settings icon
share icon
Swali

Je! inamaanisha nini kujisalimisha kwa Mungu?

Jibu


Dunia hii ni eneo la vita. Tangu anguko la mwanadamu katika bustani mwa Edeni (Mwanzo 3:17-19), ulimwengu ambao Mungu aliouumba umekuwa katika mgogoro naye (Warumi 8:20-22). Shetani anaitwa “mungu wa ulimwengu huu” (2 Wakorintho 4:4), na kutokana na dhambi ya Adamu, tunazaliwa na dhambi (Warumi 5:12).

Tunapofikia umri ambapo tunaweza kufanya maamuzi ya kiadili, lazima tuchague kama tutafuata mwelekeo wetu unaogemea dhambi au kumtafuta Mungu (ona Yoshua 24:15). Mungu anaahidi kwamba tunapomtafuta kwa mioyo yetu yote tutampata (Yeremia 29:13). Tunapompata, tuna chaguo la kufanya: tutaendelea kufuata mwelekeo wetu, au tunajisalimisha kwa mapenzi Yake?

Kujisalimisha ni neno la kivita. Inamaanisha kuachilia haki zako zote kwa mshindi. Wakati jeshi pinzani linajisalimisha, wanaweka silaha zao chini, ni mshindi anachukua utawala kutoka kwao. Kujisalimisha kwa Mungu hufanyika vivyo hivyo. Mungu ana mpango na maisha yetu, na kujisalimisha kwake ina maana kwamba tunaweka kando mipango yetu wenyewe na kumtafuta kwa shauku. Habari njema ni kwamba mpango wa Mungu kwa ajili yetu daima ni kwa manufaa yetu (Yeremia 29:11), tofauti na mipangao yetu wenyewe ambayo mara nyingi husababisha uharibifu (Mithali 14:12). Bwana wetu ni mshindi mwenye hekima na mwingi wa rehema; anatutawala ili atubariki.

Kuna viwango tofauti vya kujisalimisha, ambavyo vyote vinaathiri uhusiano wetu na Mungu. Kujisalimisha kwa mara ya kwanza kwa kuvutwa na Roho Mtakatifu huongoza hadi wokovu (Yohana 6:44; Matendo 2:21). Wakati tunaachilia majaribu yetu wenyewe ya kupata kibali cha Mungu na kutegemea kazi iliyokamilika ya Yesu Kristo kwa niaba yetu, tunakuwa watoto wa Mungu (Yohana 1:12; 2 Wakorintho 5:21). Lakini kuna nyakati za kujisalimisha zaidi katika maisha ya Mkristo ambao huleta uhusiano wa ndani zaidi na Mungu na nguvu kubwa zaidi katika huduma. Kadri maeneo mengi ya maisha yetu tunavyojisalimisha kwake, ndivyo nafasi inavyoongezeka zaidi ya ujazo wa Roho Mtakatifu (Waefeso 5:18). Tunapojazwa na Roho Mtakatifu, tunaonyesha sifa za tabia yake (Wagalatia 5:22). Kadri tunavyojisalimisha kwa Mungu, ndivyo hali yetu ya zamani ya kujiabudu inabadilishwa na ilie inayofanana Kristo (2 Wakorintho 5:17).

Warumi 6:13 inasema kwamba Mungu anahitaji kwamba tusalimishe kikamilifu nafsi zetu; Anataka sehemu nzima, na sio sehemu: “Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu kwake kama vyombo vya haki.” Yesu alisema kwamba wafuasi wake lazima wajikane wenyewe (Marko 8:34)-wito mwingine wa kujisalimisha.

Lengo la maisha ya Kikistro linaweza kufupishwa na Wagalatia 2:20: “Nimesulubiwa pamoja na Kristo, wala si mimi tena ninayeishi, bali Kristo ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.” Maisha ya kujisalimisha kama hayo ni ya kufurahisha kwa Mungu, yanaleta utimilifu mkubwa zaidi wa kibinadamu, na yatapata thawabu kuu mbinguni (Luka 6:22-23).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! inamaanisha nini kujisalimisha kwa Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries