settings icon
share icon
Swali

Je, inamaanisha nini kumpenda yesu?

Jibu


Iili tuelewe maana ya kumpenda Yesu, ni lazima kwanza tufafanue ni nini maana ya neno upendo. Kwa kuwa tunazungumzia kuhusu Yesu, ufafanusi wetu utaangazia tu maneneo mawili ya Kigiriki ambayo yametumika kwa niapa ya “upendo” katika Agano Jipya. La kwanza ni philia. Hii inarejelea upendo wa kindugu au ushirika wa karibu na mtu mwingine. Ili kuonyesha aina hii ya upendo hautahitaji dhabihu yoyote kubwa kwa upande wa anayependa. Upendo huu unaonyeshwa kupitia nia ya ukarimu na wakati wa kushinda nao. Mtu yeyote tunayefamiana kwa karibu anaweza kupendwa na upendo wa philia. Aina hii ya upendo unaweza kuisha kwa urahisi sana, hata hivyo, huu sio aina ya upendo ambao ungetoshana na aina ya upendo ambao Yesu anaohitaji kutoka kwa wafuasi Wake.

Neno lingine la Kigiriki la “upendo” ni agape. Huu ni upendo ambao unachukuliwa kuwa usio wa masharti. Huu ndio upendo Paulo anaelezea katika 1 Wakorintho 13 na ndio unaofaa katika kuelewa ni nini maana ya kumpenda Yesu. Paulo anaelezea aina ya upendo huu kwa kile unafanya na kile ambacho haufanyi. Kulingana na 1 Wakorintho 13:4-8, agape huvumilia, hufadhili, hufurahia katika kweli, huvumilia mambo yote, unaamini mambo yote, hutumaini mambo yote na hustahimili katika mambo yote. Kinyume chake, agape hauna wivu, haujisifu, wala haufurahi makosa; hauna kiburi, sio jeuri, hauna ubinafsi, hasira, au kinyongo. La muhimu zaidi agape hauna mwisho. Hautafifia kama vile philia. Agape hautegemei hali na hauna mwisho.

Kumpenda Bwana ni kumfuata Yeye popete atakapotuongoza, kumtii kwa chochote anachouliza, na kumwamini Yeye hata majaribu yawe namna gani. Kumpenda Yesu ni kuakisi upendo ambao Mungu alio nao kwetu kwa kuwa “Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu” (1 Yohana 4:10). Kumpenda Bwana ni kuwajali wale anaowapenda (1 Yohana 4:19; ona pia Yohana 21:16).

Agape hautegemei hisia bali mapenzi. Kila sifa ya agape ni chaguo la makusudi la kutenda kwa namna fulani. Hivyo, Yesu alisema, “Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu” (Yohana 14:15), alikuwa anafundisha kwamba kumpenda Yeye itakuwa ni tendo dhahiri, na sio mhemuko wa hisia. Ikiwa Yesu anapendwa vile aliamrisha, basi chaguo la uangalifu lazima lifanywe ili kutenda kulingana na kielelezo kilichoelezwa katika 1 Wakorintho 13. yesu alikuwa wazi kwamba kumpenda Yeye ni huduma (Yohana 14:15, 21, 23, 28). Kwa hivyo, kumpenda Yeus ni kutenda kwa hiari njia ambayo kujitolea kwetu kwake kumethibitishwa kupitia matendo yetu kwake na utiivu wetu kwake.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inamaanisha nini kumpenda yesu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries