settings icon
share icon
Swali

Yamaaninisha nini kumkufuru Roho Mtakatifu?

Jibu


Wazo la “kumkufuru Roho” limetajwa katika Mariko 3:22-30 na katika Mathayo 12:22-32. neno kufuru linaweza kuelezwa kwa ujumla kama, “tabia iliyo kando”. Hilo neno laweza kutumika kwa dhambi kama zile za kumlaani Mungu au kwa makusudi ya kutotambua mambo yanohusiana na Mungu. Pia ni kumhuzisha Mungu na dhambi, ama kukana yale mazuri tunayostahili kumhusisha nayo. Hii hatia ya kukufuru ingawa ni pekee inaitwa “kukufuru Roho Mtakatifu” katika Mathayo 12:31. katika Mathayo 12:1-32, Wafarisayo baada ya kushuhudia matendo makuu yasiyopingika ya Yesu alikuwa akitenda miujiza kwa nguvu za Roho Mtakatifu, na wakadai kuwa alikuwa amepagagwa na pepo “Beelzebuli” (Mathayo 12:24) unaweza gundua kwamba katika Mariko 3:30 Yesu analengo kuhusu kwa kile ambacho hawakukifanya “kumkufuru Roho Mtakatifu.

Huku kukufuru na kuhusu na mtu kumtusi Yesu Kristo kuwa amepagagwa na mapepo badala ya kujazwa na Roho Mtakatifu. Kwa sababu hiyo kwa matukio haya ya kukufuru Roho Mtakatifu hauwezi kuongezeka hii leo. Yesu Kristo hayumo duniani leo hii, bali ameketi katika mkono wa kulia wa Mungu. Hamna mtu atakaye shuhudia Yesu Kristo akitenda miujiza na kudai kwamba nguvu hizo ni za Shetani badala ya Roho Mtakatifu. Mfano wa karibu sana leo hii utakuwa ule wa mtu akikombolewa na kubadilisha maisha yake kwa nguvu za Shetani na badala ya kujazwa na Roho Mtakatifu. Kukufuru Roho Mtakatifu leo hii, ambayo ni sawa na dhambi isiyo samehewa ni hali ya kuendelea kutokua na imani. Hakuna msamaha kwa mtu yule akufaye bila imani. Kuendelea kukataa Roho Mtakatifu ambao watusukuma kuwa na imani katika Yeus Kristo ni kufuru isiyosamehewa. Kumbuka chenye kimesemwa katika Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” mbele yake kuna aya ingine, “Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia” (Yohana 3:36). Hali pekee ambayo mtu hawezi kuwa na msamaha ni ikiwa ako kati ya wale, “yeyote atakaye mwamini” kwa maana ni yule amemkataa Mwana.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Yamaaninisha nini kumkufuru Roho Mtakatifu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries