settings icon
share icon
Swali

Je, inamaanisha nini kukesha na kuomba?

Jibu


Yesu alitumia kifungu cha maneno kesha na kuomba katika matukio kadhaa tofauti. Tukio moja lilikuwa kabale ya kusulubiwa. Yesu aliwachukua wanfunzi Wake hadi kwenye bustani ya Gethsemane, ambako aliomba kwamba “kikombe hiki na kiniondokee” (Mathayo 26:39). Baada ya mombi, aliwakuta wanafunzi wake wamelala. Alihuzunika kwamba hawakuweza hata kusali pamoja Naye kwa muda wa saa moja na akawaonya “Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu” (Mathayo 26:41).

Tukio linguine la kishazi kesha na kuomba kinapatikana katika huduma ya Yesu Alipotabiri kuhusu nyakati za mwisho. Luka sura ya 21 inaeleza kwa undani mengi ya matukio hayo, na Yesu anaonya kwamba yangetukia kwa ghafula: “Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama vile mtego unasavyo” (Luka 21:34). Kisha anasema, “Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu” (aya ya 36).

“Kesheni na kuomba.” Neno lililotafsiriwa “kesha” linamaanisha “kuwa macho kama mlinzi usiku.” Mlinzi wa usiku lazima awe macho zaidi kuliko mlinzi wa mchana. Wakati wa mchana, hatari inaweza kuonekana kwa mbali. Lakini usiku kila kitu ni tofauti. Mlinzi wa usiku lazima atumie hisia mbali na kuona kwa macho ili kugundua hatari. Mara nyingi yuko peke yake gizani na bila kinga ambayo angetumia basi hatakua na cha kutumia. Huenda kunaweza kuwa hakuna dalili za shambulio la adui hadi lifanyike, kwa hivyo lazima awe macho sana, akishuku wakati wowote. Hiyo ndiyo aina ya kukesha ambayo Yesu alizungumza juu yake

Yesu alituonya kwamba tunakengeushwa kwa urahisi sana na mambo ya kimwili na tutanaswa bila kujua ikiwa hatutaendelea kujitia nidhamu. Katika bustani ya Gethsemane, usingizi uliwalemea wanafunzi. Hitaji lao la kimwili lilishinda hamu yao ya kumtii. Alihuzunika alipoona haya, akijua yatakayokuwa mbel yao. Ikiwa hawangebaki macho kiroho, na kukaa ndani Yake (Yohana 15:5) na tayari kuukana mwili, basi wangeshindwa na yule mwovu (1 Petro 5:8).

Wanafunzi wa Yesu hii leo lazima wakeshe na kuomba. Tunakengeushwa kwa urahisi na ulimwengu huu, mahitaji yetu ya kimwili na tamaa, na mipango ya adui (2 Wakorintho 2:11). Tunapoyaondoa macho yetu kutoka kwa Yesu na kurudi Kwake hivi karibuni, maadili yetu huanza kubadilika, umakini wetu unatangatanga, na hivi karibuni tunaishi kama ulimwengu na kuzaa matunda kidogo kwa ufalme wa Mungu (1 Timotheo 6:18-19). Alituonya kwamba ni lazima tuwe tayari wakati wowote kusimama mbele Zake na kutoa hesabu ya maisha yetu (Warumi 14:12; 1 Petro 4:5; Mathayo 12:36).

“Kesheni na kuomba.” Tunaweza tu kubaki waaminifu tunapojitolea kwa maombi. Katika maombi, tunamruhusu Mungu daima atusamehe, atusafishe, atufundishe, atutie nguvu tumtii Yeye (Yohana 14:14). Ili kukesha, ni lazima tuombe kwa ajili ya uvumilivu na uhuru kutoka kwa vikengeusha-fikira (Waebrania 12:2; Luka 18:1; Waefeso 6:18). Ni lazima tuombe bila kukoma (1 Wathesalonike 5:17). Tunapoishi kwa kutazamia kwa hamu kurudi kwa Bwana na kutarajia mateso hadi wakti huo (2 Timotheo 3:12; Mathayo 24:9; 1 Petro 4:12), kuna uwezekano mkubwa wa kuweyaka maisha yetu kuwa safi na mioyo yetu tayari kukutana Naye.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, inamaanisha nini kukesha na kuomba?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries