Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?Swali: "Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?"

Jibu:
Je, unajua kwakweli kua unauzima wa milele na utaenda Mbinguni wakati ukifa? Mungu anataka uwe na uhakika! Bibilia inasema: “Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue yakuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini jina la mwana wa Mungu” (1Yohana 5:13). Kama ungelikuwa umesimama mbele za Mungu saa hii na akuulize, “Kwanini nikuruhusu uingie Mbinguni?” Je, ungelisema nini? Unaweza usijue utajibu nini. Unachohitaji kujua nikwamba Mungu anatupenda na amepeana njia ambapo tunaweza kujua kwakweli ni wapi tutaishi milele.Bibilia inasema hivi “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee,bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Mwanzo kabisa ni sharti tuelewe shida ambayo inatupinga kufika Mbinguni. Shida ni hii- dhambi yetu ya asili inatupinga kuwa na uhusiano na Mungu. Sisi ni wenye dhambi kiasili na kwa chaguo. “Kwasababu wote wamefanya dhambi,na kupungukiwa na utukufu wa Mungu” (Warumi 3:23). Hatuwezi kujiokoa sisi wenyewe. “Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha Mungu. Wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu” (Waefeso 2:8-9). Tunastahili mauti na jehanamu. “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23).

Mungu ni mtakatifu na mwenye haki na nisharti aadhibu dhambi,kisha anatupenda na amepeana msamaha kwa ajili ya dhambi zetu. Yesu alisema “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima. Mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi’’ (Yohana 14:6). Yesu alitufia pale msalabani “Kwa maana Kristo naye alikufa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki,ili atulete kwa Mungu’’ (1Petro 3:18). Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu nakufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki” (Warumi 4:25).

Sasa turudi kwa swali la kwanza – “Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?’’ Jawabu ni - Mwamini Bwana Yesu Kristo nawe utaokoka (Matendo 16:31). Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Unaweza kupokea uzima wa milele kama karama ya bure. “Karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Bwana wetu’’ (Warumi 6:23). Unaweza kuishi maisha yenye ukamilifu na yenye maana sasa hivi. Yesu alisema mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Unaweza kuishi maisha ya milele na Yesu Mbinguni. “Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi,nanyi mwep” (Yohana 14:3).

Ukiwa unataka kumkubali Yesu Kristo kama mwokozi wako na upokee msamaha wa dhambi toka kwa Mungu, hapa kunalo ombi unaweza kuomba. Kwa kuomba ombi hili au ombi lengine lolote lile haitaweza kukuokoa. Nikwakumwamini Yesu Kristo pekee ndiko kutakuwezesha kupokea msamaha wa dhambi. Ombi hili ni njia ya kumwelezea Mungu imani yako kwake na kumshukuru kwa kupeana kwa ajili ya msamaha wako.

“Mungu, najua yakwamba nimefanya dhambi kinyume chako na ninastahili adhabu. Lakini Yesu Kristo akaichukua adhabu ile niliyostahili ili kwa kumwamini yeye nipate kusamehewa. Ninaziacha dhambi zangu kwa kumaanisha na ninaweka imani yangu kwako ili niokolewe. Ahsante kwa neema yako ya ajabu na kwa msamaha! Amina!"

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninawezaje kujua kwakweli nitaenda Mbinguni wakati nikifa?