settings icon
share icon
Swali

Kifua cha Abrahamu ni nini?

Jibu


Maneno “Kifua cha Abrahamu” yanapatikana mara moja tu katika Agano Jipya, katika hadithi ya tajiri na Lazaro (Luka 16:19-31), ambapo Yesu alikuwa nafunza. Kuhusu ukweliwa mbingu na kuzimu. Neno la Kigiriki kolpos ambalo linatumika ni gumu kiasi fulani kutafsiri. Kwa mfano, wakati mwingine linafafanuliwa kama “karibu na” Abrahamu au “mikono ya” Abrahamu au “ubavu wa Abrahamu.”

Ni wazi kwamba dhana ya “Kufua cha Abrahamu” ina maana ya kwamba Lazaro alienda mahali pa kupumzika, kuridhika na amani, hivi kwamba Abrahamu (mtu aliyeheshimiwa sana katika historia ya Kiyahudi) alikuwa mlinzi au mlezi. Kinyume chake na la kuhuhuzunisha, tajiri anajipata katika mateso, bila wa kumsaidia au kumfariji.

Kinyume na wazo la wakati huu, Biblia inafunza kwamba mbingu na kuzimu ni mahali halisi. Kila mtu anayeishi ataishi milele katika moja ya sehemu hizi mbili. Hatima hizi mbili zinaonyeshwa hatika hadithi ya Yesu. Wakati tajiri alikua anaishi tu kwa ajili ya siku na lengo lake lilikua maisha humu duniani, Lazaro alivumilia magumu huku akimtumainia Mungu. Kwa hivyo mistari 22 na 23 ni muhimu: “Wakati ukafika yule maskini akafa, nao malaika wakamchukua akae pamoja na Abrahamu. Yule tajiri naye akafa na akazikwa. Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Abrahamu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake.”

Kifo kinaweza kuzingatiwa kuwa utenganisho. Kifo cha kimwili ni mwili kutengana na nafsi/roho, wakati kifo cha kiroho ni nafsi yetu kengana na Mungu. Yesu alifundisha kwamba hatupaswi kuogopa kifo cha kimwili, lakini tunapaswa kuzintatia sana kifo cha kiroho. Kama tunavyosoma katika Luka 12:4-5, Yesu pia alisema, “Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili, lakini baada ya hilo hawawezi kufanya lolote zaidi. Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo!” Matumizi ya Yesu ya maneno “kifua cha Abrahamu” yalikuwa ni sehemu ya mafundisho Yake ili kuelekeza akili za wasikilizaji wake kwa ukweli kwamba chaguo letu la kumtafuta Mungu au kumpuuza hapa duniani huathiri kiasili pale tutakapoishi milele.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kifua cha Abrahamu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries