settings icon
share icon
Swali

Je, Biblia inaunga mkono desturi ya Kikatoliki ya kubatilisha ndoa?

Jibu


Katika Kanisa la Katoliki, sakramenti saba za Ubatizo, Ekaristi (Ushirika Mtakatifu), Uthibitisho, Wakfu wa Wagonjwa, Upatanisho (Toba), Ndoa, na Daraja Takatifu zinachukuliwa kuwa onyehso la nje la neema ya ndani, iliyowekwa na Kristo. Hizo ni sehemu hasa za wokovu kama vile Kanisa la Katoliki la Kirumi linavyofundisha. Kanisa Katoliki linafundisha kwamba sakramenti zeneyewe— kwa maoni yao ni msingi wa wokovu—haziwezi kutupiliwa mbali kwa urahisi. Iwapo tu sakramenti haikuwa halali tangu ilipotolewa ndipo inaweza kutupiliwa mbali. Kwa kutambua ukweli kwamba hilo linaweza kutokea mara kwa mara, Kanisa Katoliki limeunda mchakato wa kubatilisha ndoa ya Kikatoliki, ambao unatatangaza kuwa sakramenti ni batili tangu mwanzo.

Ubatilishaji unarejelewa ipasavyo kama Tamko la Ubatili. Ingawa inaweza kutumika kwa mojawapo ya sakramenti saba, mara nyingi hutumika kwa ajili ya Ndoa. Kwa kuwa Kanisa la Katoliki hushikilia kwamba wanandoa hawawezi kutalikiana kwa sababu yoyote ile, talaka haitambuliwi na Kanisa la Katoliki kuwa mwisho halali wa ndoa. Kisha inafuata kwamba kasisi wa Kikatoliki hata fungisha ndoa watu waliotalikiwa, hata ikiwa talaka ilitokea kabla ya kujiunga na Kanisa la Katoliki, hata kama talaka ilitokea kabla ya mtaliki kuelewa matokeo yake.

Ubatilishaji unapotolewa haumalizi athari ambazo Kanisa la Katoliki hufundisha hutolewa na sakramenti. Badala yake, ubatilisho unatangaza kwamba sakramenti inayozungumziwa haikuwa halali tangu mwanzo, na mpokeaji anachukuliwa kana kwamba hakuwahi kupokea sakramenti. Hilo halimaanishi kwamba watoto waliozaliwa katika ndoa hiyo sasa huonekana kuwa wamezaliwa nje ya ndoa au kwamba wenzi wa ndoa wa zamani walifanya uasherati wa aina yoyote. Ina maana kwamba upokeaji wa sakramenti ulikuwa na dosari kwa namna fulani.

Ubatilizo hutolewa na Kanisa la Katoliki kwa sababu mbalimbali. Sababu za kawaida zinazowasilishwa kwa mahakama ni ukosefu wa busara, ridhaa yenye kasoro, na kutokuwa na uwezo wa kisaikolojia. Baadhi ya ubatilishaji ni kwa sababu hafifu na mara chache huhusisha zaidi ya kujaza fomu sahihi; kwa mfano, ikiwa mmoja wa washiriki alikuwa na mkataba wa awali (alikuwa ameolewa Kikatoliki) wakati wa harusi. Pia kuna kasoro ya fomu, ambayo inajumuisha ndoa zinazofanywa na mhudumu asiye Mkatoliki au harusi zinasofanywa nje ya Kanisa la Katoliki. Zaidi ya nusu ya ubatilishaji wote uliotolewa ni kwa kasoro ya fomu

Lakini je, dhana ya kubatilisha ndoa ya Kikatoliki ni dhana ya kibiblia? Kuhusu ndoa kuwa sakramenti, tafadhali soma Makala yetu kuhusu sakramenti saba za Kikatoliki (“Je, sakramenti saba za Kikatoliki ni za Kibiblia?”). Wazo la Wakatoliki wa Kirumi la ndoa kama sakramenti yenyewe sio ya kibiblia. Hii inaweka dhana ya ubatilishaji kwenye msingi hati hati. Mafundisho ya Katoliki yana msingi wa Maandiko na pia mapokeo ya Kanisa. Kulingana na maneno ya Yesu, “Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe” (Mathayo 19:6; Marko 10:9) na kulingana na desturi ya kanisa ya mapokeo kwamba kupokea sakramenti hutengeneza alama isiyoweza kufutwa katika nafsi ya mpokeaji. kanisa linafundisha kwamba ndoa HAIWEZI kuisha. Kanisa halipuuzi Mathayo 5:32 na 19:9 inayoruhusu talaka tu katika hali ya uzinzi mwenzi wa ndoa. Hapana, jinsi hili linavyoshughulikiwa inavuruga zaidi. Kulingana na tafsiri moja ya Biblia ya Kikatoliki, andiko la Mathayo 5:32 na 19:9 linasema hivi: “Yeyote anayemtaliki mke wake (Isipokuwa NDOA HARAMU) anamsababisha kufanya uzinzi, na yeyote anyemwoa mwanamke aliyetalikiwa anafanya uzinzi.” Dhana ya “ndoa isiyo halali” haipatikani katika tafsiri zisizo za Kikatoliki; badala yake, Yesu anazungumza juu ya “uasherati (wa ndoa)” “uzinzi,” au “uasherati.” Haionekani kuwa na msingi wowote wa kimaandishi wa uchaguzi wa maneno katika tafsiri ya Kikatoliki, isipokuwa kuunga mkono fundisho la Kanisa Katoliki lenyewe.

Ingawa Yesu alifundisha kwamba talaka iliandikwa tu katia Sheria kwa sababu ya ukaidi wa kibinadamu (Mathayo 19:8) na kwamba nia ya awali ya Mungu ilikuwa kwamba wanandoa wasitengane kamwe (Mwanzo 2:24), Yeye huruhusu talaka katika visa vya za uzinzi/kukosa uaminifu katika ndoa. Mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu ndoa hayapuuzi ukweli huu; badala yake, inatafsiri kimakosa Maandiko ili kuuanga mkono fundisho lake lisilo la kibiblia la ndoa kuwa isiyokwisha, na kisha kuunda machakato wa kubatilisha ili kuruhusu njia iliyoidhinishwa na Kikatoliki kukomesha ndoa hiyo kwa kuitangaza kuwa na batili. Mchakato wa kubatilisha ndoa ya Kikatoliki sio wa kibiblia kwa maana kwamba Yesu aliruhusu tu uzinzi/ukosefu wa uaminifu katika ndoa kuwa msingi wa kukomesha ndoa, na mchakato wa kubatilisha unaruhusu sababu nyingi sana, lakini si kwa sababu moja aliyotaja Yesu. Kanisa Katoliki halikubali sababu pekee ya kibiblia ya talaka kuwa halali na, kwa kweli, huunda orodha mpya ya sababu zisizo za kibiblia za kuvunjika kwa ndoa.

Desturi ya Kanisa Katoliki ya kubatilisha si ya kibiblia. Msingi wake ni wa dhana isiyo ya kibiblia, ile ya sakramenti zinazotoa neema. Kimsingi ni “kuepuka” kutokana na kile ambacho Biblia inafafanua kuwa ndoa. Inapuuza yale ambayo Biblia husema kuhusu ndoa, talaka, na ukosefu wa uaminifu katika ndoa. Kimsingi, desturi ya kikatoliki ya kubatilisha ndoa ni njia isiyo ya kibiblia ya kuepuka fundisho ambalo lenyewe si la kibiblia.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Biblia inaunga mkono desturi ya Kikatoliki ya kubatilisha ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries