settings icon
share icon
Swali

Mkristo anapaswa kumtendea namna gani rafiki anayejitokeza kuwa yeye ni shoga?

Jibu


Kama Wakristo wanaoishi katika ulimwengu uliongauka, kwa kawaida tutakuwa na marafiki au jamaa kutoka nyanja mbalimbali za maisha. Katika utamaduni wa leo, kuna uwezekano mkubwa kwamba baadhi ya marafiki zetu ambao hawajaokoka watajitokeza hadharani kama “mashaga,” na tunahitaji kuwajibu ipasavyo.

Ni lazima tutambue ukweli fulani kuhusu Mungu na asili ya dhambi ya mwanadamu ili tuwe na mtazamo unaofaa kwa wale walio karibu nasi, ii ikiwa ni pamoja na marafiki wanaotuambia kuwa na wapenzi wa jinsia moja. Kama Wakristo, tunatambua kwamba watu wote wanhitaji upendo na neema, ikiwa ni pamoja na marafiki wanaojitokeza kama mashoga. Na, kama Wakristo, sisi ni mabalozi wa Kristo (2 Wakorintho 5:20). Kupitia Kristo, tuna uhusiano na Mungu aliye hai na tuna tumaini la uzima wa milele ambalo tunaweza kulitoa kwa wengine.

Hatupaswi kukata uhusiano na marafiki ambao hawajaokoka wanaojitokeza kama mashoga. Yesu alishirikiana kwa hiari na wenye dhambi, wakiwemo makahaba na washiriki wa jamii yake (ona Luka 5:30; 7:34). Yesu alimjua Baba yake, na alijua kile kilichokuwa ndani ya mwanadamu (Yohana 2:25). Hilo lilimfanya Yesu awe tayari kuwaongoza wale waliokuwa mbali na mungu hadi kwenye wokovu. Sisi, kama Wakristo, tunaweza kuwa tayari pia, ikiwa tunasoma Biblia na kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu.

Ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu ni mwenye haki na wakati huo huo ana upendo (Kutoka 34:6-7). Mungu hawezi kusamehe dhambi bila dhabihu ya upatanisho ya Mwanawe. Kila dhambi ambayo mtu anafanya lazima ihesabiwe, na haiwezekani kwa mwanadamu kulipa dhambi yake mwenyewe. Ni kwa njia ya Kristo tu ndipo kuna msamaha wa dhambi.

Pia, tunapaswa kufuata amri ya Petro katika kushughulika na wale ambao Mungu anatuma katika maisha yetu, ikiwa ni pamoja na marafiki wanaojitokeza kuwa mashoga: “Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao” (1 Petro 3:15-16). Kwa hivyo tunapaswa kuwa tayari kuwakilisha ukweli kuhusu Mungu, dhambi, na wokovu; tunawakilisha ukweli huo kwa “unyenyekevu na heshima”; na tumtukuze Bwana Yesu Kristo zaidi ya yote.

Marafiki wanaojitokeza kama mashoga wanapaswa kuelewa kwamba msimamo wetu kuhusu ushoga ni msimamo wa Biblia: tabia ya ushoga ni dhambi (ona Warumi 1:26-27). Pia wanapaswa kuelewa kwamba Biblia haielezei ushoga kuwa dhambi “kubwa” au “ndogo” kuliko dhambi nyingi yoyote. Na wanapaswa kujua kwamba, kulingana na Biblia, msamaha wa Mungu unapatikana kwa wote. Injili ni “uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye” (Warumi 1:16).

Rafiki anapotuambia yeye ni shoga, tunapaswa kumwonyesha mtu huyo upendo na heshima bila kuung amkono maisha yake ya ushoga. Tunapaswa kuomba “kwa matumaini kwamba Mungu atawajalia kutubu na kuijua kweli” (2 Timotheo 2:25). Tunapaswa kuhakikisha kuwa tumejazwa na Roho Mtakatifu na kuonyesha tunda la Roho. “Tunamheshimu Kristo kama Bwana” (1 Petro 3:15). Na tunachukua tahadhari kwamba “Maneno [yetu] yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili [sisi] mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu” (Wakolosai 4:6).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo anapaswa kumtendea namna gani rafiki anayejitokeza kuwa yeye ni shoga?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries