settings icon
share icon
Swali

Je, ni njia zipi za kivitendo za kumtegemea Mungu pekee?

Jibu


Kumtegemea Mungu ni nguzo katika maisha ya Kikristo. Tunamtumainia, au kumtegemea Mungu kwa wokovu wetu (Waefeso 2:8-9). Tunamtegemea Mungu kwa hekima (Yakobo 1:5). Kwa kweli tunamtegemea Mungu kwa kila jambo (Zaburi 104:27) na katika kila kitu (Mithali 3:5-6). Mtunga zaburi anafundisha vile Mungu ni wa kutegemeka kwa maelezo yenye sehemu tatu “Bwana ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba, ambaye kwake ninakimbilia. Yeye ni ngao yangu na pembe ya wokovu wangu, ngome yangu” (Zaburi 18:2).

Kumtegemea Mungu pekee haimaanishi kwamba tufuatilie kiupumbavu. Yesu hakuhitaji kuruka kutoka kilele cha hekalu ili “kuthibitisha” kwamba alimtegema Mungu (Mathayo 4:5-7). Kuna tofauti kati ya kumwamini Mungu na kumjaribu Mungu. Kumtegemea Mungu pekee haimaanishi kuwa tunaachana na karama za Mungu. Kwa mfano, mtu aliye na uchungu/mchirizi wa koo anaweza kukataa kwenda kwa daktari, akisema “nitamtegemea Mungu pekee aniponye.” Au mtu anayeendesha gari anaweza kufunga macho yake na kuachilia usukani na kusema “nitamtegemea Mungu pekee anipeleke nyumbani.” Matendo haya yatakuwa ya upumbavu. Mungu ametupatia madaktari na madawa kutusaidia kupona. Ametupa akili ya kuendesha gari, tukijua kwamba uponyaji wote hatimaye hutoka kwa Mungu; na bado tunaweza kumtegemea Mungu tunapoendesha gari, tukijua kwamba usalama wote hatimaye hutoka kwa Mungu.

Tunamtegemea Mungu nyakati zote, na kuna nyakati hatuwezi kufanya lolote lingine. Mungu anatupa imani tunayohitaji ya kustahimili nyakati hizo. Shadraka, Meshaki, na Abednego hawakuweza kubadilisha mapenzi ya mfalme, na hawakuweza kupunguza ukali wa tanuru lile la moto. Walichojua ni kwamba hawawezi kumsujudia mungu wa uongo. Walitupwa motoni wakitegemea Mungu pekee kwa matokeo (Danieli 3).

Hapa kuna baadhi ya njia za vitendo za kumtegemea Mungu pekee:

1) Maombi. Maombi ni miongoni mwa mambo mengine, kukiri uwezo wa Mungu, ahadi, na utele Wake. Unapoomba, unaonyesha kuwa unamtegemea Mungu. Amri ya kibiblia ni “haja zenu na zijulikane na Mungu” (Wafilipi 4:6).

2) Heshimu Biblia. Neno la Mungu lina habari, maagizo, mifano, na ahadi kwa waumini wa Agano Jipya. Isome Biblia kila siku. Chunguza kila kitu dhidi ya ukweli wa Neno la Mungu (Matendo 17:11). Na kunapokuwa na mgongano kati ya kile ambacho Biblia inasema na kile mtu yeyote anasema, fuata Biblia inavyosema. “Nitasikiliza lile atakalosema Mungu aliye Bwana” (Zaburi 85:8).

3) Fanya haki. Nyakati zote, katika hali zote, fanya kile ambacho unajua ni sawa na mwachie Mungu matokeo. Yekebedi alifanya haki kwa kumwokoa mtoto wake, Musa (Kutoka 2:1-10). Danieli alifanya haki kwa kuasi mfalame na kumwomba Bwana (Danieli 6). Daudi alifanya haki kwa kumzuia Goliathi (1 Samweli 17). Katika kila kisa, kumtegemea kwao kwa Mungu pekee kulithawabishwa.

4) Kuwa dhabihu iliyo hai. Warumi 12 inasema itoeni miili yenu iwe ”dhabihu iliyo hai” kwa Mungu. Dhabihu zinazokubalika hutakaswa kutoka kwa dhambi na kuwekwa wakfu kwa Mungu. Unapokuwa dhabihu iliyo hai, unaishi kwa ajili ya Bwana. Unaacha kupigania haki zako mwenyewe na kuacha kutegemea nguvu zako mwenyewe. Unapojifunza kuwa dhabihu iliyo hai kwa ajili ya Mungu, utagundua ukweli kwamba, “ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu” (2 Wakorintho 12:10).

5) Kaa ndani ya Kristo. Maisha ya kikristo si mkutano wa kila mara na Mungu. Ni kumfanya Mungu kuwa makao yako, kuishi Naye. Yesu anasema hivi: “Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa matunda lisipokaa ndani ya mzabibu, vivyo hivyo ninyi msipokaa ndani yangu hamwezi kuzaa matunda” (Yohana 15:4). mtegemee Kristo kama tawi lenye matunda linavyotegemea mzabibu. Tawi lililoshikamana na mzabibu linatimiza kusudi lake.

6) Kataa fadhaa. Mungu anawajali watoto wake, hata zaidi zaidi ya majani ambayo Yeye huvika maua na ndege ambao huwalisha kila siku. Naam, uko na mahitaji, lakini “Baba yenu wa mbinguni anajua” (Matahayo 6:32). Jifunze “Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu” (1 Petro 5:7). Kuweka ndani yako baadhi ya fadhaa ni kutilia shaka utunzaji wa Mungu.

Siku moja wanafunzi walimuuliza Yesu ni nani aliyekuwa mkuu katika ufalme wa mbinguni. Yesu aliwajibu kwa mfano: “Yesu akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. Naye akasema: “Amin, nawaambia, msipookoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. Kwa hivyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni (Mathayo 18:2-4). Sifa moja ya watoto ni kwamba wanategemea wengine kwa ajili ya ustawi wao. Watoto wa Mungu wanapaswa kushiriki ubora huo wa kumtegemea Baba yao wa Mbinguni mwenye upendo kwa kila kitu wanachohitaji.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni njia zipi za kivitendo za kumtegemea Mungu pekee?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries