settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nini maana ya kumcha Mungu?

Jibu


Kwa kafiri, kumcha Mungu ni hofu ya hukumu ya Mungu na mauti ya milele, ambayo ni kujitenga na Mungu milele (Luka 12:5, Waebrania 10:31). Kwa muumini, kumcha Mungu ni kitu tofauti sana. hofu ya muumini ni heshima ya Mungu. Waebrania 12:28-29 ndio ufafanuzi mzuri wa kifungu hiki: “Kwa hivyo, tangu sisi tupokea ufalme usioweza kutikiswa, hebu shukuruni, na hivyo mwabudu Mungu kwa njia inayokubalika kwa heshima na hofu, kwa ajili Mungu weti ni moto mkali unaoteketeza.” Heshima hii na kumcha Mungu ndio maana sahii kwa Wakristo. Hii ni sababu motisha kwa ajili yetu kujisalimisha kwa Muumba wa Ulimwengu.

Mithali 1:07 inasema, “Kumcha Bwana ndio mwanzo wa maarifa. Hadi sisi tuelewa kuwa Mungu ni nani na kuendeleza hofu yetu na heshima kwake, hatuwezi kuwa na hekima ya kweli. Hekima ya kweli hutoka tu kwa kuelewa Mungu ni nani na kwamba yeye ni mtakatifu, na mwenye haki. Kumbukumbu la Torati 10:12, 20-21 yasema, “Na sasa, Ee Israeli, je, Bwana, Mungu wako anachohitaji kutoka kwenu ni kumcha Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake zote, na kupenda, kumtumikia Bwana, Mungu wenu kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. Mche Bwana, Mungu wako na kumtumikia yeye. Ambatana naye, na kuapa kwa jina lake. Yeye ni sifa yako, yeye ni Mungu wenu, ambaye alifanya maajabu makubwa na ya kutisha kwa ajili yenu, amboyo uliyaona kwa macho yako mwenyewe.” Kumcha Mungu ndio msingi wa mwendo wetu katika njia zake, kumtumikia, naam na, kumpenda.

Baadhi ya wengine hutafsiri upya kumcha Mungu kwa waumini “heshima” kwake. Wakati heshima ni dhahiri pamoja na dhana ya kumuogopa Mungu, kuna maana zaidi kuliko hiyo. Kumcha Mungu kibiblia, kwa muumini, ni pamoja na ufahamu kiasi gani Mungu anachukia dhambi na kuogopa hukumu yake juu ya dhambi hata katika maisha ya Mkristo. Waebrania 12:5-11 inaeleza adhabu ya Mungu ya muumini. Wakati huo huo inafanyika kwa upendo (Waebrania 12:06), bado ni jambo la kutisha. Kama watoto, hofu ya nidhamu kutoka kwa wazazi wetu hakuna shaka huzuia baadhi vitendo viovu. Vile vile lazima pia hiyo iwe katika uhusiano wetu na Mungu. Tunapaswa kuhofu nidhamu yake, na kwa hiyo kutafuta kuishi maisha yetu kwa namna ambayo inayompendeza.

Waumini hawastahili kuwa na hofu kwa Mungu. Sisi hatuna sababu ya kuwa na hofu kwa Mungu. Tuna ahadi yake kwamba hakuna kitu kitakachotutenga na upendo wake (Warumi 8:38-39). Tuna ahadi yake kwamba kamwe hatatutenga wala kutuacha (Waebrania 13:05). Kuogopa Mungu maana yake ni kuwa kama heshima kwake kwamba ina athari kubwa juu ya njia ya kuishi maisha yetu. hofu ya Mungu ni kuwa na heshima kwake na kumtii, kujiwasilisha kwa nidhamu kwake, na kumuabudu katika hofu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nini maana ya kumcha Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries