Swali
Je, kuna uwezekano kuishi maisha yako na kufanya mambo ambayo yanamtukuza Mungu?
Jibu
Kila Mkristo anataka kumheshimu Mungu. Je, haingekuwa vizuri ikiwa kila kitu tulichofanya, bila ubaguzi, kilileta heshima kwake? Lakini je, Mkristo anaweza kufikia hatua ya kutokuwa na dhambi? Je ni jambo la akili kutazamia kwamba baada ya muda tunaweza kukua kiroho hivi kwamba hatujikwai kamwe? Kunaweza kuwa na majibu mawili kwa swali hili.
Kwanza kabisa, kuishi katika utakatifu kunapaswa kuwa lengo la kila mtoto wa Mungu. Mungu anatuamuru “Kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1 Petro 1:16). Na anatupa uwezo wa kufanya hivyo. Waraka wa pili wa Petro 1:3 inasema, “Uweza wake wa uungu umetupatia mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa Mungu, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe.” Petro anaendelea katika aya za 5-7 kuorodhesha hatua za ukuaji wa kiroho ambazo zinajengana: imani, wema, maarifa, kiasi, subira, utauwa, upendo wa kindugu, upendo. Na anatamatisha na ahadi ya kushangaza: “Kwa maana mkifanya hivyo, hamtajikwaa kamwe” (aya ya 10). Hivyo, je, hii inamaanisha kuwa ukamilifu unawezekana?
Kulingana na kifungu hiki hivyo ndivyo ilivyo. Dhambi za makusudi zinaweza kushindwa kwa kuendelea kujitiisha kwa mapenziya Mungu. Hata hivyo, petro hamaanishi kuwa muumini ataendelea kuishi katika ushindi kamilifu. Kwa ufupi anasema kwamba ikiwa tuko na sifa hizi kwa utele, hatuwezi anguka kwa mitego ya dhambi. Ni wangipi miongoni mwetu wanaweza sema kwa kweli kuwa kila mara tunaonyesha upendo jinsi Mungu anavyoonyesha? Je, tuko na ufahamu wote kwa kila hali? Huwa tuna lengo ambalo ni kufanana na Yesu (Warumi 8:29; 1 Yohana 4:17). Likini pia tuna adui wawili ambao hupigana vita dhidi ya lengo hilo: Shetani na mwili wetu wa dhambi (Warumi 7:18-23; 1 Petro 5:8). Wakati maisha yetu yamezalishwa na Roho Mtakatifu, tunaweza kutarajia maisha yaliyo zaidi ya dhambi za hiari, kama vile usherati, wizi na uongo. Hizo ni dhambi tunachagua tukijua, na Mungu anatutarajia tuzishinde kwa uweza na nguvu Zake (Warumi 8:37). Kwa hivyo, kwa hali kama hiyo, tunaweza kuamua kutenda vile vitu ambavyo vinamweshimu Mungu.
Kwa upande mwingine, tunaishi katika upungufu wa miili yetu. Tuko chini ya tamaa na nia kama vile kujiurumia, hasira na woga. Wazo moja la tamaa huharibu ukamilifu na hivyo kufutilia mbali pendekezo lolote kuwa tunaweza kuishi maisha yasiyo ya dhambi. Hiyo ndio sababu tumeamurishwa “tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo” (2 Wakorintho 10:5). Mara nyingi vita kuu dhidi ya mwili vinapiganwa na ndani, na havitambuliki na mtu yeyote. Dhambi zingine tunazijua kwa kuzitazama tu. Je, ni mara ngapi tumesema jambo na baadaye kugundua, “Sikupaswa kusema hivyo”?
Kwa hiyo, ijapokuwa inaweza wezekana kufikia hatua ya kujizuia kwa mwongozo wa Roho unaosababisha kufanya mambo yale tu ambayo yanamheshimu Mungu, “Moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi. Ni nani awezaye kuujua?” (Yeremia 17:9). Mara nyingi hatuelewi misukumo yetu wenyewe au kuona makosa yetu hadi Mungu ayataje. Hiyo ndio maana Mungu anatuhimiza tukiri dhambi zetu na mioyo yetu kutakazwa, na tusidhani kuwa hatuna dhambi. Waraka wa Kwanza wa Yohana 1:8-9 unaiweka wazi, “Kama tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe wala kweli haimo ndani yetu. Kama tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutoka kwenye udhalimu wote.”
Mkristo mwenye hekima hafikirii kuwa amefikia ukamilifu usio na dhambi. Kufanya hivyo ni kiburi, na hiyo ni dhambi (Yakobo 4:6; Mithali 16:5). Tunapaswa kujichunguza wenyewe daima ili kuona kama njia zetu sinampendeza Bwana. Tunaweza kuomba pamoja na Daudi, “Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu. Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele” (Zaburi 139:23-24). Tunaweza pia kuomba, “Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu” (Zaburi 19:14). Ni lazima pia tujichunge dhidi ya kufuata sheria, ambayo inatufanya kuhisi kwamba ni lazima tuwe wakamilifu ili Mungu atukubali.
Warumi 7 imenakili pambano lisilo la huruma la mtume Paulo na mwili wake mwenyewe na ni la kutia moyo kwa kila mmoja wetu. Hatimaye, tunaweza kusema sisi sote, “Ashukuriwe Mungu kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu!” (aya ya 25). Zaburi 103: 13-14 hutufariji tunapotambua kutoweza kwetu kuwa wote tuliumbwa kuwa: “Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha; kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.” Tunapokumbuka kwamba Yesu pekee ndiye haki yetu mbele za Mungu (2 Wakorintho 5:21), tuko huru kumtumikia Mungu kwa furaha kutoka kwa moyo wa upendo badala ya moyo wa woga.
English
Je, kuna uwezekano kuishi maisha yako na kufanya mambo ambayo yanamtukuza Mungu?