settings icon
share icon
Swali

Je, ni kibiblia kuuwawa katika Roho?

Jibu


Kwa kawaida, kuwa "kuuwawa katika Roho" hutokea wakati mchungaji anamwekelea mikono mtu, na mtu huyo kuanguka sakafuni, katika kushinda kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Wale ambao huonyesha kuwawa katika Roho hutumia vifungu vya Biblia ambavyo hujadili juu ya watu kuwa "kama wafu" (Ufunuo 1:17) au kuanguka kifudifudi (Ezekieli 1:28; Daniel 8:17-18, 10:7-9). Hata hivyo, kuna idadi tofauti Kibiblia katika huku kuanguka kifudifudi kwa mtu na mazoezi ya kuwa waliouawa katika Roho.

1. Kuanguka chini kibiblia kulikuwa jibu la mtu kwa kile alikiona katika maono au tukio zaidi la matukio ya kawaida, kama vile katika kubadilika kwa Kristo (Mathayo 17:6). Katika mazoezi ya kibiblia ya kuwa waliouawa katika Roho, mtu anaitikia kwa kugusa mwingine au kwa mwendo wa mkono msemaji.

2. Matukio ya Biblia ni chache na kuwa na tofauti kati yao, na wao ilitokea mara chache tu katika maisha ya watu wachache. Katika uzushi wa kuuwawa katika Roho, kuanguka chini ni tukio mara kwa mara na ni jambo linalotokea kwa watu wengi.

3. Katika matukio ya kibiblia, watu huanguka kifudifudi katika hofu aidha kwa yule ambaye au kile wanachokiona. Katika kuuawa kwa Roho bandia, wao huanguka nyuma, ama katika kukabiliana na wimbi la mkono wa msemaji au kama matokeo ya uguzo wa kiongozi wa kanisa (au kusukuma katika baadhi ya matuki mengine).

Sisi hatudai kwamba mifano yote za waliouawa katika Roho ni bandia au majibu ya kugusa au kushinikiza. Watu wengi wanadai kuwa na uzoefu wa nishati au nguvu zinazosababisha wao kuanguka nyuma. Hata hivyo, sisi hatuoni msingi wa kibiblia kwa dhana hii. Naam, kunaweza kuwa baadhi ya nishati au nguvu inayohusika, lakini kama ni hivyo, kuna uwezekano mkubwa sana si za Mungu na si matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Ni bahati mbaya kwamba watu uangalia hizi nguvu bandia za ajabu ambazo hazizalishi matunda ya kiroho, badala ya kutafuta matunda vitendo ambayo Roho anatupa kwa lengo la kumtukuza Kristo kwa maisha yetu (Wagalatia 5:22-23). Kujazwa na Roho si hakuthibitishwi kwa nguvu bandia, lakini kwa kuwa na maisha ya kufurika na neno la Mungu katika namna ambayo linajaa hadi pomoni katika sifa, shukrani, na utii kwa Mungu.

English
Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni kibiblia kuuwawa katika Roho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries