalika na ulimwengu ndio chanzo kuu cha kuafikiana na ulimwengu. Hatutaki kuteseka kwa dhihaka au kukumbana na mateso ya aina yoyote. Inapendeza zaidi kujipima na wale walio karibu nasi kuliko kujipima na Neno la Mungu (2 Wakorintho 10:12). Lakini andiko la Yakobo 4:4 linasema, “Kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa rafiki wa dunia hufanyika adui wa Mungu.”
Tunapokumbatia wazo potofu kwamba wokovu utayafanya maisha yetu kuwa rahisi, tunapatwa na mshtuko. Wale ambao wamekuja kwa Kristo kwa ajili ya kupata “mema” ambayo yeye huyatoa mara nyingi hukengeuka wanapotambua kwamba kumkubali kunamaanisha kuwa wana mtawala mpya. Yesu alipokuwa duniani, umati wa watu ulipenda chakula cha bure na miujiza, lakini alipoanza kuzungumza juu ya mambo magumu ya injili, “Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata” (Yohana 6:66).
Hatuwezi mtumikia Mungu na vile vile nafsi yetu wenyewe (ona Luka 16:13). Kumuishia Mungu kunamaanisha kwamba tunafanya uamuzi wa mwisho kuhusu ni nani anayeongoza. Wakati mwili wetu unaanza kudai haki zake, tunazirudisha msalabani na kuziruhusu kufa. Wakati dhambi inaleta majaribu, uamuzi umekwisha fanywa: tunatafuta mapenzi ya Mungu tunapuuwa na mapenzi yetu. Wagalatia 1:10 inauliza, ”Je, sasa mimi ninatafuta kukubaliwa na wanadamu au kukubaliwa na Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Jibu liko wazi: ”Kama ningekuwa bado najaribu kuwapendeza wanadamu, nisingekuwa mtumishi wa Kristo.”
Kumuishia Mungu kunaweza kuwa kugumu, lakini sio kuwa hauna furaha. Paulo aliandika barua zake za furaha zaidi alipokuwa akiteswa huko Rumi (ona kitabu cha Wafilipi). Bado tutakumbana na majaribu na magumu, lakini utukufu wa Mungu unapokuwa lengo letu, kuishi kwa ajili yake kunakuwa chanzo cha furaha yetu badala ya kuwa jambo la kuchosha (Zaburi 100:2; 1 Wakorintho 6:20; 1 Petro 4:16).
English
Kumuishia Mungu—ni kwa nini ni vigumu kumuishia Mungu?