Swali
Biblia inasemaje nini kuhusu uhalali?
Jibu
Neno "kufuata sheria " halionekani katika Biblia. Ni neno Wakristo hutumia katika kuelezea nafasi ya mafunzo kusisitiza mfumo wa sheria na kanuni kwa ajili ya kufikia zote wokovu na kukua kiroho. Wafuata sheria huamini na kudai uzingatiaji sheria na kanuni wa hali ya juu. Kikanuni ni mafundisho ambayo yamejinafasi kimsingi kinyume na neema. Wale ambao hushikilia nafasi mshika-sheria mara nyingi hushindwa kuona kusudi halisi kwa sheria, hasa lengo la sheria la Agano la Kale la Musa, ambalo linafa kuwa kwetu " kiongozi " au " mwalimu " na kutuleta kwa Kristo (Wagalatia 3:24).
Hata waamini wa kweli wanaweza kuwa wa sheria. Sisi tunaamrishwa, badala yake, tuwe wema kwa sisi wenyewe: "Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake" (Warumi 14:1). Kwa bahati mbaya, kuna wale ambao wanaona kwa nguvu kuhusu mafundisho ya mashirika yasiyo ya muhimu kwamba wao watawashinda wengine kwa ushirika wao, hata kuruhusu usemi wa mtazamo wa mwingine. Kwamba, pia, ni sheria. Wengi wa waumini washika-sheria hii leo hufanya makosa ya kudai kuzingatia yanayoridhisha na tafsiri yao wenyewe ya Biblia na hata mila zao wenyewe. Kwa mfano, kuna wale ambao wanaona kwamba kuwa mmoja wao kiroho lazima uepukane tumbaku, vinywaji, kusakata, sinema , nk . ukweli ni kwamba kuepuka mambo haya sio akikisho la kiroho.
Mtume Paulo anatuonya kuhusu sheria katika Wakolosai 2:20-23 : "Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundihso ya awali ya ulimwengu, kwa nini kukitia chin ya amri, kama weney kuishi duniani, msishike, msionje, msiguse; mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa; hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika naman ya ibada mliyojitungia weneyew, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili." Washika sheria wanaweza kuonekana kuwa waadilifu na kiroho, lakini kufuata sheria hatimaye inashindwa kukamilisha makusudi ya Mungu kwa sababu ni utendaji wa nje badala ya mabadiliko ya ndani.
Ili kuepuka kuanguka katika mtego wa kufuata sheria, tunaweza kuanza kwa kuyashika maneno ya mtume Yohana, "Kwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo"( Yohana 1:17) na kukumbuka kuwa neema, hasa kwa ndugu na dada zetu katika Kristo. "Wewe u nani unayemhukumu mtumish wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha" (Warumi 14:4). "Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wew je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maan sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu"(Warumi 14:10).
Neno la tahadhari ni muhimu hapa. Huku tukistahili kuwa na neema na uvumilivu kwa watu wengine na kukubali tofauti zetu kwa mambo ya uzushi. Sisi pia tunahimizwa kushindania imani kwamba wakati mmoja ilikabidhiwa watakatifu kwa jumla (Yuda 3). Kama tunakumbuka miongozo hii na kuitumia kwa upendo na huruma, tutakuwa salama kutoka kwa sheria na uzushi. "Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani " (1 Yohana 4:1).
English
Biblia inasemaje nini kuhusu uhalali?