settings icon
share icon
Swali

Ni mahali gani pazuri pa kuanzia kusoma Biblia?

Jibu


Kwa kuanzia, ni muhimu kutambua kwamba Biblia si kitabu cha kawaida ambacho husomwa vizuri kutoka bima hadi bima. Kweli ni maktaba, au ukusanyiko, wa vitabu vimeandikwa na waandishi mbalimbali katika lugha kadhaa zaidi ya miaka 1500. Martin Luther alisema kuwa Biblia ni "utoto wa Kristo" kwa sababu historia yote ya Biblia na unabii hatimaye uhakika hulenga Yesu. Kwa hiyo, kusoma kwa kwanza kwa Biblia lazima kuanzie na Injili. Injili ya Marko ni ya haraka na ina ufahamu wa kutosha na ina sehemu nzuri ya kuanzia Basi kutaka kwenda kwenye Injili ya Yohana, ambayo inaangazia katika mambo yote Yesu aliyadai juu yake mwenyewe. Marko anaelezea kuhusu yale Yesu alifanya, wakati Yohana anaelezea kuhusu kile Yesu alisema na Yesu alikuwa nani. Katika Yohana kuna baadhi ya vifungu rahisi na wazi, lakini pia baadhi ya vifungu kamili na vizito zaidi. Kusoma Injili (Mathayo, Marko, Luka, Yohana) itakuwa kujifahamisha na maisha ya Kristo na huduma yake.

Baada ya hayo, zisome baadhi ya Nyaraka (Warumi, Waefeso, Wafilipi). Hizo hutufundisha jinsi ya kuishi maisha yetu kwa njia ambayo ni ya kumheshimu Mungu. unapoanza kusoma Agano la Kale, kisoma kitabu cha Mwanzo. Inatuambia jinsi Mungu alivyoumba ulimwengu na jinsi watu walianguka katika dhambi, kama vile athari za kuanguka zilikuja juu ya dunia. Kutoka, Walawi, Hesabu, Kumbukumbu na zinaweza kuwa ngumu kusoma kwa sababu zinaingia katika sheria zote ambazo Mungu alihitaji Wayahudi kuishi kwayo. Huku haupaswi kuepuka vitabu hivi, ndivyo labda bora Zaidi vimebaki kwa ajili ya utafiti wa baadaye. Katika hali yoyote, jaribu sama isokwame katika hivyo vitabu. Kusoma Yoshua kupitia Mambo ya kupataNyakati ili kupata historia nzuri ya Israeli. Soma Zaburi kupitia Wimbo Ulio Bora itakupatia hisia nzuri ya mashairi ya Kiebrania na hekima. Vitabu vya unabii, Isaya hadi Malaki, inaweza kuwa vigumu kuelewa vile vile. Kumbuka, la muhimu katika kuelewa Biblia ni kuuliza hekima kwa Mungu (Yakobo 1:5). Mungu ndiye mwandishi wa Biblia, na anataka wewe ulielewe neno lake.

Ni muhimu kujua kwamba si kila mtu anaweza kuwa na mafanikio mwanafunzi wa Biblia. Ni wale tu na muhimu "sifa " kwa ajili ya kusoma neno la anaweza kufanya hivyo kwa baraka za Mungu :

Je, umeokolewa kwa imani katika Yesu Kristo (1 Wakorintho 2:14-16)?
Je, wewe una njaa ya neno la Mungu (1 Petro 2:2)?
Je, watafiti neno la Mungu kwa bidii (Matendo 17:11)?

Kama jibu lako ni "naamu” kwa maswali haya matatu, unaweza kuwa na uhakika kwamba Mungu atabariki jitihada zako za kumjua pamoja na neno lake, haijalishi ni wapi utaanzia wala mtindo wako wa utafiti. Kama wewe huna uhakika kwamba wewe ni Mkristo - kwamba umeokolewa kwa imani katika Kristo na Roho Mtakatifu aliye ndani yenu - utapata ni vigumu kuelewa maana ya maneno ya maandiko. Ukweli wa Biblia umesitiriwa kutoka kwa wale ambao hawaja kuja kwa imani katika Kristo, lakini ii uzima yenyewe kwa wale watakao amini (1 Wakorintho 2:13-14, Yohana 6:63).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni mahali gani pazuri pa kuanzia kusoma Biblia?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries