Swali
Je, inamaanisha nini kumweka Mungu kuwa wa kwanza?
Jibu
Ni kawaida kusikia Mkristo akisema, ”Ninamweka Mungu kuwa wa kwanza” au kuwashauri wengine “hakikisha kwamba Mungu amechukua nafasi ya kwanza katika maisha yako.” Misemo kama hiyo hutumiwa mara nyingi sana na kusababisha hatari ya kuwa msemo wa Kikristo. Lakini hakuna kitu kigeni kuhusu wazo la kumtanguliza Mungu kwanza: kwa kweli, ni la kibiblia kabisa.
Kila mtu ana vapaumbele. Tunapanga ratiba yetu, makadirio, na mahusiano kulingana na umuhimu unaotizamiwa. Kumtanguliza Mungu kunamaanisha kwamba tunampa Yeye nafasi ya kwanza zaidi ya kila kitu kingine. Yeye ndiye mkuu katika maisha yetu na kiungu kikuu cha kila kitu tunachofanya au kufikiria. Wakati tunachagua kumweka Mungu wa kwanza, tunaamua kwamba Yeye ni wa maana zaidi kuliko mtu mwingine yeyote, Neno Lake ni la thamani zaidi kuliko ujumbe wowote, na mapenzi Yake ni mazito kuliko jambo lolote la lazima.
Kumtanguliza Mungu kunamaanisha kwamba tunashika amri kuu zaidi: “Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote” (Mathayo 22:37). Kwa njia nyingine, tumewekeza kikamilifu katika uhusiano wetu na Mungu. Kila kitu tulicho nacho na kila kitu chochote kile tulicho kimewekwa wakfu Kwake. Hatumiliki chochote.
Kumtanguliza Mungu kunamaanisha kwamba tunatunza maisha yetu kutokana na ibada ya sanamu ya namna yoyote: “Watoto wapendwa, jilindeni nafsi zenu kutokana na sanamu” (1 Yohana 5:21). Sanamu ni kitu chochote kinachochukua nafasi ya Mungu mmoja, wa kweli ndani ya mioyo yetu. Kama vile Gideoni alibomoa madhabahu ya Baali na kukata nguzo ya Ashera (Waamuzi 6:25-27), lazima tutoe kutoka mioyoni mwetu chochote kinachopunguza kujitolea kwetu au kumcha Mungu kwetu. Gideoni alipomjengea Bwana madhabahu badala ya sanamu ile kuondoa zile sanamu za kuchongwa, ni lazima tujitoe wenyewe kama “dhabihu iliyo hai” kwa Mungu na kwa njia hiyo kumweka Yeye kuwa wa kwanza (Warumi 12:1).
Kumtanguliza Mungu kunamaanisha kwamba tujitahidi kufuata nyayo za Yesu (1 Petro 2:21). Maisha ya Yesu yalikuwa na sifa ya kujitiisha kabisa kwa mapenzi ya Baba, huduma kwa wengine, na sala. Katika bustani, akikabiliwa na uchungu usiowazika, Yesu aliomba, “Lakini si kama nipendavyo, bali mapenzi yako yatendeke” (Luka 22:42). Hiyo ni kumweka Mungu wa kwanza. Maneno, matendo na mafundisho ya Yesu yote yalitoka kwa Baba (Yohana 5:19; 7:16; 12:49). Yesu alimtukuza Baba katika kila jambo la maisha yake na alitimiza yote ambayo alitumwa kufanya (Yohana 17:4).
Yesu alitufundisha “utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake” (Mathayo 6: 33). Yaani, tunapaswa kutafuta mambo ya Mungu juu ya mambo ya dunia. Tunapaswa kutafuta wokovu ambao ni wa asili katika ufalme wa Mungu, tukizingatia thamani ile kuu kuliko utajiri wowote wa ulimwengu ukiwekwa pamoja (ona Mathayo 13:44-46). Ahadi inayohusiana na amri ni kwamba, ikiwa tunamweka Mungu kwanza, “atakupa kila kitu unachohitaji.”
Wakati wa janga la njaa, nabii Eliya alitembelea mji fulani ambako alikutana na mjane aliyekuwa akitayarisha chakula cha mwisho chake na mwanawe. Eliya alimwomba mkate na maji, na mjane huyo akaeleza kwamba alikuwa na chakula cha mlo mmoja tu, baada ya chakula hicho kuisha wangekabilina na njaa. Eliya akaendelea na kusema: “Usiogope... Lakini kwanza unitengenezee mimi mkate mdogo kutoka vile ulivyo navyo kisha uniletee na ndipo utayarishe chochote kwa ajili yako na mwanao” (1 Wafalme 17:13). Kwa kweli, Eliya alimwambia amtangulize Mungu. Kwa imani, mjane yule alitii. Alimtanguliza Mungu na kumlisha nabii. Na kisha muujiza ulikuja: “Kwa hiyo kukawa na chakula kila siku kwa ajili ya Eliya, yule mwanamke na jamaa yake. Kwa kuwa lile gudulia la unga halikwisha na ile chupa ya mafuta haikukauka” (mistari ya 15-16).
Wale wanaomtanguliza Mungu kwanza watakuwa tofauti na ulimwengu. Watatii amri za Mungu (Yohana 14:15), watachukua msalaba wao na kumfuata Yesu (Luka 9:23), na hawatauacha upendo wao wa kwanza (Ufunuo 2:4). Wanampa Mungu malimbuko, na si mabaki. Maisha ya Kikristo yana sifa ya utumishi wa muda kwa muda hadi wakati usio na ubinafsi kwa Mungu unaobubujika kutoka kwa upendo Kwake na kwa watu wake. Katika mambo yote, muumini humwamini, hutii na kumpenda Mungu zaidi ya yote. Kumweka Mungu kwanza huwa tarahisi tunapoyachukulia kwa uzito maneno ya Warumi 11:36: “Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele! Amina.”
English
Je, inamaanisha nini kumweka Mungu kuwa wa kwanza?